Ni kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo yapo taratibu sana?

Ni kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo yapo taratibu sana?

Kigamboni, eneo la Pembamnazi serikali iliuza viwanja kwa wananchi tokea mwaka 2015. Mwaka leo eneo hilo bado ni pori. Barbara ya vumbi ni moja tu. Watu wanashindwa kujenga maana hakuna njia za kuingia kwenye viwanja (saiti). Serikali imepasusa Kigamboni sijui kwa nini. Anahitajika mkombozi ili kuikomboa Kigamboni
 
Kweli aisee Mimi mwenyewe naonaga kama pameshuswa hivi, wilaya kama ilala nunua popote maendeleo yanakujia fasta tuu
 
Kigamboni ni kubwa sana, wewe unataja huko mwanzo mwanzo, Toka dege nenda kimbiji Hadi Pemba mnazi, tokea kibada pita mwasonga nenda kimbiji au tundwi songani, mkamba, Shariff, sacos, ngoma mapinduzi ni mapori tu unaweza ukasema sio dar Kuna nyumba Hadi za tope
Nimeishi kigamboni huku barabarani, Vijibweni,kisiwani na Tungi kwenye nyumba za kupanga..ila inabd Mungu akijalia nitafute kiwanja sasa,maana miaka 5 ijayo pataamka sana.

Hii ni ishara nzuri, watu kuzungumzia tu
 
Daresalaam estate housing projects..nyingi ziko Kigamboni kuliko wilaya yeyote Ile Dar..
Watumishi housing
Avic town..
South beach geza
South beach Kisota
Nssf Mwongozo
Nssf kijichi
NHC kibada
NHC mwongozo
Hamidu city mikwambe...

Halafu mtu anasema Kigamboni haipigi maendeleo kisa hakuna bar nyingi kama Sinza
Hahaha sasa bro,nipo na castle light hapa..

Umenichekesha, kwamba watu wanataka bar na bata..Kigamboni hata mm nimeishi, bar zipo chache ila kuna utulivu kulinganisha na wilaya zngne za Dar..

Siku hizi nikitua dar, natulia tu TYPE C, hahah..au Asimwe.
 
Nimeishi kigamboni huku barabarani, Vijibweni,kisiwani na Tungi kwenye nyumba za kupanga..ila inabd Mungu akijalia nitafute kiwanja sasa,maana miaka 5 ijayo pataamka sana.

Hii ni ishara nzuri, watu kuzungumzia tu
Kama unataka kununua kiwanja kigambon mwisho kibada, mwisho GEZA, na hapo anazaa M15 20*20 huko kwengine utajua maendeleo hamna kigambon sehemu nzuri iliojengeka nindogo sana wewe umekaa huko mwanzo tembea wilaya nzima ujionee
 
Hahaha sasa bro,nipo na castle light hapa..

Umenichekesha, kwamba watu wanataka bar na bata..Kigamboni hata mm nimeishi, bar zipo chache ila kuna utulivu kulinganisha na wilaya zngne za Dar..

Siku hizi nikitua dar, natulia tu TYPE C, hahah..au Asimwe.
Bar chache maana wanaona hapajachangamka sana, biashara haitakua nzuri sana
 
Mbona husifii kwingine kunakoboreshwa??
Ni asilimia ngapi panaboreshwa ndani ya wilaya nzima? Sehemu kubwa ni mapori na barabara mbovu sehemu nzuri ni chache ukilinganisha na wilaya nyingne, angalia hata barabara za lami za kigamboni ni ngapi, halafu angalia temeke, ilala, ubungo na kino utapata jibu kua kigamboni ndio wilaya iliyo ya mwisho kimaendeleo Kwa mkoa huu wa dar
 
Nimesoma kila comment.
Kweli binadamu tunatofautiana. Mimi ningependa Kigamboni zijengwe barabara kama kilometa 500.
Yaani itengwe trilioni moja ya miundombinu ya Kigamboni. Angalau bilioni 200 kwa mwaka.
Halafu pabaki hivihivi, kusiwe na misongamano kama vijibweni.
Ikiwezekana vijibweni ipigwe greda watu wake wahamie Goba au Chanika.
Hatutaki fujo kigamboni, kajengeni bar na maduka ya mangi huko.
 
