Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Kuamini watu kupita kiasi:
Naamini kabisa huwezi zungukwa na marafiki muda wote. Kuna wengine wanaokuzunguka si watu wazuri. Mfano watu ambao wanakusengenya na kukusemea mabaya. Watu ambao hawataki mafanikio yako.

Kuruhusu watu wajue mapungufu yako:
Wanafamilia au watu wa karibu pale wanapojua mapungufu yako wanayatumia kama fimbo ya kukuchapia. Angalia sana wa kumweleza mambo yako.
 
Habari zenu wananchi wa Taifa la Jamii Forum, Leo katika kutafakari kwangu nimewaza sana haya maisha kuna ups and down nyingi sana ambazo zingine zina utata sana kutokana na makosa tuliyoyafanya huko way back na unatamani kuwasaidia wengine wasirudie makosa hayo, Ni kosa gani kubwa ulilifanya kipindi cha maisha yako na ungependa wengine wajifunze wasikosee ?
Ndoa niliyowahi kufunga.
 
Kuamini ana chura kufika ndani kumbe kavaa kigodoro.
FqpKUMHWIAMXCvt.jpeg.jpg

Acha ubaguzi mkuu
 
Kukimbilia kuwa na familia mapema kabla sijajiweka vyema kifedha.

Nimekwama mambo mengi ada unastruggle , chakula unastruggle, kodi unstruggle.

Huwezi kujilipua tena unakuwa na limit ya tyme in short ukishakuwa na familia maisha yanabadilika sana.

Bado napambana nije kuishi maisha ya ndoto yangu ingawa mpambano ni mkali sana.
Hii imewakumba wengi
 
Niliwahi kuwa mraibu wa makamari haya ya karata,makamari makubwa ambayo yalinirudisha nyuma kimaendeleo pamoja na kuondoa uaminifu kwa watu ambao ni muhimu sana, majuto ya hali ya juu na maumivu ya hali ya juu zaidi, nilikuwa na marafiki ambao nikiwa na hela na nikiwa nashinda mara kwa mara kwenye hayo makamari huwa wana ni heshimu, kunisifia juu ya uwezo wangu pia na kunikubali kuwa me ni wina,nishavunja {kushinda} sana kwenye makamari makubwa makubwa, ila sijawahi kuingia CASINO na kucheza kamari,ila nikianza kupunwa na kuishiwa kabisa nilikuwa nanyanyasika, kutengwa na mifano mengine ifananayo na hayo,nilitamani saana niache huo mchezo wa haramu, nilishaacha na kurudi mara kwa mara.

Niwahi kuyaona hayo MADUBWI na hata kukaa nayo karibu ila hayo MADUBWI {MABONANZA} sikumbuki kama nishawahi kucheza kwa kuwa siwezi kusubiri mia mbili {200} ambazo zinazotoka mule hata kama zikiwa na uwezo wa kufika Million, napambana na nafsi yangu kule nisirudi, maisha ya mateso na manyanyaso, watu washaliwa hela muhimu. Mtu unaweza kufanya tukio la kuogopeka, kukutana na watu ambao wanafanya shughuri mbali mbali ambazo si za halali.

Naona watu wanasifia tu sijui CHAFU TATU {3}

Nikisema imenirudisha nyuma basi muelewe,na ukipata hela yake sidhani kama unafanyia kitu cha maana.

Piga vita kamari
 
Nilipoteza al
Habari zenu wananchi wa Taifa la Jamii Forum, Leo katika kutafakari kwangu nimewaza sana haya maisha kuna ups and down nyingi sana ambazo zingine zina utata sana kutokana na makosa tuliyoyafanya huko way back na unatamani kuwasaidia wengine wasirudie makosa hayo, Ni kosa gani kubwa ulilifanya kipindi cha maisha yako na ungependa wengine wajifunze wasikosee ?
Most 15milion baada ya kumuoa mwanamke asiye na future wala nini! Mungu mlaani but now nazidi kurecover
 
Daa nina makosa hadi najiona paka,,

Kuchagua kutanyia kazi wilaya ya nyumbani(unaogopa kuchanganyikana)

Kujiunga vicoba,saccos

kuoa kwa kuvuta/pasi kushirikisha

kuoa mapema

Kukopa pesa ndefu

Kubeti pesa ndefu tena kwa wachina(mbaya mnoo)!!

Kumpa uhuru sana mwanamke(mke wangu)

Kukubali kesi(ilikuwa inanikabiri) iishe ili twende kwenye bargain!!(bora ningekaza)!!

kutokupenda kusali,kujumuika na waumini!!
 
Back
Top Bottom