Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Hujafanya vizuri cost analysis kati ya nyumba za kawaida na ghorofa. Naomba nikupe mwongozo kidogo tu. Kwa mfano unahitaji nyumba 2 zinazofanana. Itakuwa faida kwako ukijenga katika mfumo wa ghorofa au ujenge moja moja?

Faida za Ghorofa.
-ukijenga ghorofa ni sawa na kupata eneo jingine bure kabisa (Saving)
-Ukijenga ghorofa, ni kweli gharama ya msingi itaongezeka (Kwa 120%-150%) ukilinganisha na nyumba ya kawaida. Lakini kumbuka huo msingi unabeba nyumba 2 (hiyo ni saving)
-Kumbuka floor iliyopo ina serve kazi mbili.1 Ni paa kwenye nyumba ya chini,2 ni msingi kwenye nyumba ya juu. (2 in 1 hiyo ni saving)
-kwenye ghorofa, huhitaji kuweka ceiling kwenye nyumba ya chini (Hiyo ni serving)

Hayo ni Kwa uchache tu faida za Ghorofa. Lakini ukijenga nyumba 2 tofauti, gharama zitakuwa Mara 2 , tofauti na kwenye ghorofa hazitakuwa double kwa sababu ya baadhi ya vitu kuwa shared. Hata waswahili walisema umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu.

Pia chukulia familia mbili tofauti zenye watu watatu watatu. Zikiungana kuwa moja, gharama za matumizi zitakuwa ndogo ukilinganisha na pale Kila familia inaishi kivyakevyake.

Kwa hiyo "Sharing factor" siku zote hupunguza gharama (unit cost) kwenye mambo mengi hata kwenye ujenzi pia (ghorofa).

Nimeeleza kwa uchache ngoja niishie hapo. Lakini pia na declare interest kuwa Mimi Ni Quantity Surveyor (QS) kwa hiyo nimesomea ujenzi, na ninauzoefu wa kutosha kwenye ujenzi wa majengo na barabara kwa zaidi ya miaka 10.
Chief umenigusa kidogo, nina mpango wa kujenga fremu ya ghorofa lakini nahofia gharama za ujenzi mpaka sasa.. Eneo ni linatosha fremu 5 hivi, unaweza kunisaidia hata kupiga hesabu za rough?
 
Wazungu walijenga nyumba za ghorofa kutokana na uhaba wa ardhi kwao. Nimekutana na Wafrika Magharibi pia mawazo yao ni ya kujenga ma ghorofa. Nikipowauliza sababu waliniambia kwao ardhi ni ghali sana. Kupata kiwanja cha kujenga nyumba inakulazimu uwe na kuanzia milioni 20 kwa pesa ya Tanzania. Wanasema ukijenga ghorofa hukosi mpangaji na wewe unapata na sehemu yako ya kuishi kwa amani.

Wengine wanasema wanajenga ghorofa kuyaona matunda ya mafanikio yake kwa macho. Sasa ninajiuliza sisi ardhi tunayo kubwa sana. Mpaka sasa bei ya kiwanja ni wastaniwa milioni tano mijini. Ni kwanini unawaza kujenga ghorofa kama una wazo hilo au ni kwanini ulijenga ghorofa?

Baadaye utauliza kwanini tutumie bati wakati nyasi zipo, baadaye kwanini tuweke tiles
Unatuchosha
 
View ya bahari.

Mfano mzuri Pemba Mnazi saa hizi ni kama Mbweni mpya. Watu wenye beach Front wana ghorofa kwa hiyo ukisogea nyuma kidogo na ukajenga ghorofa moja unaiona bahari ingawa kiwanja siyo beach front.

Hata Salasala hivyohivyo.

Ukitoka balcony unaiona bahari, au ukiwa bedroom.
mkuu wale samaki prones bado wa napatikana huko

kitambo sana kumbe kumekuwa kuzuri sana

vipi barabara ina lami kwa sasa kuelekea huko baharini
 
View ya bahari.

Mfano mzuri Pemba Mnazi saa hizi ni kama Mbweni mpya. Watu wenye beach Front wana ghorofa kwa hiyo ukisogea nyuma kidogo na ukajenga ghorofa moja unaiona bahari ingawa kiwanja siyo beach front.

Hata Salasala hivyohivyo.

Ukitoka balcony unaiona bahari, au ukiwa bedroom.
Pemba mnazi, Kimbiji bado bei iko chini na unaweza kupata eneo la kujenga na kupata upepo mwanana wa kutoka baharini...mkuu nitafute nikupe eka kwa milioni sita tu ujimwage na kupata upepo wa baharini
 
Ila ukijenga ghorofa ombea usije kufulia tu
Maana ghorofa nalo litafulia kimuonekano

Ova
😂😂😂 kuna utafiti ulifanyika kila mtu aeleze maana ya umasikini.
1. Kuna waliosema umasikini ni hali ya kukosa uhakika wa chakula.

2. Kuna waliosema uhakika wa mahitaji muhimu kama chakula, malazi na nguo za kujistiri ukivikosa wewe ni masikini.

3. kuna waliosema kushindwa kununua ticket ya ndege ya business class ni dalili ya umasikini

3. Kuna waliosema kununua wine badala ya champagne ni dalili ya umasikini.
 
Back
Top Bottom