Kwa msingi wa ghorofa unaweza kununua viwanja viwili.
Hujafanya vizuri cost analysis kati ya nyumba za kawaida na ghorofa. Naomba nikupe mwongozo kidogo tu. Kwa mfano unahitaji nyumba 2 zinazofanana. Itakuwa faida kwako ukijenga katika mfumo wa ghorofa au ujenge moja moja?
Faida za Ghorofa.
-ukijenga ghorofa ni sawa na kupata eneo jingine bure kabisa (Saving)
-Ukijenga ghorofa, ni kweli gharama ya msingi itaongezeka (Kwa 120%-150%) ukilinganisha na nyumba ya kawaida. Lakini kumbuka huo msingi unabeba nyumba 2 (hiyo ni saving)
-Kumbuka floor iliyopo ina serve kazi mbili.1 Ni paa kwenye nyumba ya chini,2 ni msingi kwenye nyumba ya juu. (2 in 1 hiyo ni saving)
-kwenye ghorofa, huhitaji kuweka ceiling kwenye nyumba ya chini (Hiyo ni serving)
Hayo ni Kwa uchache tu faida za Ghorofa. Lakini ukijenga nyumba 2 tofauti, gharama zitakuwa Mara 2 , tofauti na kwenye ghorofa hazitakuwa double kwa sababu ya baadhi ya vitu kuwa shared. Hata waswahili walisema umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu.
Pia chukulia familia mbili tofauti zenye watu watatu watatu. Zikiungana kuwa moja, gharama za matumizi zitakuwa ndogo ukilinganisha na pale Kila familia inaishi kivyakevyake.
Kwa hiyo "Sharing factor" siku zote hupunguza gharama (unit cost) kwenye mambo mengi hata kwenye ujenzi pia (ghorofa).
Nimeeleza kwa uchache ngoja niishie hapo. Lakini pia na declare interest kuwa Mimi Ni Quantity Surveyor (QS) kwa hiyo nimesomea ujenzi, na ninauzoefu wa kutosha kwenye ujenzi wa majengo na barabara kwa zaidi ya miaka 10.