Ni kweli hali ya maisha imekuwa ngumu, na pia ni kweli hizi tozo hazikubaliki, sasa wananchi tuseme kwa vitendo imetosha

Ni kweli hali ya maisha imekuwa ngumu, na pia ni kweli hizi tozo hazikubaliki, sasa wananchi tuseme kwa vitendo imetosha

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Kwa lugha rahisi tu wananchi sisi ndio wenye nchi na huyu Mwigulu Nchemba na mama sisi ndio mabosi wao, sisi siyo vijakazi wao hili lieleweke dhahiri shairi.

Kwakuwa ugumu huu wa maisha hauchagui itikadi za vyama au wasiokuwa na vyama, kupitia thread hii tukusanye maoni ya wananchi jinsi ya kuratibu na kufanya maandamano makubwa nchi nzima yasiyo na kikomo kupinga maisha magumu na hizi tozo za kipuuzi.

Ni muda mufafaka Sasa Kwa Watanzania tuungane tuweke vyama pembeni, dunia nzima maandamano yenye mafanikio ni ya kiraia siyo ya vyama vya Siasa, nguvu mnayoitumia kwenye Simba day na Yanga day tukiunganisha pamoja kukataa kuswagwa kama Ng'ombe kwenye nchi yetu, Mwigulu ataachia mwenyewe ofisi ya umma na mama atasikia kilio chetu.

Uamuzi ni wetu tuendelee kuwekeza kwenye ujinga na mambo yasiyokuwa na Tija kama lete mzungu au tuchukuwe hatua Sasa.

Kama hatuwezi kuchukuwa hatua Sasa tukae kimya jumla tuache ulalamishi tuache serikali itekeleze ilani ili ituletee maendeleo na watu wote tukae kimya.

Sasa nakaribisha maoni na ushauri namna ya kuratibu maandamano nchi nzima kupinga maisha magumu, hili linawezekana timiza wajibu wako, hili vuguvugu likipamba moto na wakaona tupo serious watarekebisha tatizo kabla ya maandamano makubwa nchi nzima.
 



 
Achana na kichwa Cha habari

Wakuu hizi tozo zinazoanzishwa Kila uchwao huku gharama ya maisha ikipaa Kila siku Hawa viongoz hawaoni wanachotufanyia

Vyakula vipo bei juu Sana lakn bado tunaongeza Kodi tuu na tozo juu lengo n nini?

Rais wetu yeye yupo kimya tu anafurah tu sisi kuumizwa na hili

Tujitafakari watanzania Kama nafas ya juu inaweza kushikwa na wanawake au la
CCM nyie ndio chama tawala hizi too hazimuumiz mwana TLP UPDP CHADEMA TU Bali zinatuumiza wote naomba Sana fanyeni kumshaur Rais juu ya hili

Hali n mbaya Sana mtaani



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wananchi wanalalama sana kuhusu kodi
watu wa fedha TRA mkakae mlitizame hili
Yeye ni sehemu ya tatizo, Sasa ni muda wa umma kuonesha nguvu yetu.

Tunashangilia uchaguzi wa Kenya huku tukidhani hayo wameletewa kwenye golden plate.

Wakenya walikataa kudharauliwa na wakachukuwa hatua Sasa hivi Kenya ni heshima, aliyeshinda uchaguzi kakaa Kwa adabu na Rais anayemaliza muda wake kakaa Kwa adabu.
 
Yaani Hela inakuwa hivi

Ukitoa Bank wakutana na yafuatayo

Bank charges
VAT
Gov Levy

Baada ya hayo yote bado serikali inakula tena 30% ya corporate tax

Serikali inatuumiza kwenye kila VAT maana hiyo yaja kwetu moja kwa moja
 
Kwakuwa Idara ya usalama wa Taifa wana dawati la Siasa Nina uhakika wanafuatilia hii thread ambayo tuko serious hatubeep.

Naomba wachangiaji wote tudhibiti hasira zetu tusitukane viongozi wetu, tuwe objective mwisho wa siku ni conclusion ya kuingia barabarani, wale wanaondelea kushupaza shingo waendelee tu wananchi tumeshaamuwa hatuna cha kupoteza.
 
Kwakuwa Idara ya usalama wa Taifa wana dawati la Siasa Nina uhakika wanafuatilia hii thread ambayo tuko serious hatubeep.

Naomba wachangiaji wrote tudhibiti hasira zetu tusitukane viongozi wetu, tuwe objective mwisho wa siku ni conclusion ya kuingia barabarani, wale wanaondelea kushupaza shingo waendelee tu wananchi tumeshaamuwa hatuna cha kupoteza.
Ungekuja na jina lako kamili ungeeleweka zaidi

Kuhamasisha maandamano kwa ID fake ni umbwiga
 
Tuanze na kugomea sensa kesho
Kugomea sensa ni Sawa na kujihujumu sisi wenyewe, takwimu zina umuhimu wake mkubwa.

Sensa iendelee lakini haiwezi kuzima movement ya maandamano ya nchi nzima.

Tutatumia pia mbinu za South Africa wanavyoandaa oparesheni Dundula huwa hawana kelele nyingi Ila subiri siku ya watu kuingia barabarani ndio utawapenda.
 
Wa kuandamana ni Sisi wabongo? Thubutuuuu

Usikute wewe mwenyewe unaandika hii mada huku umelala kitandani unasubiri mama watoto spoke chai unywe uende mishe..

wabongo mfumo wa ujamaa umetufanya tuwe km mbwa Koko,wazee wa kubweka Ila hatuna madhara
 
Kuna kiongozi aliwahi wafananisha Watanzania sawa na Maiti,Ni ajabu maiti akaongea kwa vitendo.kingine watanzania wa wapi unaozungumziwa mtoa mada hawa ambao asubuhi mpaka jioni wanabishana kuhusu mpira🤷🏼‍♀️
 
Kugomea sensa ni Sawa na kujihujumu sisi wenyewe, takwimu zina umuhimu wake mkubwa.

Sensa iendelee lakini haiwezi kuzima movement ya maandamano ya nchi nzima.

Tutatumia pia mbinu za South Africa wanavyoandaa oparesheni Dundula huwa hawana kelele nyingi Ila subiri siku ya watu kuingia barabarani ndio utawapenda.
Mabuza
 
Back
Top Bottom