Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Ukiipitia hyo CV yake inatosha kabisa mwenda kugombea huko, japo kushinda itategemea na ambao atashindana nao.
 
Mkuu, kwa kuwa unajitambulisha kwa Jina la Dr Mambo Jambo, naomba kuuliza swali kutokana na ulichoandika. Je, Fellowship ya Moyo peke yake, inatosha kumfanya Daktari yoyote kuwa DaktrBingwa wa Magonjwa ya Moyo?

Zaidi, unaweza kutueleza sifa za Kitaaluma za Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo?

Itapendeza kunipatia majibu ya maswali haya na kufanya huu mjadala kuwa na tija zaidi.
Mkuu samahani, naomba kuuliza.

NI nani alisema janabi Ni daktari bingwa ea magonjwa ya moyo, au nani alisema janabi anatibu watu moyo, au nani alishawai kutibiwa na janabi moyo?

Au ni zile clip zake zinakuchanganya?
 
Kuna mtu hapo nimemuuliza swali jepesi anajua fellowship ya cardiology inachukua miaka mingapi na inahusu nini hajajibu .

Hapo ndio nilipocheka na kufunga mjadala maana naona nitajadiliana na mtu ambaye mada imemzidi kimo.
Watu wanabisha ila Hata Fellowship hawajui maana Yake...
Wanahisi Fellowship Ni Course ya miezi sita..
Ile Ni kwenda Kula Mashule Wangapi hawafiki Huko?
 
🤣🤣 ndo maana Nimekuuliza Unajua Ulichokuwa unakisema..
FEllowship zinaanzia Miaka 2 Mpaka 10 inategemea Na Aina Ya Fellowship..
Sasa hayo mafunzo maalumu yenye Miaka mimgi ndo tunaita Fellowship..🤣🤣🤣
Hapana.
Kuna fellowship nyingi sana za miezi mpaka mwaka mmoja tu. Hutegemea professional, taasisi, na malengo. Hazina muda mahususi wa kufanana. Urefu wa muda wa mafunzo hauamui mafunzo kuitwa fellowship. Hakuna uhusiano wowote kati ya muda wa mafunzo na hayo mafunzo kuitwa fellowship.
 
Professor Janabi hana qualification yoyote ya kutibu moyo kibingwa, hana. Hakusomea popote na hakuwahi kutambuliwa na baraza la madaktari hapa Tanzania kama Daktari bingwa wa moyo. Na hata pale Muhimbili hajawahi kutibu moyo mtu kibingwa tangu awepo. Hana huo uwezo.
Hayo mavyeo sijui wanayapataga wapi
 
Sijui chochote kuhusu NAPLEX wala miaka ya kusomea Doctor of Pharmacy huko USA.

Ninachokifahamu ni kuhusu sifa za mtu kuwa mfamasia hapa Tanzania. Na ziko mbili tu.
1. Kuwa na degree ya Pharmacy inayotambulika na TCU.
2. Kusajiriwa katika bodi ya famasi ya (katika hali ya kawaida mhusika anfanya na kufaulu mtihani wa bodi)
Ngoja sasa nikusaidie jibu ni jepesi.

Mtu mwenye leseni ya NAPLEX akifika Tanzanzia anapractice moja kwa moja bila mtihani wowote atakachoapply ni ile registration ni kama $75.

Ila mtu mwenye leseni ya PCTZ akija US lazima afanye training kadhaa upya na lazima afanye application na kufanya NAPLEX ndio ataruhusiwa kupractice.
 
Unazungumzia habari za kina Dr. Sarungi ambao zama hizo walikuwa ni wao pekee kwa uchache walikuwa wamesomea ubingwa, tena nje kwa kuwa Tanzania hakukuwa na vyuo vya kufundisha mabingwa wa kutosha wa fani kama mifupa. Kwa sasa mambo yamebadilika mnoo.

Nenda sasa pale Muhimbili (MOI) ukakutane na vijana wadogo na wamoto sana wakijifunza vilivyo kuchoronga na kurekebisha mfupa kisasa kabisa.

