Ni kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo yapo taratibu sana?

Nafikiri Swala la Lami litafuatia baada ya barabara ya Msongola Mbande kukamilika.

Si unajua wananchi wa Kitunda Kivule wasivyo na dogo.

Una wazo kama langu ila Mkuu mbona bar unaweza kuanza ujenzi Lami itakukuta kati kati ya project yako

Mimi mfanyabiashara sitaki kufukia hela.

Nitakapoona mkandarasi yupo site wa kujenga lami ya Banana mpaka Msongola. Ndipo nami nitaenda site kuanza ujenzi. Najua ndani ya miaka mitatu lami imekamilika nami bar yangu imekamilika.. naanza waletea kina misso missondo wawarushe watoto wa Kivule.
 
Sheria ichukue mkondo wake

Moja ya masharti ya Hati ya ardhi ni kuanza kujenga ndani ya miezi 36 tangu kumilikishwa ardhi
 
Umetisha mkuu
 
Sijajua ila nimekaa cheka... Naona freshi kabisa kabisa kwa wasiopenda fujo za dar...


Chanika nilienda 2017 kulikuwa kuna wazaramo tuu siku hizi unaweza potea...


Charles kilian toa neno kuhusi kigamboni yako
Ukitaka uishi kwa raha mustarehe pasi na fujo njoo ujenge Kigamboni.
Kilichonipendeza kingine ni upepo mwanana maana uoto wa asili bado upo pia maji ya kumwaga aisee.
Sehem ya uswahilini ni Vijibweni tu.
Miji mingine inayoendelea kujengeka taratibu ni kuanzia Kibada chekechea kuelekea Mwasonga nyuma karibia na magodani.
Kuanzia mji mwema kuelekea Cheka huko asahv wanauza viwanja kwa kupima.
 
Kg ikifikia level za Sinza nahamia Kimbiji huko.
 
Kuna baadhi ya Wahindi walishikilia maeneo Kigamboni, Magufuli aliwanyang'anya wengi hawakumuelewa. Hao ndio wakwamisha maendeleo. Wao wako Upanga wanawekea mapori wenzao.

Huo ndio ukweli. Wanaochelewesha maendeleo ni watu wanaokaa mijini. Ila wanamiliki viwanja nje ya mji na hawajengi

Hiyo siri alinipa afisa ardhi mzoefu aliyewahi hudumia manispaa zote za Dar es Salaam

Kwa sasa ni afisa ardhi temeke anaitwa .............

Aliniambia ukitaka sehemu inayokuwa haraka. Achana na Kigamboni wala sehemu ambayo Serikali imepima viwanja vingiii.. huko utasubiri miaka 20 ila mji haukui bado mapori utayaona yapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…