Ni Kosa gani la ovyo ulilowahi kufanya tangu uanze kuendesha gari?

Ni Kosa gani la ovyo ulilowahi kufanya tangu uanze kuendesha gari?

View attachment 2183189
Namfukuza Ranger.. Ameshaingia kwenye radar yangu.. Kumbe kuna Lorry mbili kati.. Nikahisi ninaweza kuzimaliza.. Aisee Lorry la kwanza limeisha naona TD42 Civilian inapanda.. Breki nimeshachelewa nitagusa Lorry.. Ikabidi nidownshift gear niingie pembeni..!uzembe..
MUNGU ni mwema..!
Mkuu ulifanya maamuzi ya faster kwenda pembeni, lasivyo mmh
 
Kuna siku parapanda ingelia sema Mungu hakupenda Tu,tulikua tunatoka kumwangalia mgonjwa makete huko hospitali moja ya masista,sasa wakati narudi ilikua usiku tuko na washakaji wawili ebwana mida ya usiku kama saa tano hivi naona Kwa mbele pikipiki imepiga full then Kwa mbele yangu ni overtake Ile nataka Ku overtake lahaulah la Kwata kumbe sio pikipiki ni mbaula imewasha jicho moja then tuko speed aisee kama sio busara za Yule jamaa wa semi trailer ilikua Ile nyimbo yetu maarufu ndungu marafiki na jamaa waimbe.nilitukana sana hii kitu ya kutukana nahisi madereva wote!
Poleni sana aisee, hospital ni Ikonda eeh
 
Daaaah acha kabisa kuna siku nimetoka dar saa 12 jion kuja mwanza niko peke yangu kwenye gari, basi nikafika moro nikaona isiwe shida acha nitafte abiria, bahati nzuri nikapata wa mwanza na shy gari ikakaa level seat.

Mida ya saa tisa usiku nlikuwa singida sehem reli inapishana na barabara, and kabla ya hapo huwa kuna kona ya mushoto sasa nlikuwa nimetanguliza semi nikaona inanichelewesha, usiku nikitaka kuovertake kwenye zero visibility huwa naangalia taa za gari inayokuja mbele yangu nikiona kimya huwa nachomoa tu.

Bwana eeeeh ila nimetokeza tu hivi nipo ubavuni mwa semi katikati gjafla naona semitrail ingine inapandisha ipo speed, jamaa ilibidi tu awe mstaarabu akaitoa nje ila nlikuwa nishakubali yaishe.

Abiria wangu hakuna alojua kitu walikuwa wamelala wote
Kuna siku natoka dar kwenda moro nipo kwenye coaster,dereva wetu aliovertake roli la mafuta dereva wa roli hilo alitusaidia kwa namna hyo kwa kuingia pembeni na tukapata upenyo maana kulikuwa na semi la mbao lipo speed jamaa alichofanya nikutuwashia taa tu hakupunguza wala nini mbele ya siti ya coaster kulikuwa na wanawake mpaka waliruka kurudi nyuma wakiogopa kukutana uso kwa uso na semi

Baada ya kupata upenyo dereva wetu hakusimama kumshukuru dereva wa roli la mafuta,kumbe jamaa alikasirika sana akawa anatufatilia taratibu ile coaster kwasababu ya kusimama simama sana baadae jamaa alitupata akamtukana sana dereva wetu na akachukua funguo akaondoka nazo,ikabid dereva amfatilie kumbe alienda akazikabiz kituo cha polisi kilichokuwa mbele
 
Duh hatar nilichukua gar ya cousin wangu Sjui kitu balaa niliponda mbele nusu niingie chooni nikapaniki nikaiponda nyuma dah nikaisi Niko naota ndoti
Watu wa hv kuna siku nitapiga mtu lisasi,hujui kitu kwanini uchezee vitu vya watu
 
Haaa...[emoji28][emoji28][emoji28]
Tuache kidogo...
Humu kila mtu ana ndinga kali.
Kila mtu ana kazi au biashara nzuri..
Kila mtu ni handsome [emoji85]
Kila mwanadada ni pisi kali..
Kila mtu ana nyumba
Kila mtu amesoma moaka university..

