Ni kosa kubwa sana la kiufundi kumteua Paul Makonda kuwa Mwenezi wa CCM Taifa

Nyumba haina mlango na imeshajiweka nyufa
Badala ya kuziba nyufa wanapuuzia as if hawaoni
Badala ya kuweka mlango wameweka pazia ambalo kimsingi nalo halitoshi
masoudkipanya-20231027-0001.jpg
 
Huenda ni kwa kutotathmini au kushauriwa vibaya kwa CCM kumpendekeza Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, hili litakigharimu kwa kiasi kikubwa sana.

Hii ni nafasi ya kukisemea chama kwa wananchi na siyo kwenda kulazimisha baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali kufanya kazi kulazimishwa kibabe na kusutwa ama kutukanwa. Siyo nafasi ya kwenda kulazimisha viongozi kufanya kazi nje ya utaratibu

Tatizo la Makonda ni hili hapa;
Makonda ni aina ya kiongozi anayefanya kazi nje ya tararibu kwa kulazimisha, matumizi ya nguvu na dharau kwa walio chini yake. Ikumbukwe wakati wa Magufuli ilifika mahali akiwa RC tu wa Dar es Salaam alikuwa haambiliki na kiongozi wa aina yeyote, si Waziri mkuu, si mawaziri wala kiongizi yeyote wa chama na wala hakuna aliyemkemea zaid ya Rais wa Magufuli pekee. Ilifika hatua mpaka Magufuli anamsuta hadharani Makonda kwa kufanya baadhi ya mambo nje ya utaratibu.

Kwa aina ya uongozi wa Rais Samia na falsafa yake, aina ya viongozi na watendaji walio chini yake, naona kabisa hawataweza kufanya kazi na Makonda.

Ujue mpaka sasa Makonda anaamini anaweza kuongea na Rais pekee na siyo Katibu Mkuu wa Chama wala Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Tatizo la Makonda hana uwezo wa kujuia mipaka ya majukumu yake, anachofahamu yeye ni kutumia ubabe mambo yaende, kwa akili yake kila aliye chini yake akienda kinyume na yeye basi ni mkwamishaji.

Mtifuano ndani ya chama
Kitakachofuata ndani ya CCM ni mtifuano na kuanza kutengeneza makundi ndani ya chama. Hali hii inaweza kuwatimua baadhi ya watu ndani ya chama, wataanza kukata tamaa na chama maana wataanza kudharauliwa, na kufanya kazi kwa mashinikizo.

Mimi ukiniambia watu kama Makamba Jr, Nape, Kinana, Bashe, Kikwete Jr, Katibu Mkuu wa Chama, nk, wanaweza kufanya kazi na Makonda wakiwa na amani itakuwa ni kujidanganya. Mfumo mzima wa sasa wa CCM unalalia kwenye hii safu lakini Makonda hafiti hapa.

Kufitinisha Viongozi wa Serikali na Wananchi
Kama nilivyosema, Makonda akipata nafasi yeyote ile huamini ya kwamba walio chini yake wanamhujumu kila wakati, anapenda yeye atoe maagizo na asikilizwe haijalishi ni sahihi au yana makosa!

Tutegemee sasa neno "Maagizo kutoka juu" likitamalaki, viongozi watalazimika kufanya kazi kwa maagizo ya mwenezi wa CCM. Sitashangaa kwa baadhi ya Mawaziri wakitofautiana kwa kiasi kikubwa na Makonda, au baadhi ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakipishana kwa kiasi kikubwa na Makonda.

Hii inaweza kuwapunguzia ari ya kufanya kazi kwa bidii na misingi ya kisheria ama taratibu, watanaki watu wa kusononeka.

Kiama kwa Vyombo vya Habari
Naona vyombo vya habari vikielekea kuripoti habari kwa maelekezo kutoka CCM, hakuna chombo kitakachokuwa huru kuripoti taarifa kwa balance.

Kila chombo kitaripoti siyo tu ni serikali inataka bali ni nini Chama au Makonda anataka. Kuhusu hili la vyombo vya habari kila mtu ni shahidi alivyokuwa tatizo wakati akiwa RC wa Mkoa tu, sasa akiwa Mwenezi itakuwaje?

CCM ya Samia wanayo nafasi ya kusahihisha uteuzi huu
Kwa ushauri wangu ambao unaweza usiwe na mbolea sana kwa Pro-Makonda kama kina Bananga na wanufaika wake wengine, ila kwa haki ya Mungu kabisa na ustawi wa taifa hili na Chama, katika kukiunganisha chama, CC ya CCM pamoja na kwamba maamini inampa muda kumpima lakini wana nafadi ya kusahihisha utauzi huu.

Wapo Wanaccm wazuri wanaoweza kukisemea Chama bila kuhitalifiana na yeyote, Heri James, Jery Muro na makada wa CCM wengine chungu mzima wenye uwezo wa kuifanya kazi hii kwa utaratibu na kuheshimu misingi ya kazi.

