Tatizo lenu hamna akili ya kuelewa hoja ya mleta mada.
Mleta mada
Sexless anazungumzia nepotism. Je, mnaelewa maana ya nepotism au mnakurupuka tu mifano yenu isiyokuwa na kichwa wala miguu.
Unatoa mfano wa George Bush Junior, Uhuru Kenyatta, Hussein Mwinyi nk. Je, George Bush Junior aliteuliwa na baba yake kugombea urais wa Marekani?
Je, Uhuru Kenyatta aliteuliwa na baba yake marehemu Jomo Kenyatta kugombea urais wa Kenya? Au Hussein Mwinyi aliteuliwa na baba yake Ali Hassan Mwinyi kugombea urais wa Zanzibar?
Jibu ni dogo na rahisi. Hapana. Sababu wakati wanagombea urais wazazi wao hawakuwepo madarakani.
Lakini, kwa issue ya Shaka ni tofauti. Samia yupo madarakani kama Rais na mwenyekiti wa chama halafu anamteua ndugu yake kushika wadhifa mkubwa ndani ya chama, hiyo ndiyo inaitwa "nepotism", kupeana nafasi za kazi au kupandishana vyeo au kuteuana kindugu. Hii ndiyo hoja ya mleta mada.
Sasa turudi kwenye hoja ya msingi, Je, Shaka, ni kweli ni mpwa wa rais Samia?
Na kama ni kweli, Je, uteuzi wake siyo nepotism??