Ni kwanini bado Waarabu wanatubagua, hata Mwafrika anapokuwa Muislam wanamkatalia kumuoa binti yao?

Ni kwanini bado Waarabu wanatubagua, hata Mwafrika anapokuwa Muislam wanamkatalia kumuoa binti yao?

Umenikumbusha story moja ya zanzibar! Nadhani huko uarabuni ni mbali sana! Ubaguzi unaanzia hapa hapa kwetu Tanzania, kipindi nipo Zanzibar, kuna nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye tulisoma nae kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari Ordinary level pamoja na shule moja! Tulikuja kuachana Advance level (five &six).

Kisha yeye akaenda kusomea uhasibu pale TIA, Mimi nikaingia kwenye kada nyingine! Wanasema milima haikutani Bali wanadamu hukutana, Sasa kwenye harakati za maisha baada ya kutengana kwa muda mrefu, tukaja kukutana Zanzibar!

Yeye akiwa mwanajeshi (jwtz), Mimi nikiwa kwenye kada nyingine (jina kapuni).Tulifurahi sana na kuongea mambo mengi ikiwa pamoja na kukumbushana mambo yaliyopita! Sasa to cut the story, jamaa alikuwa amempenda binti mmoja wa kipemba mwenye asili ya kiarabu yaani wale halfcast, alikuwa mpemba, akaniambia ana Mpango wa kumuoa lakini tatizo kwao binti hawataki mtu wa bara! Wanataka aolewe na mpemba mwenzake!

Sasa baada ya kupambana sana jamaa akaona isiwe tatizo , akakodisha (aliwaomba) watu wazima fulani yaani wazee akawapanga wawe kama wazazi wake, waseme wao ni wazazi wake na wanaasili ya zanzibar (pemba). Baada ya kuwalipa vizuri kweli walikwenda nao ukweni pemba na jamaa akakubaliwa kuoa huyo binti wao chotara!

Sasa Mambo yalitibuka siku ya harusi (ndoa) siku ya kwenda kumchukua mke kwao, sijui wakina nani waliwatonya wazee wa binti kwamba jamaa (mume) ni mtu wa bara Wala sio mzanzibar mpemba kama alivyowaambia, jamaa alikuwa mtu wa bara , Mnyamwezi wa Tabora! Mweusi tii kuliko hata Mimi! (Usicheke). Japo jamaa alikuwa muislam kamili tangu wazazi na mababu, na mtanzania halisi, lakini wazazi wale wa binti walivunja shughuli yote na kumtimua jamaa! Hivyo alikosa mke na maji ya moto! Sherehe yote ikawa Imeishia hapo licha ya gharama zote za harusi aliyoingia. Tatizo tu hakuwa mpemba Wala mzanzibar Bali alikuwa Mnyamwezi wa Tabora!

Nikaamini kweli racism never end!
 
Shida inakuja kwa kina waarabu, yani hata uwe muislam uliekariri aya nyingi za korani na sauti nzuri ya kuzinukuu
kwahiyo ukaenda madrasa , ukajifunza, ukanukuu kwa mwembwe kumbe kisa umvue mwarabu gaguro?
 
Kwa wazungu ndoa za waafrika na wazungu zipo nyingi tu, ni kawaida.

Shida inakuja kwa kina waarabu, yani hata uwe muislam uliekariri aya nyingi za korani na sauti nzuri ya kuzinukuu hawawezi kukupa binti yao labda kama utaweza kutumika kimaslaho aidha uwe na cheo kikubwa ama uwe na pesa nyingi sana.

