Mie sikubaliani na hili, na naona kama raisi akifanya hivi anakosa busara na ustaarabu.
Kama ambavyo unapaswa kumwambia kimbele mtu kabla ya kutangaza kumteua kuwa waziri, unapaswa kumtaarifu mtu kimbele kawma unamtengua mtu uwaziri. Kinyume na hilo ni kukosa ustaarabu, hata kama wewe ni raisi.
Kuna shida gani kumwambia Nape, hata kutumia maofisa wa Ikulu, kwamba Raisi atatengua uwaziri wako, angalau hata masaa mawili kabla ya kutangaza rasmi? Wanaogopa mtu atatangaza kujiuzuru ili isionekane ametenguliwa? Kuteua au kutengua hakupaswi kuwa jambo la kushitukizana.
Haya mambo ya kukosa ustaarabu ndio maana wanaishia kuteua watu waliokufa