Ni kosa kubwa mwanamke kumtawala mwanaume na Mungu amekataa hili

Ni kosa kubwa mwanamke kumtawala mwanaume na Mungu amekataa hili

Kollebundle

Senior Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
176
Reaction score
109
Nikosa kubwa mwanamke kumtawala mwanaume na Mungu amekataa hili, soma 1timotheo2:12 (Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha Wala kumtawala mwanaume). Je, waislamu maandiko yenu yanasemaje kuhusu hili?

Wanawake wa sasa hawalitii hili agizo la Mungu wanalazimisha wawe sawa na wanaume na ni kitu ambacho hakitawezekana kamwe kuwa na mafahali wãwili katika zizi moja.

Kuendelea kulazimisha hili ndio inapelekea wanawake wengi siku hizi wana uawa kila kukicha Lakini bado hawakomi kutaka kuwa Sawa na wanaume.

Je, hili lina ukweli? tujadili kwa pamoja waislamu na wakristo ruksa pia kuilinda hoja kwa kutumia maandiko ya biblia na Quran, karibuni wadau!
 
Sawa! Lakini Mwanamme asitumie mwanya huu kumnyanyasa Mwanamke.
 
Tatizo huwa mnawapigia magoti kuomba ndoa.

Magoti yanapigwa Kwa Muumba tu. Mkuu wa Falme zote.

Sasa unampigia mwanamke magoti halafu unashangaa yeye kukupanda kichwani!?
 
Aliyepewa nguvu ndio kaiachia kwa mpinzani. Kwakweli kwa aina ya vijana naowaona sasahivi acha tu wananawake wawe kichwa cha familia. Ngoja niwashauri vijana hakuna kosa kubwa mnalodanganyana na vijana wenzetu kuwa Kuna mtoto wa geti Kali sijui kakuzimia na unajiona kidume kweli, Sasa muoe kama huna akili timamu ndio tutajua kidume ni wewe au huyo mtoto wa geti Kali. Kamwe na narudia tena kamwe huwezi kuwa juu ya mwanamke kama huna kipato lamda uwe na akili nyingi sana ya kiuanaume ndio utaweza kumcontroll
 
Wapo watawala wanawake hata enzi hizo za Pontio Pilato huna hoja wewe.

Waamuzi 4:5
 
Nikosa kubwa mwanamke kumtawala mwanaume na Mungu amekataa hili, soma 1timotheo2:12 (Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha Wala kumtawala mwanaume). Je, waislamu maandiko yenu yanasemaje kuhusu hili?

Wanawake wa sasa hawalitii hili agizo la Mungu wanalazimisha wawe sawa na wanaume na ni kitu ambacho hakitawezekana kamwe kuwa na mafahali wãwili katika zizi moja.

Kuendelea kulazimisha hili ndio inapelekea wanawake wengi siku hizi wana uawa kila kukicha Lakini bado hawakomi kutaka kuwa Sawa na wanaume.

Je, hili lina ukweli? tujadili kwa pamoja waislamu na wakristo ruksa pia kuilinda hoja kwa kutumia maandiko ya biblia na Quran, karibuni wadau!
Ni makosa kwa binadamu kumtawala mwenzake bila kujali ni mwanamke au mwanaume. Ndiyo maana tulipigania uhuru ili kujitawala na si kutawaliwa.
 
Back
Top Bottom