Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Kufanya biashara ya miamala badala ya vifaa vya umeme jumla na reja.
Hakika nakuwaga na majuto kwa kuchelewa kuianza hii biashara.
Nawaza nimepoteza 3 years kwa miamala na hakuna kitu nimevuna.
Nahitaji wakala wa SMP TAA
 
Kukimbilia kuwa na familia mapema kabla sijajiweka vyema kifedha.

Nimekwama mambo mengi ada unastruggle , chakula unastruggle, kodi unstruggle.

Huwezi kujilipua tena unakuwa na limit ya tyme in short ukishakuwa na familia maisha yanabadilika sana.

Bado napambana nije kuishi maisha ya ndoto yangu ingawa mpambano ni mkali sana.
Ahsante kwa ONYO mkuu.
 
Wasia wangu kwa vijana wenzangu, tumieni umri wenu vyema kila moyo wako unapopiga basi umeshapunguza idadi katika ile hesabu maalumu uliyoandikiwa, msihangaikie sana hii dunia kwani kwa namna yeyote hamuwezi kutoka hapa mkiwa hai.

Jambo la pili, mkitaka amani ya kudumu katika nyoyo zenu toeni viumbe wote na mumtie mola wenu aliyewaumba peke yake, hapo atawapatia wenza wazuri na wenye mapenzi kutoka kwake, atawapatia maisha mazuri na yenye kuwatosheleza, atawazidishia furaha na baraka katika maisha yenu, lakini mkirundika virus na bakteria wa kila aina humo ndani mtajuta na mtazidiwa na stress mpaka kupoteza muelekeo jumla.

Mwisho, ninajuta sana kuchelewa kugundua siri ya maisha ya furaha, nimetumia umri wangu kwa sehemu kubwa kuhangaika kuokota mawe kumbe pana mahali almasi zimejaa tele, kwa hasara hii kila mara nawaeleza watu wa karibu na ndugu jamaa na marafiki kuwa wasipate hasara kama niliyopata mimi wajiandae na siku yao ya kufa kwani hapo ndio mwanzo wa maisha ya kweli.
 
Kuamini watu kupita kiasi:
Naamini kabisa huwezi zungukwa na marafiki mda wote. Kuna wengine wanaokuzunguka si watu wazuri. Mfano watu ambao wanakusengenya na kukusemea mabaya. Watu ambao hawataki mafanikio yako. .

Kuruhusu watu wajue mapungufu yako:
Wanafamilia au watu wa karibu pale wanappjua mapungufu yako wanayatumia kama fimbo ya kukuchapia. Angalia sana wa kumwelexa mambo yako. .
NAKAZIA HAPA... Hili ni jambo muhimu sana sana sana..dawa ya hii ni kuwa mkimya kupita kiasi...
 
Kumuamini mtu kupita kiasi kujaribu kumridhisha na kumpenda mtu asieijua dhamani yako kamwe usije kufanya haya mambo utajutia kupoteza muda wako binadamu hawana shukrani
Kosa kubwa sana hil, dah kweli binadamu unamwambia mwenzio huna mbelw wa nyuma kama mche wa sabuni! Hakika kumpenda yule mwanamke ndio lilikuwa kosa kubwa sana
 
Back
Top Bottom