Kwa maoni yangu ukikuta Traffic Police yuko katika makutano ya barabara akiongoza magari kwa muda mrefu katika siku, basi ujue sehemu hiyo inahitaji mataa ili kuwa mbadala kwa kuwepo kwa Traffic. Lakini kama kuna eneo linahitajika mataa basi ni vizuri hiyo hoja ikapenyezwa kwa madiwani, nina imani mapato ya mji wa Moshi yanaweza kutenga sehemuya fedha na kununua hayo mataa kwa kushirikiana na TARURA. Arusha walianza kwa kupata ufadhili, hata Moshi inwezekana.