Kwanza mtazamo wa maendeleo kwa mtu. Inatofautiana mtu mmoja na mtu mwingine.
Kwa wale wanaoamini maendeleo ni watu kuwa wengi, mji kuchangamka, makelelele, vuruguvurugu, mara gari linapita, mara pikipiki zinakimbia, watu mara wana sherehe, vigoodoro wadada wanatikisa matako yao, mara huku bar, mara huku disko, mara singeli. Mtu ambaye kiufupi anaamini maendeleo ni amshaamsha, lazima atataka amshaamsha. Kuna wengine wanaaamini maendeleo ni huduma bora na utulivu pamoja na ukimya. Mara nyingi ni watu wenye pesa zao na wanapenda Sehemu ya kutulia na kurelax.
Sasa kwa uzoefu wangu ni kuwa bei ya viwanja ndio inaamua aina ya eneo, spidi ya kukua na kupangika. Maeneo ambayo bado watu wanauziana kwa kupima miguu na kiwanja ni bei nafuu lazima hilo eneo litakuwa na wateja wengi na kutachangamka ndani ya muda mfupi sana, ukilinganisha eneo ambalo kiwanja kimepimwa kitaalam na serikali, kwanza bei ni kwa square meters tena unaona square meter moja inacheza kuanzia 8000(porini) mpaka 30,000-50,000(sehemu iliyo na huduma) 55,000-85,000(sehemu iliyochangamka sana na yenye huduma zote na majirani wapo)
Maana yake kiwanja cha miguu 20x20 ambacho mtu anapata kwa 800,000 mpaka 1,600,000 ambayo ni bei hiyo watanzania wengi wa kawaida wanaimudu ndio kitanununulia haraka na kuendelea kwa haraka.
Ila 20x20 ikishakutana na wataalam wa ardhi waje waigeuze kuwa square meters zinakuwa 400sqm. Ambayo kwa bei ya kibosi itaanzia 4,000,000-8,000,000. Na sehemu yenye huduma itakuwa 12,000,000- 20,000,000. Sasa hizo bei za juu ndio bei za huko kigamboni. Sehemu iko porini mno ila bei milioni 20, na sasa Matajiri wao wanachukua maeneo makubwa tu kuanzia 10,000sqm mpaka 50,000sqm wengine mpaka 100,000sqm. Halafu wanakaa nayo wanatulia tena kwa bei ambazo ni highly overpriced mpaka 200m-500m. Maana yake huko kuja kuendelea bado sana. Mpaka hao Matajiri waanze kuja kuendeleza sio leo. Hawana njaa wala shida ya nyumba. Sanasana hao Matajiri wanatumia hizo hati ilikukopea hela benki ili kukuza biashara zao. Sanasana NMB na CRDB n.k.
Muda umefika serikali ikubali kupima ardhi na kuuza kwa bei nafuu kwa ajili ya wananchi wa kawaida bei ya square meters 1 iwe chini ya 2000. Masuala ya kuuza bei ya kiwanja bei juu kuanzia 10,000@sqm mpaka 50,000sqm hayasaidii wananchi.