LadyRed
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 9,636
- 11,483
Ardhi milioni tano mijini???😳😳Wazungu walijenga nyumba za ghorofa kutokana na uhaba wa ardhi kwao. Nimekutana na Wafrika Magharibi pia mawazo yao ni ya kujenga ma ghorofa. Nikipowauliza sababu waliniambia kwao ardhi ni ghali sana. Kupata kiwanja cha kujenga nyumba inakulazimu uwe na kuanzia milioni 20 kwa pesa ya Tanzania. Wanasema ukijenga ghorofa hukosi mpangaji na wewe unapata na sehemu yako ya kuishi kwa amani.
Wengine wanasema wanajenga ghorofa kuyaona matunda ya mafanikio yake kwa macho. Sasa ninajiuliza sisi ardhi tunayo kubwa sana. Mpaka sasa bei ya kiwanja ni wastaniwa milioni tano mijini. Ni kwanini unawaza kujenga ghorofa kama una wazo hilo au ni kwanini ulijenga ghorofa?
viwanja vya wapi hivyo na vina ukubwa gani?.