Na hapa navomaanisha waafrika ni hadi wazanzibari ambao hufanana na wasomali, hali ni hivyo hivyo tu, japo wao hupenda kujiweka kundi moja na waarabu ila waarabu huwatolea nje.
Wewe unaweza kuoa/kuolewa kwenye nyumba ya Waziri wako ama Rais wako wa Nchi bila kua na Money na Power? Basi ujue ubaguzi huanzia ndani kwako,

Kumbe mnawanyima kuwekeza bandari yenu kisa wanawanyima Ndoa [emoji15]
 
Serikali zenu Waafrika zisingekua katili hao wadada wasingekua huko Arabuni wanafanyiwa ukatili,
Akili yako fupi sana kubaini ubaguzi na ukatili unaanzia nyumbani kwako halafu unataka kwenda kupendwa nchi za wenzako!
Mbona waarab wapo huku Africa hawafanyiwi ukatili? Akili yako fupi sana, mtu sio mlima akae sehemu moja.
 
Ila ubaguzi wa Wa-Italy, Warusi, Germany na Waarabu ni next level.
Hao waarabu unaowaita wabaguzi ndio pekee Dunia nzima ambao wame wa Asimilate watu weusi kama one of their own.

Nchi zote za kiarabu zina watu weusi, raia, wana nyadhifa kubwa na wanapata benefit zote wanazopata raia wengine.

Saudi pekee asilimia 10 ni Afro Arabs ambao wengi wametoka kabila la Hausa Nigeria Kule Saudi wanaitwa Hawsawi, Fulani kule wanaitwa Falaata na kunari wanaitwa Barnawi.

Wakati Taifa la Saudia linaundwa Hawsawi walikua ndio wa kwanza kuukubali utawala wa House of Al saud na wapo kwenye Cabinet, kama Elites wa Nchi, google Hawsawi Saudi Arabia utawaona kibao.

Pia angalia Oman, Kuwait kote wamewahi kuwa na Viongozi weusi

Nioneshe Tu Hapa Tanzania Viongozi waarabu, Salum Ahmed Salum Aliekewa figisu mpaka kazeeka.
 
Mbona waarab wapo huku Africa hawafanyiwi ukatili? Akili yako fupi sana, mtu sio mlima akae sehemu moja.
Hawafanyiwi ukatili sababu nyie Waafrika mnajibagua wenyewe kwa wenyewe,
Akili yako fupi kuweza kubaini kua ngozi nyeusi ndio yaongoza kwa ubaguzi wa wenyewe kwa wenyewe na kuwakumbatia wasiokua na nasaba nao,

Utaona muafrika wa kiislam anakataa kata kata kuozesha kwa muafrika wa kiikristo na vice versa, na bado wengine wanaitana majina mabaya kwa tofauti ya dini zao badala ya kuungana kwa nasaba zao.
 
Kwamba kwenye comment yangu haujaona Germany, Russia na Italy ila umeona waarabu tu, si ndio?

Punguzeni mihemuko ya kidini wanapotajwa wavaa kanzu wenzenu.
 
Sipo kuichafua Dini yangu ila hawa Jamaa ni next level.... niliingiaga Msikiti wao kwa kweli nilipata tabu sana... kukaa Mstari mmoja na Mtu mweusi kwao hawataki na ukikaa nao utaona wanavyosegea na kuacha nafasi kubwa kati yao na wewe.... wakiingia Msikitini wote wewe ukija wakikuona kufunga Mlango si jambo la kushangaa
Huo msikiti wa waarabu upo sehemu gani? Just curious!
 
Mbona waarab wapo huku Africa hawafanyiwi ukatili? Akili yako fupi sana, mtu sio mlima akae sehemu moja.
Unakumbuka Richa Adhia alivyokuwa Miss Tanzania alivyokua anabaguliwa waziwazi? Watu kibao walikua wanambagua Nchi ya weusi hatuwezi wakilishwa na mweupe. Ubaguzi upo wa kutosha Hapa kwetu, sababu wewe sio Mwarabu huwezi jua,

Mimi wakati mdogo naenda shule kawaida sana kukuta watu Mtaani wanakuimbia huu wimbo "mwarabu koko sukuma gari twende"
 
