Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Kumwamini fundi
na kumwachia pesa
na kujenga bila mimi kumsimamia au kuwepo

Ni kosa kubwa sana kwa mafundi hawa wa sasa hivi.
Materials nilikuwa nanunua mimi mwenyewe na uzuri nina idea za ufundi ilikuwa si rahisi kunidanganya

Wakati naanza ujenzi alikuta tayari nimeshanunua tofali, kokoto na mchanga. Cement na nondo nilikuwa nimeshazilipia tayari hardware ya jirani
 
Ramani za wenzetu mbele huko store kwao sio muhimu kama laundry room ona hapo chumba cha katikati ya jiko na public toilet ni laundry room, mbongo angefanya hiyo iwe ni store

Halafu jiko ni open kitchen saafi kabisa.

Ramani simple na imejitosheleza kwa wale wa kipato cha kawaida inawafaa
 
Point muhimu
 
Panda mti
 
Wewe ndo mshamba kwa kuona uchaguzi wa wenzako wa kishamba wako ndo bora zaidi.

Wewe kama unapenda ndogo ni wewe. Waache wanaopenda kubwa wafanye wakipendacho.
Huyo jamaa anapenda nyumba ndogo kama kilinge
 
Mkuu Naomba ramani PM
Ukipata ni PM na mimi, ila sio kila ramani ipo poa. Kuna moja niliiona ya mkenya nikitukia namtafuta mtaalam atengeze structral drawing na badiliko modification kidogo kukidhi vionjo vyangu. Huwa narndelea kuangalia ipi bora zaidi, mpaka nikianza niwe nimapata hasa bora kuliko
 
kufanya wiring mbili ni nzuri zaidi, Bomba ni moja ila zinapitisha wires za Tanesco na hizo za Solar! Inapendeza zaidi
Yes. Mana kuweka inverter, kuzuia matumizi ya vitu kama pasi umeme ukikatika ni ngumu na italeta usumbufu
 
Kosa ni lako, kabla ya kuanza ujenzi ilipaswa uangalie mrejesho wa ramani. Hii ni lazima, hata huyo uliemkabidhi ilipaswa akuhoji vitu flan ili ajue ukubwa wa chumba. Mfano chumba cha watoto unataka vikae vitanda vingapi vya ukubwa gani? Hivyo
 
Hata hiyo ndogo inajengwa vizuri hewa unapata, unaeeka madilisha ya nguvu ukilala kama upo nje. Wewe unasemea nyumba enzi za wazee wetu vidiridha milango ilikuwa midogo. Hiyo nyumba ya 83 m3 ni kali ukiijulia wapi uiweke na vipi. Nikijenga hiyo hapo mbele naweza fanya midifikation kidogo ili mlango wa kuingilia usianzie dinning.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…