Ni kwanini mji wa Moshi hauna taa za barabarani za kuongoza Magari?

Ni kwanini mji wa Moshi hauna taa za barabarani za kuongoza Magari?

Kwa kuwa watu wengine kule wanajitambua wanajingoza wenyewe siyo kama hawa nyumbu wengine wamejua chuma juzi
Wakuu imebidi niuize ili nijue.

Ni kwanini mji wa Moshi ambao ndio makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro hauna taa za kuongozea magari, ili hali miji midogo kama Singida, Shinyanga na Babati naona wameweka taa za kuongoza magari.

Ifahamike kuwa mpaka sasa Manispaa ya Moshi ndio manispaa inayoongoza kwa kuwa na mtandao mpana wa barabara ukiondoa majiji machache yalioyopo Tanzania, hii ni kwa mujibu wa TARURA. www.tarura.go.tz

Nini kinashindikana kuziweka hizi taa?
 
Ni kweli mji wa Moshi hauna taa za barabarani licha ya kuwa mji muhimu unaoiunganisha kanda ya Kaskazini.
Mji huu hauna taa za barabarani kwa sababu zifuatazo:
1. Mpangilio mzuri wa mji. Wengi mtakubaliana na mimi kuwa Moshi ndio mji pekee uliopangiliwa vizuri zaidi..... Njia zote ndani ya mji zinaungana.
2. Mji wa Moshi una mizunguko kwenye maeneo muhimu ya makutano. Mzunguko wa mnara wa mwenge ukitokea au kwenda Arusha, mzunguko wa YMCA unaunganisha njia ya DSM, KCMC, Arusha na kuingia Moshi mjini. Mzunguko wa Clock tower, mzunguko wa Stand ya mboya, mzunguko wa police line.
3. Kuwepo kwa barabara ya njia nne (double roads) katikati ya mji. Magari yanapita mengi kwa wakati mmoja na pia ni rahisi kukatiza kwenye makutano.
4. Mtandao mpana wa barabara. Barabara za Moshi zote zina njia mbadala ikiwa moja itakuwa na foleni na zote zinawezesha kutoka au kuingia mjini.
5. Uelewa mkubwa wa matumizi ya barabara. Wakazi wengi wa Moshi wana uzoefu mkubwa wa kutumia barabara na ni nadra sana kuona "road rage" Moshi. Hata kipindi cha mwezi wa 12 wageni wanapokuwa wengi haijawahi kuwa changamoto.
6. Matumizi ya public transport. Wakazi wengi wa Moshi hutumia zaidi usafiri wa umma (vibasi) kuliko usafiri binafsi. Sio ajabu kukuta tajiri wa moshi akiwa kwenye bajaji akienda ofisini. Hii ni kwa sababu za kiuchumi zaidi [emoji23]
7. Uwepo wa huduma muhimu nje ya mji. Mji wa Moshi sio kila huduma imerundikwa mjini. Huduma nyingi kama mahoteli, hospitali na masoko yako pembeni au nje ya mji.
Naam mahotel ,ma supermarket yamejaa huko vijin. Kama marangu,himo ROMBO nk kwahyo mji hauna pilika nyingi
 
Ni mji wa kishamba sana wakazi wake ni wezi sana
Washamba wapo kwenu chato
Mji wa moshi hauna haja ya taa kwakuwa una barabara nyingi za mzunguko(round abouts) za kuingia na kutoka mjini
Pia ni mji unaoongoza Kitaifa kwa mtandao mpana wa barabara kwa mujibu wa tarura umeelewa ewe mchunga mbuzi?
 
Moshi ni manispaa iliyojaa wezi wa mali za uma ndiyo maana haiendelei hadi leo ni manispaa tu.
 
Moshi ni manispaa iliyojaa wezi wa mali za uma ndiyo maana haiendelei hadi leo ni manispaa tu.
Hahaaahahaaaaaa...... Wezi wa mali ya uma ni viongozi wanaoletwa na serikali.
Halafu kuna wakati bora ukae kimya ufiche upumbavu wako. Unasema Moshi haiendelei.... Hebu tuambie tafsiri ya maendeleo kwa kikwenu? Au taa za barabarani ndio maendeleo?
Na kwa taarifa yako Moshi ilishapata sofa za kuwa jiji zamani kabla ya Tanga, Mbeya. Kikwazo kikuu ni ukubwa wa eneo tu. Manispaa ya Moshi ina eneo dogo sana la ukubwa. Mazungumzo yanaendelea na Halimashauri ya Moshi (Moshi DC) ili kumega eneo la Moshi DC kwenda Moshi MC (Manispaa) ili kuwa na Jiji la Moshi......... COMING SOON...
 
tulikuwa tunajenga kwanza chato.
Na mnakumbuka alisema 'mikoa ya kaskazini mtasubiri kwanza tujenge kwingine'
Da! nachelea kusema kitu!
 