Hawafanyiwi ukatili sababu nyie Waafrika mnajibagua wenyewe kwa wenyewe,
Akili yako fupi kuweza kubaini kua ngozi nyeusi ndio yaongoza kwa ubaguzi wa wenyewe kwa wenyewe na kuwakumbatia wasiokua na nasaba nao,

Utaona muafrika wa kiislam anakataa kata kata kuozesha kwa muafrika wa kiikristo na vice versa, na bado wengine wanaitana majina mabaya kwa tofauti ya dini zao badala ya kuungana kwa nasaba zao.
Ubaguzi upo kwenye jamii zote, kabla ya dini ulikuwepo ukabila kwa babu zetu, hata wahindi weusi na weupe wanabaguana hata wazungu, issue arabs ni jamii kielimu ipo nyuma hata wa wabantu wapo mbele, utajiri wa mafuta usikutishe, hamna kitu mule.
 
Unakumbuka Richa Adhia alivyokuwa Miss Tanzania alivyokua anabaguliwa waziwazi? Watu kibao walikua wanambagua Nchi ya weusi hatuwezi wakilishwa na mweupe. Ubaguzi upo wa kutosha Hapa kwetu, sababu wewe sio Mwarabu huwezi jua,

Mimi wakati mdogo naenda shule kawaida sana kukuta watu Mtaani wanakuimbia huu wimbo "mwarabu koko sukuma gari twende"
Arabs hayo ni matokeo ya kubagua weusi.
 
Unakumbuka Richa Adhia alivyokuwa Miss Tanzania alivyokua anabaguliwa waziwazi? Watu kibao walikua wanambagua Nchi ya weusi hatuwezi wakilishwa na mweupe. Ubaguzi upo wa kutosha Hapa kwetu, sababu wewe sio Mwarabu huwezi jua,

Mimi wakati mdogo naenda shule kawaida sana kukuta watu Mtaani wanakuimbia huu wimbo "mwarabu koko sukuma gari twende"
Leo hii nchi ya arabs anaweza tokea mtu mweusi kuwa miss, Morocco tu hio walikuwa wanaongea ubaguzi tu kombe la dunia, akili hamna ndio maana mzungu anawabonda huko middle East.
 
Huyo alpha blond unamlinganisha na nan? Jamaa ana pesa pia ni maarufu kama huna pesa ya kutosha huwezi kuwapata huwa wanataka wakutumie na kamwe hawezi kuzaa na mtu mweusi wabaguzi mno hao.
Kama Wenye pesa weusi wanaoa waarabu na masikini hawaoi waarabu huo unakua sio ubaguzi wa rangi, unaitwa ubaguzi wa pesa,

Viongozi wengi Nchi hii kuanzia kina Karume (Kabla ya Mapinduzi), Mwinyi, wabunge wa kutosha wana wake waarabu, sehemu Zote zenye waarabu wengi Nchi hii Tanga, Tabora kuna Intermarriage za Kutosha tu. Kila siku humu Jukwaani Nyuzi kama hizi zikija Watu wa Tanga na Tabora wakiwaambia mnabisha, na nyie mnaobisha hamna Experience yoyote ya kuishi na waarabu mnabisha for the sake of Kubisha.
 
Ubaguzi upo kwenye jamii zote, kabla ya dini ulikuwepo ukabila kwa babu zetu, hata wahindi weusi na weupe wanabaguana hata wazungu, issue arabs ni jamii kielimu ipo nyuma hata wa wabantu wapo mbele, utajiri wa mafuta usikutishe, hamna kitu mule.
Una chuki nao kisa hawana elimu lakini wamekupita maendeleo!! Hao wasiokua na elimu si ndio dada zako wamejazana huko kufanya kazi za ndani? Wasiokua na elimu ndio wanakuja kuwekeza kwenye bandari yenu,

Je na sisi tupo kundi gani???
 
Back
Top Bottom