Umenikumbusha story moja ya zanzibar! Nadhani huko uarabuni ni mbali sana! Ubaguzi unaanzia hapa hapa kwetu Tanzania, kipindi nipo Zanzibar, kuna nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye tulisoma nae kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari Ordinary level pamoja na shule moja! Tulikuja kuachana Advance level (five &six).
Kisha yeye akaenda kusomea uhasibu pale TIA, Mimi nikaingia kwenye kada nyingine! Wanasema milima haikutani Bali wanadamu hukutana, Sasa kwenye harakati za maisha baada ya kutengana kwa muda mrefu, tukaja kukutana Zanzibar!
Yeye akiwa mwanajeshi (jwtz), Mimi nikiwa kwenye kada nyingine (jina kapuni).Tulifurahi sana na kuongea mambo mengi ikiwa pamoja na kukumbushana mambo yaliyopita! Sasa to cut the story, jamaa alikuwa amempenda binti mmoja wa kipemba mwenye asili ya kiarabu yaani wale halfcast, alikuwa mpemba, akaniambia ana Mpango wa kumuoa lakini tatizo kwao binti hawataki mtu wa bara! Wanataka aolewe na mpemba mwenzake!
Sasa baada ya kupambana sana jamaa akaona isiwe tatizo , akakodisha (aliwaomba) watu wazima fulani yaani wazee akawapanga wawe kama wazazi wake, waseme wao ni wazazi wake na wanaasili ya zanzibar (pemba). Baada ya kuwalipa vizuri kweli walikwenda nao ukweni pemba na jamaa akakubaliwa kuoa huyo binti wao chotara!
Sasa Mambo yalitibuka siku ya harusi (ndoa) siku ya kwenda kumchukua mke kwao, sijui wakina nani waliwatonya wazee wa binti kwamba jamaa (mume) ni mtu wa bara Wala sio mzanzibar mpemba kama alivyowaambia, jamaa alikuwa mtu wa bara , Mnyamwezi wa Tabora! Mweusi tii kuliko hata Mimi! (Usicheke). Japo jamaa alikuwa muislam kamili tangu wazazi na mababu, na mtanzania halisi, lakini wazazi wale wa binti walivunja shughuli yote na kumtimua jamaa! Hivyo alikosa mke na maji ya moto! Sherehe yote ikawa Imeishia hapo licha ya gharama zote za harusi aliyoingia. Tatizo tu hakuwa mpemba Wala mzanzibar Bali alikuwa Mnyamwezi wa Tabora!
Nikaamini kweli racism never end!