Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ujenzi hautakiwi kukurupuka. Na usisubiri upate pesa ndipo uplan ujenzi wako utaanzaje. Muda mzuri wa kuplan nyumba ni pale ukiwa hauna hata mia mfukoni. Akili huwa inafanya kazi vizuri sana.

Haya ni mambo ya msingi ya kuyatafakari na haitakugharimu kuyafanya:

1. Kadiria mahitaji ya makazi yako je ni ya kudumu au unajenga makazi ya mpito huku ukiwa na plan ya kujenga makazi mengine ya retirement.

Mfano, unaweza kwa sasa kulingana na mazingira yako na hali ya uchumi ukawa unaona inakugharimu sana kupanga nyumba au kuishi kwa ndugu au nyumba ya familia so unahitaji kupata sehemu yako ya kuwa huru kwa muda ili uweze hata kupanga maisha yako vizuri. Hii itakusaidia ni ujenzi gani utafanya.


2. Ukishajua ni aina gani ya ujenzi unataka kufanya itakusaidia kujua ni ukubwa gani wa eneo utaanza nalo. Mfano unaweza kuwa unataka makazi ya mpito so hata eneo la Meter 15 kwa 30 likawa ni sawa tu maana unajenga makazi ya kukuficha kwa muda wakati ukikusanya nguvu za kuanzisha sasa makazi ya kudumu au retirement home.

Au unaweza ukawa unataka kuanza straight ujenzi wa makazi ya kudumu so hata eneo utakalohitaji litatakiwa kuwa kubwa kwa size mfano meter 80 kwa 80 au hata ekari moja kulingana na mipangilio yako.

3. Ukishafahamu aina ya ujenzi unataka kufanya na eneo linalohitajika utakuwa sasa na nafasi ya kupangilia mkao wa makazi yako kwa mazingira ya nje na ndani. Nyumba itakaa kona gani au eneo gani. Makaro ya maji yatakaa wapi, tenki la maji utaweka wapi, parking ya gari ni wapi, na landscaping itakaa mkao gani geti litakaa upande gani na kadharika.

4. Jambo lingine muhimu la kutazama wakati utakuwa umeshajua makazi unajenga na mpangilio ni mahitaji yako. Kosa ambalo huwa linafanyika ni kuwahi kumaliza nyumba ili kuhamia ila tunasahau features za hiyo nyumba. Matokeo yake ndio unaingia katika nyumba inakosa sifa za kuwa nyumbani (home [emoji537] [emoji536]) inabakia kuwa jengo yaani building. Hii ndio inakufanya hata ukianza kuishi hapo mahala ukose amani na utulivu matokeo yake unaanza kupata msongo wa mawazo ukiwa kwako na hata furaha ya kuishi hauoni ila unashangaa ukienda kwa rafiki yako ambaye alituliza kichwa wakati wa ujenzi unapata amani sana katika makazi yake hadi unatamani mbadilishane makazi akupe kwake ubakie.


5. Vema sana kuchagua location nzuri ya makazi kulingana na mahitaji yako ya makazi. Mfano unanunua kiwanja uswahilini au high density area ila wewe si mtu wa kujichanganya na haupendi makelele, mazoea ya hovyo, kelele za muziki sijui Bar kelele za hovyo. Kuna maeneo ambapo ukienda kujenga na kuishi utasema upo ikulu. Kupo kimya hautasikia sauti ya msikiti, wala walokole wakiimba mapambio wala kelele za wala bata.

6. Ni vema kujua nyumba utaidesign vipi na hii ni rahisi na unaweza ifanya wewe mwenyewe hapo ulipo muda huu ukiwa hauna hata mia. Yaani ni simple, kwa kuchukua penseli na karatasi kisha jaribu kuingia mtandaoni na kutazama 3d plans za mijengo kulingana na idadi ya vyumba. Kisha kaa chini fanya rough sketch ya aina ya mpangilio wa nyumba utakuwa kisha chukua huo mchoro au michoro kaa na watu wenye akili timamu wanaoweza kutoa dosari na kukwambia hapa futa weka hivi kwa sababu moja mbili tatu ili kupata matokeo mazuri. Usiogope ni mara ngapi itakulazimu kufuta na kuchora tena sababu haikuhitaji kuwa mtaalamu wa uchoraji kufanya ni kazi ya kitoto sana hata darasa la pili wanaweza kuifanya.

