Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ni mpwa au sio mpwa?
Watu wengine mnashangaza Sana mawazo yenu na namna mnavyofikiri, kwa hiyo akiwa mpwa wa Rais haruhusiwi kuwa kiongozi? Akiwa mpwa wa Rais anakuwa amekosa sifa za kuwa kiongozi? Akiwa mpwa wa Rais Hana haki ya kuteuliwa ? Kwa hiyo akili yako na mawazo yako maana yake mpaka leo George bush au Uhuru kenyata wasingefika walipo kiuongozi na kuwa Marais wa nchi zao kwa kuwa baba zao walikuwa Ni marais,. Hillary Clinton asingefika alipofika kiuongozi kwa kuwa mume wake alikuwa Rais. Acha mawazo mfu na ya kizamani, kinachoangaliwa ndani ya CCM Ni uwezo wa mtu kiuongozi katika kumudu mujukumu ya nafasi husika pamoja na sifa alizonazo kiuongozi kiujuzi kielimu kiuzoefu kitaaluma na mambo mengine Kama hayo. Ndani ya CCM haiangaliwi Dini ya mtu au kabila la mtu au ukoo wa mtu au fedha za mtu au sura ya mtu au ukanda wa mtu.Hakuna ubaguzi wa aina hiyo ndani ya CCM na ndio maana CCM inaendelea kuungwa mkono na mamillion ya watanzania na kuwa kimbilio la wanyonge,. Ndani ya CCM yeyote anaweza kuwa kiongozi ikiwa amekidhi sifa na vigezo vya nafasi anayoomba bila kujari Hali yake ya kiuchumi,hakuna ubaguzi ndani ya CCM ndio maana watu wanatimiza ndoto zao bila shida yoyote Ile Wala vizingiti vya kibaguzi Kama ilivyo katika vyama vingine.