Yaani humu hamna mnyonge..[emoji28][emoji28][emoji28]
Ni mimi tu ndio sina hata kimoja hapo.
 
Me mwaka 2020 hapo nipo na gari jipya (kwangu jipya), sasa nikaona ngoja nilionje maana speed 260 wapi hapa Dar nitaitest, nikaenda Tanga kupitia Bagamoyo.

Baada ya siku mbili nikarudi. Sasa njiani nikasema ngoja nijaribu kupiga kibati hadi mwisho. Mvua ilikua imetoka kunyesha barabara ina madimbwi dimbwi ya maji.

Nikatafuta mahali njia imenyooka. Bwana nikakoleza kibati hadi 200 hivi. Kwa bahati mbaya nikapishana na Roli kubwa sasa ile likarusha maji yakajaa kwenye kioo cha mbele.

Ile kupanic nikataka kuwasha wiper zipunguze maji, sasa hapo nimetoka kutumia gari la Toyota nimehamia Mjerumani, aisee Toyota wipers zipo kushoto hafu taa kulia, mjerumani kinyume chake, dah aisee nilipanic sioni kitu mbele hafu nipo kibati mbaya.

Nashukuru Mungu njia ilikua imenyooka na haina magari zaidi ya ilo roli tuliopishana. Ilipokuja kukubali wipers nilirudisha speed maximum 80 aisee.
Hii ishanitokeaga zaidi ya mara 6 Mungu tu ananilinda na mara kadhaa nakuwa sipo speed ila ni hatari saaana.

Hadi siku hizi nina utaratibu... Barabara ikiwa na madimbwi tu hata kama hainyeshi nitawasha wiper mpaka nimalize safari hata kama dar mwanza
 
Nilikuwa maeneo ya Tabata relini 2011,ilikuwa imenyesha mvua kubwa sana kwahiyo barabara maeneo yale pamejaa maji kiasi ambapo ukipita taratibu haina shida,mimi nilitokea Buguruni na Suzuki Escudo yangu nikiwa kwenye 80kph,ile kukanyaga maji wimbi la maji likapiga kwenye kioo, sikuweza kuona kitu mbele na gari ikatupwa pembeni,bahati nzuri barabara ina ukingo gari ikagota pale nikafunga brake,kwakweli pale kilichonisaidia ni ule ukingo vinginevyo ningetumbukia kwenye mtaro...
 
ilikuwa mwaka 2014 nimetoka airport nipo na familia naelekea mbezi. mvua ilikuwa inanyesha siku hiyo. nawahi Mbezi beach kulikuwa na issue ya kifamilia. so nipo Mimi Mke, Mtoto na Binti wa kutusaidia kazi. nimefika maeneo ya Hostel za mabibo kwa mbele kulikuwa na maji barabarani... mimi nikakanyaga tu mafuta kwa nguvu nilikuwa speed 100+ so gari ikawa nyepesi . yale maji yalinivuta kushoto ikawa napelekwa kwenye ule mtaro pembeni wa ya barabara na yale maeneo yana mtaro mkubwa sana...ilibidi niwe nafinya brake taratibu huku nimekamata usukani kwa nguvu zote kurudisha gari kulia taratibu.... ilikosa kidogo tu kuingia mtaroni..

wife muda huo alikuwa busy anaangalia Instagram kuja kuangalia mbele anakuta gari inavuta kushoto na imechapa yale maji yameruka kuchafua vioo sioni vizuri...Mungu ni mwema gari ikawa imeelekea kumaliza eneo lenye maji na kukaa sawa..... nikajifanya kama kila kitu kilikuwa sawa...nikakanyaga kibati mpaka riverside huku nikimshukuru Mungu. nikapark pembeni kukagua gari kule chini maana nilihisi pengine kuna vitu vimekatika.... nikaendelea na safari toka siku hiyo nikipita barabarani nikakuta kuna maji hata kama ni kidogo kiasi gani napita kwa adabu sana. niligundua maji yana nguvu sana na si ya kutaka shindana nayo.
 
Hizi sehemu zimetuama maji barabarani huwa naziheshimu sana.
 
Back
Top Bottom