Ni kweli Askari Polisi wengi hawana ajira za kudumu? Ni kama vibarua?

Ni ajira ya kudumu, RPC hawezi kumfukuza kazi ila anaweza kupendekeza afukuzwe kazi, baada ya huyo polisi kupelekwa kwenye mahakama ya kijeshi na kutolewa ushahidi juu ya makosa aliyofanya akishatoa mapendekezo ya kumfukuza kazi baada ya kumkuta na hatia anatoa ripoti kwa wakubwa wake wa juu kina IGP ila mwisho atakae msomea hukumu ya kumfukuza kazi ni RPC

akifukuzwa anauwezo wa kukata rufaa pia na akarudi kazini kama kafukuzwa kimakosa na akalipwa fidia.

Ila polisi ni miongoni mwa kazi ngumu sana.
 
Kwa mujibu wa PGO,inamtambua Police Officer kama Askari mwenye kuanzia Nyota Moja(Assistant Inspector)na kuendelea. Kuanzia Constable mpaka Station Surgent(Meja) hao wanatambulika kama Rank and File.
asante sana sana
 
Weeee basi Tanzania tumepiga hatua kumbe Mpwa. Thanks Kwa maelezo
Hapana, kuna hasara pia zinazotokana na kuzifanya hizi kazi kuwa za kudumu badala ya mikataba mifupi mifupi.

Mkataba kwa mwanajeshi Marekani ni miaka minne full ya active duty na miwili 2 ya reserve. Unaweza kuongezewa mkataba wa kazi kulingana na uhitaji na umuhimu wako, ndio hao unawaona wengine wanakuwa maofisa wa jeshi.
 
Kuna kitu Yoda hujaelewa kabisa.
 
Hawa ajira yao inapaswa kuwa ya mkataba wa miaka ata 7, kwasababu ikiwa ya kudumu wanajisahau sana, hawatendi haki, rushwa na dhulma imekithiri.
 
Ni kweli askari polisi wana mikataba.
 
Kwa mujibu wa PGO,inamtambua Police Officer kama Askari mwenye kuanzia Nyota Moja(Assistant Inspector)na kuendelea. Kuanzia Constable mpaka Station Surgent(Meja) hao wanatambulika kama Rank and File.

ofisa anayetambulika ni nyota 3 na kuendelea.labda ungesema mtumishi mwajiriwa ni kuanzia nyota 1 na kuendelea.

ila kuna Afisa wa polisi.
huyu ni askari yeyote wa polisi unayemuona.
 
nadhani wanazo ila zitakua zile za chini kabisa kwa baadhi yao, nazungumzia hawa wadogo kwa rank
Duuuh! basi yawezekana ndiyomaana wengine wanaamua kula rushwa,maana wanajua muda wowote wanaweza kufukuzwa kazi au kupata majeraha kutokana na utimizaji wa majukumu yao...,sasa kama askari polisi anakua hana bima yenye kueleweka,si tatizo hilo aisee,mi naona hili jeshi la polisi, yawezekana viongozi wao hawako makini.
 
ofisa anayetambulika ni nyota 3 na kuendelea.labda ungesema mtumishi mwajiriwa ni kuanzia nyota 1 na kuendelea.

ila kuna Afisa wa polisi.
huyu ni askari yeyote wa polisi unayemuonconstabla.
Kwa maelezo yako, inamaana askari wa jeshi la polisi,yule ambaye yuko PLAIN,nikimaanisha constable,siyo mwajiriwa wa jeshi la polisi,inamaana anatambulika kama KIBARUA tu,anaenda kituoni,akifanya kazi,anaandikiwa,mwisho wa mwezi anapigiwa hesabu,analipwa,anasepa zake,sindiyo?
 
kwa lugha inayeoeleweka ni kwamba yuko ktk muda wa matazamio bado.

wakati taasisi nyingine ni miezi6,mwaka nk,hawa ni miaka 12.
sasa hiyo miaka 12 ikikitimia kimahesabu anatakiwa awe amefikia cheo hicho cha nyota moja na kuajiriwa rasmi,lakini haiwi hivyo.

miaka 12 inamkuta mtu hata cheo cha pili cpl hana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…