Ni kwanini wanawake wa siku hizi wanapenda kumtawala mwanaume ?

Tatizo ulishaumbwa hivyo kutupenda sisi Wanaume, so endelea kujitekenya huku unacheka mwenyewe 7bu utazunguuuka weee hatimaye utarudia pale pale ulipoondokea...[emoji23]
Wewe ndo unazuga ila maandiko yapo yanajieleza nimekwambia niletee andiko hata moja linaloruhusu wanaume kuwasaliti wake zao au kuoa wake zaidi ya mmoja nipe japo andiko moja tu bila kutolea mifano ya wale mitume na manabii ambao walikuwa binadamu kama sisi na tena walikuja kutubu uzeeni
 
Exactly wewe umenielewa hata hawa unadhani hawaelewi basi? Wanaelewa sana ila basi tu wanapenda ligi.
 
Hatutaki kupigwa pingwa pasipokuwa na hoja za kimantiki
Hoja za kimatiki kama zipi? Labda nikwambie tu mwanaume anayestahili kuheshimiwa ni yule mwenye sifa hizi: mwenye mwanamke mmoja tu kama maandiko yanavyotanabaisha, mwenye mapenzi ya dhati kwa mkewe na kuyaonyesha, anayetimiza wajibu wake kwa mkewe na watoto na kusimamia nafasi yake kama mwanaume na mwenye kusikiliza mawazo ya mkewe na kumpa uhuru

Mwanaume mwenye sifa hizo tu ndo hatakiwi kupingwa na hata akikosea unaona kabisa ni bahati mbaya hivyo unamsamehe tu tofauti na hapa mwanaume utapingwa tu utake usitake maamuzi utakayoamua kuchukua ni juu yako ila ukweli lazima muambiwe siyo mnataka wanawake wakamilifu halafu nyie mna maovu kibao hayaelezeki
 
Hahaaa...hujakutana na Me wanaojitambua wakakunyoosha wewe ndiyomaana unatapa tapa tu hapa [emoji56]
 
Me gani aliyemsaliti Mke wake bila ya Mke kuwa chanzo/7bu [emoji848]
 
[emoji16][emoji16][emoji16] atatokea mtu kubisha tu hapo.
Huyo tushamzoea labda kashaathirika sana kwa kutendwa au amegubikwa na pepo la ubishi kupitia ushetani wa "HAKI SAWA" so tumuombee tu ili abadilike taratibu Mzee Baba [emoji851]
 
Kama hutegemei kupigwa pia hutofanya makosa yanayofanya upigwe, cousin sis wangu babaake alikuwa anampiga sana shangazi. Very violent akilewa ila akiwa mzima mtu mmoja very caring.

Sasa yeye amekuwa na hio spirit hataki mwanaume wa kumpiga ila mwenyewe ni mpole vibaya mno hata kuongea sana hawezi. Nachekaga namwambia hutakaa upigwe ukiwa msikivu na mtulivu, ila ukijifanya jeuri kuchapa kidomo utafurahia show.

Amebahatika kupata mtanga wanaenda fresh tu. Hateseki wala hapigwi japo jamaa nae mtu wa vyupa.
 
Me gani aliyemsaliti Mke wake bila ya Mke kuwa chanzo/7bu [emoji848]
Wapo wanaume wanaosaliti wake zao bila sababu kwa kisingizio cha tamaa tu tena wanakiri kabisa kuwa wao hawata wapate wanawake wenye sifa zote nzuri bado watachepuka tu

Halafu pia kwanini makosa ya wake zenu yawe chanzo cha ninyi kuchepuka? Kwani ninyi hamfanyi makosa? Haya mnataka na nyie mkifanya makosa wake zenu wawafanye nini?
 
Huyo tushamzoea labda kashaathirika sana kwa kutendwa au amegubikwa na pepo la ubishi kupitia ushetani wa "HAKI SAWA" so tumuombee tu ili abadilike taratibu Mzee Baba [emoji851]
Ni maombi tu tumfanyie huyu binti jamaa yetu. She seems to have gone through many abusive relationships ambapo watu hawa appreciate wema wake. Ana chuki flani ya kisaikolojia.
 
Hapo penye uhuru ndipo huwa mnapojisahau na kutaka usawa kwa kujiona nanyi ni Me.

So kwa Me anayejitambua kama mimi siwezi kutupatia uhuru kupita kiasi ni lazima niwe nabadilika kila wakati ushindwe kunielewa vzr akili zangu ili uendelee kuongozwa na mimi kama kichwa cha familia bora.
 
Sasa ni wanaume wangapi wanafanya hivyo? Mnajua kabisa wapo wengi wasiofanya hivyo ila hao hamuwaambii kutwa kuhangaika na wanawake tu oh sijui wanawake acheni hiki fanyeni hiki huwa tunaona kama maovu ya wanaume wenzenu mnayafumbia macho vile ila ya kwetu ndo mnayaona
 
Ndiyomaana ktk kuumbwa kwetu wewe uliumbiwa upendo na Me tuliumbiwa tamaa.

Bila shaka Biblia inanena wazi kuwa "upendo wa kweli huvumilia wala hausabu hesabu mabaya na kutoa toa kasoro"

Nadhani hadi hapo utakuwa ushajua kuwa Ke ndiye anastahili awe mvumilivu sana kuliko Me 7bu ni yeye ndiye aliyeumbiwa elements za upendo wala siyo Me

So acha kushindana na asili yako 7bu utapata tabu sana [emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…