Ni Kosa gani la ovyo ulilowahi kufanya tangu uanze kuendesha gari?

Mkuu ulifanya maamuzi ya faster kwenda pembeni, lasivyo mmh
 
Poleni sana aisee, hospital ni Ikonda eeh
 
Kuna siku natoka dar kwenda moro nipo kwenye coaster,dereva wetu aliovertake roli la mafuta dereva wa roli hilo alitusaidia kwa namna hyo kwa kuingia pembeni na tukapata upenyo maana kulikuwa na semi la mbao lipo speed jamaa alichofanya nikutuwashia taa tu hakupunguza wala nini mbele ya siti ya coaster kulikuwa na wanawake mpaka waliruka kurudi nyuma wakiogopa kukutana uso kwa uso na semi

Baada ya kupata upenyo dereva wetu hakusimama kumshukuru dereva wa roli la mafuta,kumbe jamaa alikasirika sana akawa anatufatilia taratibu ile coaster kwasababu ya kusimama simama sana baadae jamaa alitupata akamtukana sana dereva wetu na akachukua funguo akaondoka nazo,ikabid dereva amfatilie kumbe alienda akazikabiz kituo cha polisi kilichokuwa mbele
 
Duh hatar nilichukua gar ya cousin wangu Sjui kitu balaa niliponda mbele nusu niingie chooni nikapaniki nikaiponda nyuma dah nikaisi Niko naota ndoti
Watu wa hv kuna siku nitapiga mtu lisasi,hujui kitu kwanini uchezee vitu vya watu
 
Ni mimi tu ndio sina hata kimoja hapo.
 
Hii ishanitokeaga zaidi ya mara 6 Mungu tu ananilinda na mara kadhaa nakuwa sipo speed ila ni hatari saaana.

Hadi siku hizi nina utaratibu... Barabara ikiwa na madimbwi tu hata kama hainyeshi nitawasha wiper mpaka nimalize safari hata kama dar mwanza
 
Nilikuwa maeneo ya Tabata relini 2011,ilikuwa imenyesha mvua kubwa sana kwahiyo barabara maeneo yale pamejaa maji kiasi ambapo ukipita taratibu haina shida,mimi nilitokea Buguruni na Suzuki Escudo yangu nikiwa kwenye 80kph,ile kukanyaga maji wimbi la maji likapiga kwenye kioo, sikuweza kuona kitu mbele na gari ikatupwa pembeni,bahati nzuri barabara ina ukingo gari ikagota pale nikafunga brake,kwakweli pale kilichonisaidia ni ule ukingo vinginevyo ningetumbukia kwenye mtaro...
 
ilikuwa mwaka 2014 nimetoka airport nipo na familia naelekea mbezi. mvua ilikuwa inanyesha siku hiyo. nawahi Mbezi beach kulikuwa na issue ya kifamilia. so nipo Mimi Mke, Mtoto na Binti wa kutusaidia kazi. nimefika maeneo ya Hostel za mabibo kwa mbele kulikuwa na maji barabarani... mimi nikakanyaga tu mafuta kwa nguvu nilikuwa speed 100+ so gari ikawa nyepesi . yale maji yalinivuta kushoto ikawa napelekwa kwenye ule mtaro pembeni wa ya barabara na yale maeneo yana mtaro mkubwa sana...ilibidi niwe nafinya brake taratibu huku nimekamata usukani kwa nguvu zote kurudisha gari kulia taratibu.... ilikosa kidogo tu kuingia mtaroni..

wife muda huo alikuwa busy anaangalia Instagram kuja kuangalia mbele anakuta gari inavuta kushoto na imechapa yale maji yameruka kuchafua vioo sioni vizuri...Mungu ni mwema gari ikawa imeelekea kumaliza eneo lenye maji na kukaa sawa..... nikajifanya kama kila kitu kilikuwa sawa...nikakanyaga kibati mpaka riverside huku nikimshukuru Mungu. nikapark pembeni kukagua gari kule chini maana nilihisi pengine kuna vitu vimekatika.... nikaendelea na safari toka siku hiyo nikipita barabarani nikakuta kuna maji hata kama ni kidogo kiasi gani napita kwa adabu sana. niligundua maji yana nguvu sana na si ya kutaka shindana nayo.
 
Hizi sehemu zimetuama maji barabarani huwa naziheshimu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…