Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Haijalishi, je umma wa Watanzania unamudu hizo gharama? Tukizungumzia umma ni lazma ufuatilia the lowest income earners of the country. Mtu analipwa laki na nusu kwa mwezi. Je, akiumwa anatibiwaje hapo?Mkuu Ungeelewa Usingeona Kuwa Jibu langu ni la kifedhuli!
Tatizo watu Wengi mnadhani Kuwa hospitali za Serikali.Huwa zinapewa Pesa ya Kujiendesha..
Lakini Ukweli utaujua kama Ukiwa ndani ya Field hii..
Nitarudia tena Serkali haitoi ruzuku wala offer ya pesa Kwa hospitali yoyote..
Watumishi Wa afya ,Madaktari l, Nurses na wafanyakazi wote wanao wahudumia Nyinyi Mnafikiri wanatoa wapi Posho?? Na Motisha?
Madawa ambayo mnatumia, Na vifaa mnavyotumiwa kuhudumiwa vinatoka wapi??
Mnafikiri uendeshwaji wa Hospitali, Ukarabati na Vitu vingine vyote kwa Ujumla Pesa zimatoka wapi?
Wakati mwingine ni vyepesi sana Kulaumu kwakuwa Haujui Hali ilivyo, Sisi tulio ndani ya Hiyo hali.tunajua Maumivu yake..
Na ndo maana Nikakwambia kwa huduma Unayopewa Humo na Hadhi ya Hospitali yenyewe gharama ya 50k Kwa Siku Ni ndogo sana...
kuna Kipimdi nilikuwa na Rafiki angu Mmoja ni Mbunge..
Kuna Muda tulikuwa Tukibishana sana Kuhusu haya mambo (Kama wewe Hivi) tulifikia Mpaka Kutukanana..
Alipopata Ubunge akapelekwa kamati ya Afya Baada ya Kujua Kuhusu Hospitali zinavyoendeshwa baada ya Miaka miwili ndani ya kamati ya afya aliniita na Kuniomba Msamaha..
Kuna Muda Ni vema Kufanya Research ya Kina Kuhusu Kitu kabla hujalaumu na Kubeza
Huyo mbunge rafikio anaweza kwenda kulala hata wodi ya million kwa siku maana bunge linamlipia. Wewe unaweza lipa hio elfu 50 maana unaweza kuwa unatengeneza 6 times the sum of money kwa siku.
Je, yule mtanzania muuza maji ya kandoro atawezaje kumudu kumlipia mzazi wake alielazwa elfu 50 kila siku?