Ujenzi hautakiwi kukurupuka. Na usisubiri upate pesa ndipo uplan ujenzi wako utaanzaje. Muda mzuri wa kuplan nyumba ni pale ukiwa hauna hata mia mfukoni. Akili huwa inafanya kazi vizuri sana.
Haya ni mambo ya msingi ya kuyatafakari na haitakugharimu kuyafanya:
1. Kadiria mahitaji ya makazi yako je ni ya kudumu au unajenga makazi ya mpito huku ukiwa na plan ya kujenga makazi mengine ya retirement.
Mfano, unaweza kwa sasa kulingana na mazingira yako na hali ya uchumi ukawa unaona inakugharimu sana kupanga nyumba au kuishi kwa ndugu au nyumba ya familia so unahitaji kupata sehemu yako ya kuwa huru kwa muda ili uweze hata kupanga maisha yako vizuri. Hii itakusaidia ni ujenzi gani utafanya.
2. Ukishajua ni aina gani ya ujenzi unataka kufanya itakusaidia kujua ni ukubwa gani wa eneo utaanza nalo. Mfano unaweza kuwa unataka makazi ya mpito so hata eneo la Meter 15 kwa 30 likawa ni sawa tu maana unajenga makazi ya kukuficha kwa muda wakati ukikusanya nguvu za kuanzisha sasa makazi ya kudumu au retirement home.
Au unaweza ukawa unataka kuanza straight ujenzi wa makazi ya kudumu so hata eneo utakalohitaji litatakiwa kuwa kubwa kwa size mfano meter 80 kwa 80 au hata ekari moja kulingana na mipangilio yako.
3. Ukishafahamu aina ya ujenzi unataka kufanya na eneo linalohitajika utakuwa sasa na nafasi ya kupangilia mkao wa makazi yako kwa mazingira ya nje na ndani. Nyumba itakaa kona gani au eneo gani. Makaro ya maji yatakaa wapi, tenki la maji utaweka wapi, parking ya gari ni wapi, na landscaping itakaa mkao gani geti litakaa upande gani na kadharika.
4. Jambo lingine muhimu la kutazama wakati utakuwa umeshajua makazi unajenga na mpangilio ni mahitaji yako. Kosa ambalo huwa linafanyika ni kuwahi kumaliza nyumba ili kuhamia ila tunasahau features za hiyo nyumba. Matokeo yake ndio unaingia katika nyumba inakosa sifa za kuwa nyumbani (home [emoji537] [emoji536]) inabakia kuwa jengo yaani building. Hii ndio inakufanya hata ukianza kuishi hapo mahala ukose amani na utulivu matokeo yake unaanza kupata msongo wa mawazo ukiwa kwako na hata furaha ya kuishi hauoni ila unashangaa ukienda kwa rafiki yako ambaye alituliza kichwa wakati wa ujenzi unapata amani sana katika makazi yake hadi unatamani mbadilishane makazi akupe kwake ubakie.
5. Vema sana kuchagua location nzuri ya makazi kulingana na mahitaji yako ya makazi. Mfano unanunua kiwanja uswahilini au high density area ila wewe si mtu wa kujichanganya na haupendi makelele, mazoea ya hovyo, kelele za muziki sijui Bar kelele za hovyo. Kuna maeneo ambapo ukienda kujenga na kuishi utasema upo ikulu. Kupo kimya hautasikia sauti ya msikiti, wala walokole wakiimba mapambio wala kelele za wala bata.
6. Ni vema kujua nyumba utaidesign vipi na hii ni rahisi na unaweza ifanya wewe mwenyewe hapo ulipo muda huu ukiwa hauna hata mia. Yaani ni simple, kwa kuchukua penseli na karatasi kisha jaribu kuingia mtandaoni na kutazama 3d plans za mijengo kulingana na idadi ya vyumba. Kisha kaa chini fanya rough sketch ya aina ya mpangilio wa nyumba utakuwa kisha chukua huo mchoro au michoro kaa na watu wenye akili timamu wanaoweza kutoa dosari na kukwambia hapa futa weka hivi kwa sababu moja mbili tatu ili kupata matokeo mazuri. Usiogope ni mara ngapi itakulazimu kufuta na kuchora tena sababu haikuhitaji kuwa mtaalamu wa uchoraji kufanya ni kazi ya kitoto sana hata darasa la pili wanaweza kuifanya.