mimi nadhani ungetaja vitu ambavyo unique, sehemu ikiitwa wilaya kuwa na huduma muhimu kama maji, hospital sijui polisi, chuo kikuu ni mambo ya kawaida siyo kushangaa ni haki yako mwananchi
wilaya pekee yenye Zoo
Wilaya pekee isiyo tegemea maji kutoka mkoani
Wilaya inayoongoza kuwa na maeneo yaliyo pangwa na kupimwa.
Wilaya yenye miradi mingi ya majengo ya makazi/apartments.
Wilaya yenye eneo kubwa la Viwanda
Wilaya yenye visiwa vingi vya utalii
Wilaya pekee isiyo kumbwa na adha ya mafuriko
Wilaya yenye Viwanja bei nafuu
Wilaya isiyo na foleni
 
Nimesoma kila comment.
Kweli binadamu tunatofautiana. Mimi ningependa Kigamboni zijengwe barabara kama kilometa 500.
Yaani itengwe trilioni moja ya miundombinu ya Kigamboni. Angalau bilioni 200 kwa mwaka.
Halafu pabaki hivihivi, kusiwe na misongamano kama vijibweni.
Ikiwezekana vijibweni ipigwe greda watu wake wahamie Goba au Chanika.
Hatutaki fujo kigamboni, kajengeni bar na maduka ya mangi huko.
Pashasuswa, hizo hela za kujenga barabara zinatoka wapi miaka yote Kuna sehemu mvua zikinyesha hapapitiki, ishu sio maduka na bar
 
wilaya pekee yenye Zoo
Wilaya pekee isiyo tegemea maji kutoka mkoani
Wilaya inayoongoza kuwa na maeneo yaliyo pangwa na kupimwa.
Wilaya yenye miradi mingi ya majengo ya makazi/apartments.
Wilaya yenye eneo kubwa la Viwanda
Wilaya yenye visiwa vingi vya utalii
Wilaya pekee isiyo kumbwa na adha ya mafuriko
Wilaya yenye Viwanja bei nafuu
Wilaya isiyo na foleni
Wewe unajivunia zoo wenzako wanajivunia miundombinu
 
Hebu tujuze Chanika huko Miundombinu ipi ni mizuri, anzia hapo ?
Kwa miundombinu ipi imeizidi Kigamboni.
Kama unataka kupambanisha, linganisha ilala na kigamboni, Mimi nazungumzia wilaya ya kigamboni, chanika Iko ilala, kwahyo kama unataka tuanze kuzilinganisha ni kati ya kigamboni na ilala, sio chanika na kigamboni, kama unataka kuifananisha chanika na Kisarawe II ntakuelewa, hapo utapata jibu
 
Attachments

  • 20240229_152429.jpg
    20240229_152429.jpg
    428.4 KB · Views: 17
mimi nililenga kukupinga huko coz Ulisema Chanika imeendelea kuliko Kigamboni...

Na lazima ukumbuke, Ilala ni Wilaya Kongwe sana,ndipo kwenye Ikulu na Majengo ya serikali.
Lakini mpaka leo kuna kata takribani 10 zina mapori na Miondombinu mibovu kinoma....
Ilala uzuri wake unaishia Airport tu,huku kwengine we paskie tu.
Ubungo nayo ni wilaya kongwe? Haya tuanze kuifananisha chanika na kata ya kisaraweII, wapi mjini wapi porini?
 
Hivi tunaishi Dar tofauti ama...
Hivi kwa mfano wilaya ya Ubungo: Mbezi,Goba,Kibamba,Kwembe na Msigati kuna miundombinu ipi ambayo iliwekwa baada ya kutangazwa Wilaya .
Unajua barabara za haya maeneo ilivyo kweli...
Ushapita kipindi cha mvua katika haya maeneo...
Unajua adha ya maji?
Au wewe unaongelea miundombinu ipi?
Tuanze kutaja kata moja moja tulinganishe maendeleo ya miundombinu yake, nadhani wewe utakua unaongelea kigamboni eneo Dogo sana, haujazunguka ukaona walima matikiti na wakata mkaa, na nyumba za matope, watu wanakunywa maji ya visima machafu, zunguka kigamboni yote usiongelee kaeneo kadogo
 
Hivi tunaishi Dar tofauti ama...
Hivi kwa mfano wilaya ya Ubungo: Mbezi,Goba,Kibamba,Kwembe na Msigati kuna miundombinu ipi ambayo iliwekwa baada ya kutangazwa Wilaya .
Unajua barabara za haya maeneo ilivyo kweli...
Ushapita kipindi cha mvua katika haya maeneo...
Unajua adha ya maji?
Au wewe unaongelea miundombinu ipi?
Kwanza wewe unakaa kigamboni sehemu gani?? Inawezekana haujui hata uhalisia, Mimi Nina nyumba na shamba la mpunga kigamboni naongea nnachokijua
 
Back
Top Bottom