Kumbuka siyo kila kitu kina linganishwa. Yani Unalinganisha Texas Marekani na Tanzania? Dunia ya kwanza na Dunia ya 100 sijui?
Kipato chetu na chao havilingani, na hata standard za huduma wapatazo ni tofauti na tupatazo hapa kwetu. Na kama ilivyo kwa Tanzania hata marekani raia wengi hawana health insurance kwa sababu hawawezi kuzimudu. Wengi wenye Health Insurance huzipata kupitia kwa waajiri wao kama tu ilivyo hapa kwetu.
Gharama inatokana na package anayo weza kumudu, hata wao siyo suti kwamba one fit all. Ni wachache wanaweza kujinunulia Health Insurance huko Texas Marekani kama tu ilivyo hapa kwetu.
Kuhusu gharama, nadhani wao hupata value of their money, hapa kwetu hakuna kitu, kila kukicha NHIF wana hamisha magoli, utasikia utapata vipimo vya awali vya damu, vipimo zaidi utalipia, au utasikia huduma za tiba ya mionzi na uchunguzi wa mionzi utajilipia. Lakini utakuta wenzetu kule hizo huduma za uchunguzi wanapata zote kwenye basic package isipokuwa specialized procedures ndizo wanabidi wajipange.
Na hata hivyo wao sheria inawasaidi, mgonjwa hanyimwi huduma hata kam ahwezi kumudu, huduma atapata, deni litapelekwa kwa serikali.
Muhusika atakua na deni lakini halitomfanya ashindwe kuishi maisha yake, kwa maana nyingine siyo lazima alipe.
Hapa kwetu Insurance gharama iko juu sana ukilinganisha na vipato vya wananchi waliowengi. Sioni kama ni sawa kulinganisha gharama anazolipa mwananchi wa Texas marekani na hapa kwetu.