Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Khaaa!! Mkuu ndio hukumtia hata kofi ???
 

Asante kwa maelezo mazuri. Na solar yenye ukubwa gani naweza kufunga ili kutumia kwenye vifaa vya kawaida kama pasi, TV nk? Umesema hapo nikifunga invertor sina sababu ya kubadilisha taa, maana yake hata vifaa vingine naweza kutumia kwa hiyo solar?

Somo la solar haijanikaa vizuri.
 
Mnaejenga mijumba mikubwa mjitafakari mambo yamebadilika siku hizi hakuna kutembeleana ovyo wala kuishi kwa ndugu kama zamani na watoto wakikua wanakimbilia sehemu nyingine kutafuta maisha ,kwahiyo utabaki na jumba kubwa kama msikiti peke yako
Mi napenda mjumba mkubwa asee mambo ya kubanana hapana...acha hao watoto wasepe
 
Eeeheehe ukafanyaje sasa hapo?
 
Hili Jambo ni muhimu. Inabidi tuulize wataalam nisije kurudia kosa.
Kwa sasa,kulingana na mambo ya mgao wa umeme, kuwa na mfumo wa solar ni muhimu sana.
Mfumo wa solar utatumia hiyohiyo wiring kwa mtu mwenye uwezo kwa kuweka inverter na change over switch ili kubadili tanesco/solar, vyote hivyo vitahitaji distribution network mapema ikiwa ni sehemu ya battery,inverter na solar yenyewe.


Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Mfumo wa solar ni pesa yako tu kila kitu unaweza unganisha,
Ila vitu vinavyotumia umeme mkubwa kama pasi,jiko huongeza gharama za solar upande wa battery, solar, inverter na charger controller,
Lakini kwa mfumo rahisi unaweka uthibiti wasitumie hivyo vitu pindi unapotumia solar

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…