7. Ukishachora na kufuta mara nyingi uwezavyo ma kujua michoro yako itakaaje na umejiridhisha kuwa hapa sasa huu mpangilio ni zero errors katika ujenzi then chukua huo mchoro tafuta hawa madogo wasanifu majengo wa mtandaoni ambao mnaweza kuonana na kuketi chini mkazungumza juu ya kuchora sasa ramani yenye mchoro wa 3d, Cost estimations (BOQ),na vipimo kabisa. Then mzungumze bei ya kukufanyia design ya aina ya mjengo unataka. Huo mjengo utamwambia sifa zake kama unataka zile za hidden roof au za mgongo wa tembo, unataka ghorofa au nyumba ya chini. Then muachie yeye sasa utundu wa kudesign muonekano mzuri kulingana na original idea ya mpango makazi wako.

Kuhusu swala la gharama tazama namna utazungumza nae na kama utaona ni kazi tafuta mtu unayemuamini akusaidie kunegotiate nae bei ya gharama ya usanifu. Wapo wanaoweza kufanya kwa 50,000,100,000,200,000,300,000 hadi laki 500,000. Jitahidi muongee na kuelewana kulingana na uwezekano wa kuifanya kazi yenyewe maana unaweza kuwa na maelekezo mengi sana kiasi kwamba akataka pesa ya juu ili akufanyie kazi nzuri,au ukawa very simple na direct hadi akawa hana kazi kubwa sana.

[emoji779]Angalizo fanya kazi na wasanifu majengo wasio kuwa na makampuni ya ujenzi ambayo yapo busy na ujenzi maana hawa wanakuwaga wajuaji sana na unaweza shangaa anakupangia nyumba kwa matakwa yake badala yako sababu ya Ego. Mimi nimepishana na kuwakataa wengi kwa tabia za ujuaji na kulazimisha ufuate anachotaka yeye kwa design zake na ukimuelekeza unachotaka anakuwa anafanya kazi kama analazimishwa na anataka bei iwe juu. Hawasikilizi mteja then wacustomize michoro kwa kuproject matakwa ya mteja.

8. Utakafanikiwa kumalizana na msanifu majengo then utakuwa umeshapata picha ya ujenzi wako utakwendaje kuanzia gharama zake na namna utafanyika. Huyu anayekuchorea atakuelekeza na kukupa plan ya phases au hatua za ujenzi ambazo hizi zitakusaidia kama utaamua kusimamia ujenzi wewe mwenyewe though ni vema kuwa na mkeo, mumeo wakati wa kupanga haya ili msaidiane kwenye ujenzi eneo la usimamizi au engineering incase hauwezi kumudu kuajiri mtu kusimamia ujenzi wako ila kama unae then mtaketi na kupanga nae namna kazi itaenda.

9. Ukishajua kuwa umetimizia haya itakuwa rahisi sasa kusema upo tayari kuanza ujenzi maana unampango mkakati wa kueleweka sasa kila utakachofanya hapa kitareflect au akisi Plan yako ya ujenzi makazi na sio kukurupuka kurupu kwa kushauriwa na kila mtu au kufuata mkumbo. Unasikia watu wananunua viwanja unakurupuka kuwahi chako kisha baadae unajiuliza why ulikurupuka kununua. Au unaanza ujenzi halafu umefika kwenye rinta unaanza jilaumu kuwa ungefanya hiki ama kile baada ya kutembelea site na washkaji na kuona dosari au kuona designs za wenzako.

Ujenzi hautaki pupa though unaweza kwenda haraka kama umejiandaa vema na kwa akili wasababu ukikosea kubomoa ni gharama na itakuuma na kuendelea ni maumivu maana unaona kabisa namna umevagaa majanga. So be very careful katika mipango yako ikiwa kwa wakati huu hauna hata kiwanja unaweza anza kupanga sasa na ukafanya kitu kizuri sana baadae.

Oh halafu nilisahau, pia zingatia sana gharama za ujenzi ili usiumie kama wengine waliokurupuka kwa kutafiti kwanza bei za manunuzi. Unaweza pata deal nzuri ya cement,tofali,nondo mbao na kadhalika kama utapeleleza vizuri na kukutana na wadau sahihi na ukakata bajeti yake chini kwa hata 60% ya cost ya original plan. Hii itategemea na wewe sasa na utafiti wako unafanyaje na unafanyia wapi. Ila kuwa makini tu usijeuziwa mali za wizi au utapeli. So kuwa makini.
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Ilibakia kidogo niingie huu msala. Fundi alinitamanisha Kwa kuwa tofali za msingi zillingia nyingi sana so Kwa ndani chooni kulikuwa na shimo kubwa
Self container ndani choo shimo bado ( mr ebo voice)
 
Nilikuwa wa kwanza kujenga nyumba sehemu ambayo ilikuwa imepanuliwa kuwa sehemu ya jiji la Mwanza sehemu za Mkolani. Nikajenga nyumba yangu kubwa ya kisasa kwa gharama kubwa sana hasa kwa vile ilinilazimu kujivutia maji na umeme mwenyewe. Baada ya miaka 15 eneo likavamaiwa na ujenzi holela wao wakiuita upimaji shirikishi na hivyo jumba langu kuzungukwa na vijumba visivyo na mpangilio kiasi kuwa hata njia ya kwenda nyumbani kwangu haipo tena inabidi nizunguke zunguke kwa kubahatisha hadi kufika nyumbani.