Makonda mpaka sasa ana zuio la kusafiri kwenda US kwa sababu ya matendo yake, huku siyo kurudi kuifunga nchi badala ya kuifungulia kama alivyo sema Mama?

Nawatakieni weekend njema.
Bora Makonda kuliko Heri James na Jery MURO.
 
Hicho ni cheo Cha kisiasa na siku zote siasa ni uongo uongo na ujanja ujanja tu na hizo ndio sifa za Makonda hivyo hicho cheo kinamfaa

Pia nahisi mama alikuwa hana rafiki ndani ya Chama ndio maana amemuweka Makonda hapo awe rafiki yake na chawa wake

Acha wivu wa kijinga
 
Makonda ni zero brain kweli kweli
Hii Nchi yetu ya ajabu sana, kuna watu millioni 60. Kwanza sofa zake tu ni mbaya. Aligushi vyeti yaani huyu ni open fraud, halafu alimtandika kofi Warioba, na JK akampa cheo. Wakati fulani unajuta kwa nini uko nchi hii. Lakini ndiyo ancestral home. Yaani tupo hostages kwenye nchi yetu wenyewe.
 
Jamaa ni mshirikina balaa, pia anajua kucheza na akili za watawala
 
Sasa wewe kama siyo mwana CCM, uongozi wao unakuhusu nini, nyie ndiyo mnawalalamikia chadema kutobadilisha mwenyekiti, wakati Uongozi wao wenyewe wamemekubaliana kuwa nae.
 
Jamaa ni mshirikina balaa, pia anajua kucheza na akili za watawala
Mara nyingi mtu, ambae haamini mafanikio katika njia ya kawaida ni hatari sana.
Ni kwa sababu tu una amini sana ushirikina, umeamua kumvisha jamaa, koti la ushirikina huna ushahidi nae, wala haupo karibu nae.

Na kama kweli ushirikina una uwezo wa kukufanya ufanikiwe katika maisha, mimi nauhitaji hata sasa hivi.
 
Tutegemee sasa neno "Maagizo kutoka juu" likitamalaki, viongozi watalazimika kufanya kazi kwa maagizo ya mwenezi wa CCM. Sitashangaa kwa baadhi ya Mawaziri wakitofautiana kwa kiasi kikubwa na Makonda, au baadhi ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakipishana kwa kiasi kikubwa na Makonda.
Wakibishana na Makonda nafasi za Teuzi watazisikia kwenye redio
 
Kila chombo kitaripoti siyo tu ni serikali inataka bali ni nini Chama au Makonda anataka. Kuhusu hili la vyombo vya habari kila mtu ni shahidi alivyokuwa tatizo wakati akiwa RC wa Mkoa tu, sasa akiwa Mwenezi itakuwaje?

CCM ya Samia wanayo nafasi ya kusahihisha uteuzi huu
Kwa ushauri wangu ambao unaweza usiwe na mbolea sana kwa Pro-Makonda kama kina Bananga na wanufaika wake wengine, ila kwa haki ya Mungu kabisa na ustawi wa taifa hili na Chama, katika kukiunganisha chama, CC ya CCM pamoja na kwamba maamini inampa muda kumpima lakini wana nafadi ya kusahihisha utauzi huu.
Kwenye swala la habari Makonda yuko saw ana Magufuli hawataki watu wengine wasikike.

Walivamia Clouds kwa sababu tu wamegoma kutoa habari za uzushi kumfurahisha yeye na bosi wake.
 
Huenda ni kwa kutotathmini au kushauriwa vibaya kwa CCM kumpendekeza Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, hili litakigharimu kwa kiasi kikubwa sana.

Hii ni nafasi ya kukisemea chama kwa wananchi na siyo kwenda kulazimisha baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali kufanya kazi kulazimishwa kibabe na kusutwa ama kutukanwa. Siyo nafasi ya kwenda kulazimisha viongozi kufanya kazi nje ya utaratibu

Tatizo la Makonda ni hili hapa;
Makonda ni aina ya kiongozi anayefanya kazi nje ya tararibu kwa kulazimisha, matumizi ya nguvu na dharau kwa walio chini yake. Ikumbukwe wakati wa Magufuli ilifika mahali akiwa RC tu wa Dar es Salaam alikuwa haambiliki na kiongozi wa aina yeyote, si Waziri mkuu, si mawaziri wala kiongizi yeyote wa chama na wala hakuna aliyemkemea zaid ya Rais wa Magufuli pekee. Ilifika hatua mpaka Magufuli anamsuta hadharani Makonda kwa kufanya baadhi ya mambo nje ya utaratibu.

Kwa aina ya uongozi wa Rais Samia na falsafa yake, aina ya viongozi na watendaji walio chini yake, naona kabisa hawataweza kufanya kazi na Makonda.

