Ni kweli kuwa Shaka ni mpwa wa Rais Samia? Na kama ni kweli CCM mmebariki nepotism hii ndani ya chama?

Ni mpwa au sio mpwa?
 
Ridhiwani ni mtoto wa Kikwete rais mstaafu, Salma mama yake Riz1. Hussein ni mtoto wa mwinyi, Karume nao baba na mwana Marais. Sasa ajabu ya samia na Shaka iko wapi?
Daah! Utanifanya niikimbie nchi hii. CCM adui wa haki.
 
Shaka yupo kwenye duru za CCM/ UVCCM kabla wewe hujaingia JF na kutengeneza account yako. Ni kwamba tu Mwendazake aliwavuruga mwaka 2016.
 
kinachoangaliwa ndani ya CCM Ni uwezo wa mtu kiuongozi katika kumudu mujukumu ya nafasi husika
Kwahiyo uwezo wa kiuongozi wa paymaster general (mpwa wa JPM) Dotto James ulifika mwisho mara tu Magufuli alipofariki?

Uwezo na umahiri wa kiuongozi wa mpwa wa Magufuli Herry James ulofika mwisho baada tu ya Magufuli kufariki?

Unapoleta kioja huku JF uwe umejipanga ndugu. Huku siyo Facebook.
 
Kwani hao wapo wapi kwa Sasa? Nafasi walizo nazo kwa Sasa hazitoshi kuwatumikia watanzania? Ulitaka wapewe nafasi zipi ili moyo wako uridhike?
 
Wengi hawajui Kiingereza.

Shaka anaweza kuwa ndugu yake Samia, na Shaka akawa kiongozi ndani ya chama au Serikali, na ikawa haina tatizo. Lakini kama Shaka ni ndugu yake Rais Samia, halafu Samia akamteua Zhaka kumpa madaraka, hilo ni kosa kubwa kimaadili.

Watu kadhaa wamechangia mada bila hata ya kuelewa hoja. Eti wanafananisha Kikwete, Salma na Ridhiwan. Nadhani ni kwa sababu ya upeo na uelewa mdogo.

Kikwete hakumteua Ridhiwani wala Salma. Mwinyi hakumteua Hussein, wala marehemu mzee Jomo Kenyata hakumteua uhuru.
 
Kwani hao wapo wapi kwa Sasa? Nafasi walizo nazo kwa Sasa hazitoshi kuwatumikia watanzania? Ulitaka wapewe nafasi zipi ili moyo wako uridhike?
Kwann walitumhuliwa kule walikokuwa? Dotto James alikuwa ameatamia mihela ya nchi na Herry James alikuwa anakinyaga chama. Kwann waliondolewa mara baada ya mjomba wao kufariki???

Na hata shaka siku Samia akiondoa mguu ikulu atapeperushwa kama unyoya. Yangu macho. Acha kutetea ujinga.
 
Acha ramli na ndoto
 
Kwa wazanzibar kuwa ndg inawezekana. Maana wazenji waliosomasoma karibu wote ni ndugu.

Sioni kama kuna tatizo katika hilo ili mradi tu awe sifa stahiki. Mbaya ni kuteua wasio na sifa kwa kigezi cha undugu au kujuana!
 
Sifa hizo zimeonekana baada ya Samia kuingia ikulu?
Mkuu sijasema kwamba ana sifa. Nimesema ilimradi awe na sifa stahiki.
Sasa kama anazo au hana, waliomteua ndio wanajua.
Na kama hata aliyemteua naye hana sifa, basi hapo ni ngoma droo!

Muhimu ni kutengeneza njia ili watoto, wapwa, wajukuu nk, na wao wasijekulalamika kama mtoa hoja. Nepotism haiwezi kuisha
 
Shaka ndiyo nani wengine huku vijijini nishida kupata taarifa zote za mjini[emoji29]
 
Shaka ndiyo nani wengine huku vijijini nishida kupata taarifa zote za mjini[emoji29]
Mtu fulani hivi kapewa kazi ya kuieneza ccm. Huko kijijini kwenu hajafika?
 
Mbona wamejazana kifamilia huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…