Ushauri wangu ni kwamba epuka kujenga eneo ambalo halijajengwa kwani hujui litakuja kujengwa vipi.
Sijui kwa nini hakuna mtu mwingine aliyewahi kukumbana na kadhia hii ambayo nusura inipe ugonjwa wa moyo!
 
Kwa mafundi wetu hawa wa tujenge tupumzike bila usimamizi wako mwenyewe wanapojenga ujue.

1. Utajengewa chini ya Kiwango, kwakuwa ni wavivu na kupenda kulipua kazi hata kama wamelipwa vizuri.

2. Utaibiwa raslimali za ujenzi iwe simenti, mbao, Nondo, misumali yaani kila kilichopo hapo.

Lazima uwepo wakati wa Ujenzi.
Kwa utafiti wangu mafundi ujenzi wote ni wezi wanapishana kwa viwango tu.
Kumbukeni hata kuchukua msumari mmoja bila ruhusa ya mwenyewe ni wizi.
Fundi wa kiswahil usipokuwepo wakat wa kaz.analipua.wachache sana wanafata vigezo.inabdi hata kama huna muda jenga kila unapopata kalikizo unakatumia effectively unakomaa site mwanzo mwisho.
 
Haya nyumba hii hapa 83 SQm ,ni matumizi mabaya sana ya akili na pesa kujenga nyumba ya vyumba 3 kwa SQM 150 ama 200 ni poor mind!,mwisho wa siku unatumia gharama kubwa pesa ambayo ilitakiwa uwekeze sehemu nyingine![emoji276],ni maaajabu sana tena sana kwa mtu mwenye kipato cha kati kujenga nyumba ya SQM 150 yenye vyumba 3,kuanzia SQM 150 kuendelea hiyo ni Guest house View attachment 2468926
Umetumia kanuni ipi ya hesabu iliyokupa jibu kwa hiyo nyumba ni sq 83 na kwa hivyo vipimo ulivyoambatanisha kwenye ramani yako
 
Hujui ujenzi ukiingia utaelewa...

Ngoja nikusaidie msingi tu wenye mzunguko wa tofali 400 mara kozi 7 ni tofali 2800 za kulaza. Boma ni idadi hiyo hiyo ya mzunguko wa msingi yaani 400× kozi 17 = 6800 mpaka kufikia slab/ renta ukumbuke zote zimelazwa then juu mzunguko ni huohuo tena ila hapa ni za kusimama nchi 5 kama ni ghorofa moja ila kozi zinakuwa 10 piga hesabu na huku nilipunguza idadi ya kuta kupata nachotaka zilitumika 2100+ bado kuna vitu vingi sana sijagusia... ukiona mtu kaweka floor kadhaa mpe heshima yake.
Hamna nyumba utajenga na tofali kiasi hichoo
 
Nimejenga uelekeo wa jua linapochomoza na jua linapozama yaani ilo joto lake full shangwe mchana hakukaliki jua linapiga sebuleni na chumbani kwangu usiku napo hakulaliki.mafundi vimeo sana wanashindwa hata kutoa ushauri
Hapo tatizo ni kiwanja kilivyo kaa au wewe mwenyewe.
 
Nimejenga uelekeo wa jua linapochomoza na jua linapozama yaani ilo joto lake full shangwe mchana hakukaliki jua linapiga sebuleni na chumbani kwangu usiku napo hakulaliki.mafundi vimeo sana wanashindwa hata kutoa ushauri
Nenda wanapouza maua nunua ile miti mikubwa kama vile royal palm, golden palm na ya aina hiyo, pande uelekeo wa kutokea na kuzama jua, itasaidia kuweka kivuli na kupunguza makali ya jua kwenye ukuta wako
 
Mchwa dawa yake ni kumuondoa malkia lakini hayo mambo ya madawa ni kudanganyana kuna watu wenye utaalam wa kuwaondosha mchwa.
Yule malkia sehemu anapoishi pamejengwa na kuimarishwa kiasi kwamba vitu kama moto au kemikali haviwezi kumdhuru. Na kama kwenye kichuguu hujamuondosha malkia basi hujafanya kitu
 
Kuiga majirani zangu kupiga bati za bei mbaya na pesa kuishia hapo hapo
IMG_9572.jpg
 
Back
Top Bottom