Ujue mpaka sasa Makonda anaamini anaweza kuongea na Rais pekee na siyo Katibu Mkuu wa Chama wala Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Tatizo la Makonda hana uwezo wa kujuia mipaka ya majukumu yake, anachofahamu yeye ni kutumia ubabe mambo yaende, kwa akili yake kila aliye chini yake akienda kinyume na yeye basi ni mkwamishaji.

Mtifuano ndani ya chama
Kitakachofuata ndani ya CCM ni mtifuano na kuanza kutengeneza makundi ndani ya chama. Hali hii inaweza kuwatimua baadhi ya watu ndani ya chama, wataanza kukata tamaa na chama maana wataanza kudharauliwa, na kufanya kazi kwa mashinikizo.

Mimi ukiniambia watu kama Makamba Jr, Nape, Kinana, Bashe, Kikwete Jr, Katibu Mkuu wa Chama, nk, wanaweza kufanya kazi na Makonda wakiwa na amani itakuwa ni kujidanganya. Mfumo mzima wa sasa wa CCM unalalia kwenye hii safu lakini Makonda hafiti hapa.

Kufitinisha Viongozi wa Serikali na Wananchi
Kama nilivyosema, Makonda akipata nafasi yeyote ile huamini ya kwamba walio chini yake wanamhujumu kila wakati, anapenda yeye atoe maagizo na asikilizwe haijalishi ni sahihi au yana makosa!

Tutegemee sasa neno "Maagizo kutoka juu" likitamalaki, viongozi watalazimika kufanya kazi kwa maagizo ya mwenezi wa CCM. Sitashangaa kwa baadhi ya Mawaziri wakitofautiana kwa kiasi kikubwa na Makonda, au baadhi ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakipishana kwa kiasi kikubwa na Makonda.

Hii inaweza kuwapunguzia ari ya kufanya kazi kwa bidii na misingi ya kisheria ama taratibu, watanaki watu wa kusononeka.

Kiama kwa Vyombo vya Habari
Naona vyombo vya habari vikielekea kuripoti habari kwa maelekezo kutoka CCM, hakuna chombo kitakachokuwa huru kuripoti taarifa kwa balance.

Kila chombo kitaripoti siyo tu ni serikali inataka bali ni nini Chama au Makonda anataka. Kuhusu hili la vyombo vya habari kila mtu ni shahidi alivyokuwa tatizo wakati akiwa RC wa Mkoa tu, sasa akiwa Mwenezi itakuwaje?

CCM ya Samia wanayo nafasi ya kusahihisha uteuzi huu
Kwa ushauri wangu ambao unaweza usiwe na mbolea sana kwa Pro-Makonda kama kina Bananga na wanufaika wake wengine, ila kwa haki ya Mungu kabisa na ustawi wa taifa hili na Chama, katika kukiunganisha chama, CC ya CCM pamoja na kwamba maamini inampa muda kumpima lakini wana nafadi ya kusahihisha utauzi huu.

Wapo Wanaccm wazuri wanaoweza kukisemea Chama bila kuhitalifiana na yeyote, Heri James, Jery Muro na makada wa CCM wengine chungu mzima wenye uwezo wa kuifanya kazi hii kwa utaratibu na kuheshimu misingi ya kazi.

Makonda mpaka sasa ana zuio la kusafiri kwenda US kwa sababu ya matendo yake, huku siyo kurudi kuifunga nchi badala ya kuifungulia kama alivyo sema Mama?

Nawatakieni weekend njema.
Angekuwepo le mutuzi sasa.. ndio angekua reporter wa habari zake.

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Huenda ni kwa kutotathmini au kushauriwa vibaya kwa CCM kumpendekeza Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, hili litakigharimu kwa kiasi kikubwa sana.
Kosa au kuchanganyikiwa ilikuwa ni kumteua diaspora tundu kuwa makamu mwenyekiti wa chama cha kutoa taarifa.
 
Mara nyingi mtu, ambae haamini mafanikio katika njia ya kawaida ni hatari sana.
Ni kwa sababu tu una amini sana ushirikina, umeamua kumvisha jamaa, koti la ushirikina huna ushahidi nae, wala haupo karibu nae.

Na kama kweli ushirikina una uwezo wa kukufanya ufanikiwe katika maisha, mimi nauhitaji hata sasa hivi.
Unajifanya huamini ushirikina ni upumbavu tupu, wazungu, wachina, wahindi wamejaa hirizi tupu sembuse wewe uliyezaliwa Ikungi Singida! Misikiti na Makanisa vililetwa na wakoloni, uchawi hata kwenye bible umetajwa.
 
Acha maneno mengi wewe sema kuchaguliwa Makonda kuwa Mwenyezi, itawafelisha chadema Kwa ajili hiyo ndo Kali yenu
 
Wahenga wanasema hivi;

"Kuvuja kwa pakacha, ni heri ya mchukuzi.."

Acha kuwashitua, acha pakacha livuje ili mchukuzi (washindani wao kisiasa) washinde kirahisi.!
 
Back
Top Bottom