Kwa Mujibu wa Wikipedia, Wilaya ya Kigamboni imeanzishwa November, 2015. Hivyo ni Moja ya Wilaya za Karibuni kuanzishwa.
Nadhani changamoto kubwa ni uchache wa mtandao wa barabara za lami.
Japo kwasasa nimeona Kuna upanuzi wa barabara kipande cha Kibugumo hadi maeneo ya Hospitali ya Wilaya.
Ukiwa mtu wa kupenda Utulivu, Kigamboni ni pahali pazuri sana kuishi, na maeneo mengi ya ardhi yamepimwa.
Binafsi naishi hapo, na Kwa vile hupenda upepo wa bahari basi Kila weekend napita pita kwenye beach kupunga upepo wa bahari 🤗.
Chini hapa ni Moja ya beach nilitembelea huko Jana, Iko hapo Maweni - Mji Mwema.
View attachment 2924236
Kigamboni ni pazuri, atakaye na aje 🙏