Washamba wapo kwenu chato
Mji wa moshi hauna haja ya taa kwakuwa una barabara nyingi za mzunguko(round abouts) za kuingia na kutoka mjini
Pia ni mji unaoongoza Kitaifa kwa mtandao mpana wa barabara kwa mujibu wa tarura umeelewa ewe mchunga mbuzi?
Kwann utaje chato, una uhakika uyo mtu ni wa chato, ndio mnasababisha watu wahisi nyinyi ndio mnaleta ukabila dhidi ya Kanda ya ziwa, me mchaga mkazi wa moshi, ila hukuwa na haja ya kuhusisha chato, grow up
 
Taa za barabarani hufanyakazi kuingiza magari pale msongamano wa magari barabarani unapokuwa mkubwa. Kama diversion za barabara ni nyingi hupelekea msongamano kwenye barabara husika kupungua na hivyo kutokuhitajika taa. Mfano, Mji wa Kigoma-Ujiji hutumia barabara moja ya Lumumba hivyo kuwa na msongamano na ajali kwa watembea kw miguu. Hapo wameweka taa barabara hiyo ilikupunguza ajali. Taa za barabarani sio mapambo mheshimiwa eti ziwekwe hata pale pasipokuwa na maana. Umesema Moshi Kuna barabara nyingi, na hivyo hupunguza msongamano wa magari.
 
Yanaongozwa kwenda wapi?
Wakati mwingine tumia akili kidogo
 
Ni kweli mji wa Moshi hauna taa za barabarani licha ya kuwa mji muhimu unaoiunganisha kanda ya Kaskazini.
Mji huu hauna taa za barabarani kwa sababu zifuatazo:
1. Mpangilio mzuri wa mji. Wengi mtakubaliana na mimi kuwa Moshi ndio mji pekee uliopangiliwa vizuri zaidi..... Njia zote ndani ya mji zinaungana.
2. Mji wa Moshi una mizunguko kwenye maeneo muhimu ya makutano. Mzunguko wa mnara wa mwenge ukitokea au kwenda Arusha, mzunguko wa YMCA unaunganisha njia ya DSM, KCMC, Arusha na kuingia Moshi mjini. Mzunguko wa Clock tower, mzunguko wa Stand ya mboya, mzunguko wa police line.
3. Kuwepo kwa barabara ya njia nne (double roads) katikati ya mji. Magari yanapita mengi kwa wakati mmoja na pia ni rahisi kukatiza kwenye makutano.
4. Mtandao mpana wa barabara. Barabara za Moshi zote zina njia mbadala ikiwa moja itakuwa na foleni na zote zinawezesha kutoka au kuingia mjini.
5. Uelewa mkubwa wa matumizi ya barabara. Wakazi wengi wa Moshi wana uzoefu mkubwa wa kutumia barabara na ni nadra sana kuona "road rage" Moshi. Hata kipindi cha mwezi wa 12 wageni wanapokuwa wengi haijawahi kuwa changamoto.
6. Matumizi ya public transport. Wakazi wengi wa Moshi hutumia zaidi usafiri wa umma (vibasi) kuliko usafiri binafsi. Sio ajabu kukuta tajiri wa moshi akiwa kwenye bajaji akienda ofisini. Hii ni kwa sababu za kiuchumi zaidi 😂
7. Uwepo wa huduma muhimu nje ya mji. Mji wa Moshi sio kila huduma imerundikwa mjini. Huduma nyingi kama mahoteli, hospitali na masoko yako pembeni au nje ya mji.
5 na 6 nimekuelewa vi z uri sana mkuu. true true
 
Sasa moshi kuna magari gani mpaka waweke taa?
Moshi hamnaga foleni! Hasa kama unakaa mjini ndio burudani! Kutoka city centre kwenda kwako huwezi maliza 20mins kwa gari iwe Soweto, Majengo au KCMC labda kama unakaa mahali interior sana
 
Back
Top Bottom