7. Ukishachora na kufuta mara nyingi uwezavyo ma kujua michoro yako itakaaje na umejiridhisha kuwa hapa sasa huu mpangilio ni zero errors katika ujenzi then chukua huo mchoro tafuta hawa madogo wasanifu majengo wa mtandaoni ambao mnaweza kuonana na kuketi chini mkazungumza juu ya kuchora sasa ramani yenye mchoro wa 3d, Cost estimations (BOQ),na vipimo kabisa. Then mzungumze bei ya kukufanyia design ya aina ya mjengo unataka. Huo mjengo utamwambia sifa zake kama unataka zile za hidden roof au za mgongo wa tembo, unataka ghorofa au nyumba ya chini. Then muachie yeye sasa utundu wa kudesign muonekano mzuri kulingana na original idea ya mpango makazi wako.
Kuhusu swala la gharama tazama namna utazungumza nae na kama utaona ni kazi tafuta mtu unayemuamini akusaidie kunegotiate nae bei ya gharama ya usanifu. Wapo wanaoweza kufanya kwa 50,000,100,000,200,000,300,000 hadi laki 500,000. Jitahidi muongee na kuelewana kulingana na uwezekano wa kuifanya kazi yenyewe maana unaweza kuwa na maelekezo mengi sana kiasi kwamba akataka pesa ya juu ili akufanyie kazi nzuri,au ukawa very simple na direct hadi akawa hana kazi kubwa sana.
[emoji779]Angalizo fanya kazi na wasanifu majengo wasio kuwa na makampuni ya ujenzi ambayo yapo busy na ujenzi maana hawa wanakuwaga wajuaji sana na unaweza shangaa anakupangia nyumba kwa matakwa yake badala yako sababu ya Ego. Mimi nimepishana na kuwakataa wengi kwa tabia za ujuaji na kulazimisha ufuate anachotaka yeye kwa design zake na ukimuelekeza unachotaka anakuwa anafanya kazi kama analazimishwa na anataka bei iwe juu. Hawasikilizi mteja then wacustomize michoro kwa kuproject matakwa ya mteja.
8. Utakafanikiwa kumalizana na msanifu majengo then utakuwa umeshapata picha ya ujenzi wako utakwendaje kuanzia gharama zake na namna utafanyika. Huyu anayekuchorea atakuelekeza na kukupa plan ya phases au hatua za ujenzi ambazo hizi zitakusaidia kama utaamua kusimamia ujenzi wewe mwenyewe though ni vema kuwa na mkeo, mumeo wakati wa kupanga haya ili msaidiane kwenye ujenzi eneo la usimamizi au engineering incase hauwezi kumudu kuajiri mtu kusimamia ujenzi wako ila kama unae then mtaketi na kupanga nae namna kazi itaenda.
9. Ukishajua kuwa umetimizia haya itakuwa rahisi sasa kusema upo tayari kuanza ujenzi maana unampango mkakati wa kueleweka sasa kila utakachofanya hapa kitareflect au akisi Plan yako ya ujenzi makazi na sio kukurupuka kurupu kwa kushauriwa na kila mtu au kufuata mkumbo. Unasikia watu wananunua viwanja unakurupuka kuwahi chako kisha baadae unajiuliza why ulikurupuka kununua. Au unaanza ujenzi halafu umefika kwenye rinta unaanza jilaumu kuwa ungefanya hiki ama kile baada ya kutembelea site na washkaji na kuona dosari au kuona designs za wenzako.
Ujenzi hautaki pupa though unaweza kwenda haraka kama umejiandaa vema na kwa akili wasababu ukikosea kubomoa ni gharama na itakuuma na kuendelea ni maumivu maana unaona kabisa namna umevagaa majanga. So be very careful katika mipango yako ikiwa kwa wakati huu hauna hata kiwanja unaweza anza kupanga sasa na ukafanya kitu kizuri sana baadae.
Oh halafu nilisahau, pia zingatia sana gharama za ujenzi ili usiumie kama wengine waliokurupuka kwa kutafiti kwanza bei za manunuzi. Unaweza pata deal nzuri ya cement,tofali,nondo mbao na kadhalika kama utapeleleza vizuri na kukutana na wadau sahihi na ukakata bajeti yake chini kwa hata 60% ya cost ya original plan. Hii itategemea na wewe sasa na utafiti wako unafanyaje na unafanyia wapi. Ila kuwa makini tu usijeuziwa mali za wizi au utapeli. So kuwa makini.