Mwisho labda nikuambie ukweli, karibu madaktari bingwa wote wazuri wa pale Muhimbili ukija Aga Khan, Regency, Selfee, Hindu Mandal utakutana nao tena. Ni madaktari wale wale.
Hii nakubaliana na wewe,mfano Dokta Kamugisha utamkuta hospitali zote hizo
 
Mimi sibishani, nakuambia ukweli wa kiujumla jumla, sio uwezo binafsi wa mtu mmoja mmoja baada ya kuhitimu. Ikiwa kiujumla jumla utalinganisha (kwenye kutibu wagonjwa) wahitimu wa udaktari waliosoma Tz dhidi ya wahitimu wa udaktari waliosoma USSR, wote wakiwa fresh from university, utagundua tofauti kupitiliza, watanzania wametangulia mbali mnoo. Na siri ni ile ile, wahitimu wa taaluma ya udaktari kutoka Tanzania wana clinical practice exposure kubwa, nzuri na kutoshea mnoo.

Kama uamini hilo, nenda hata sasa huko mahospitalini utakuja kuniambia hapa hapa. Mimi nilikuwa mbishi kama wewe, baada ya kuchunguza mwenyewe nilibadili mtazamo kabisa. Nilikuwa siwakubali wala kuwaelewa wahitimu wa udaktari kutoka Tz, baada ya kuuguza mara kwa mara na kwenda hospitali mara kwa mara niligundua kitu cha tofauti kabisa.
Ndugu yangu achana na conclusion za namna hiyo, hizo ni conclusion za kilayman sana. Wagonjwa wangapi wako wametibiwa na dr wa urusi na wangapi wametibiwa dr wa muhumbiri then ukaja na hitiimisho kwamba dr wa urusi ni mbovu kuliko dr wa tanzania!
 
Watu wanabisha ila Hata Fellowship hawajui maana Yake...
Wanahisi Fellowship Ni Course ya miezi sita..
Ile Ni kwenda Kula Mashule Wangapi hawafiki Huko?
Ni ajabu sana anayehoji ubora wa elimu ya U.S ndio mtu ambayo nchi kuna kozi ilianzisha inaitwa ADDO kama sikosei nilishangaa eti mtu anasoma mwezi mmoja na anaruhusiwa kufanya dispensing ya dawa like serious??
 
Sijui kama Ulichokiandika Umekisoma vizuri 🤣🤣🤣
Tuchukulie Mfano..
Mfano Mimi Ni Neonatologists
Nilifanya Neonatal fellowship Kwa Miaka Mitatu..
Baada ya Kupata MMED(Paed) degree ya Pili Au master Ya Miaka 3..

Kwahyo Fellow Huku Medicine tunairegard kama Degree ya tatu SO its equivalent na Phd Kama utakuwa Kwenye Track ya Proffesional ila Ulitoka kwenye proffesional Ndo unaweza ouchukua Degree ya Utawala ila ukibaki huku ndo unakuwa Super so Ma Super wote ni.Phd Holder..

Au Wanaitwa Wabobezi...

Mkuu, kwa maelezo yako haya, hakuna atakayepinga kwamba wewe siyo Daktari Mbobezi wa Watoto Njiti kwa sababu, uliofanya kwanza MMED (Paed) kisha Fellowship ya Neonatal.

Kwa Prof, hakuna mahali kwenye CV yake panaonyesha alifanya kwanza MMED (Internal Medicine) kabla ya kufanya Fellowship ya Moyo ili kuwa Daktari Mbobezi wa Moyo (Super Specialist) kama anavyotambulika. Na ndiyo Hoja ya mtoa mada.

Tujitahidi kumuelewa mtoa mada, kwa tija ya mjadala wetu na kunifanya jukwaa (JF) kuendelea kuwa kisima cha maarifa.

Naamini, wengi wataelewa ngazi/hatua za Taaluma ya Udaktari na baadhi yao kuhamasika kusoma Udaktari kwa namna moja ama nyingine.
 
Nimesoma mpaka mwisho bado sijaelewa mimi kilaza wa mambo ya afya.

Hoja ya mleta mada ingejibiwa kama mgemuhakikishia kuwa kuna uwezekano wa mtu kuwa daktari bingwa mbobezi wa moyo bila kuwa na hiyo Mmed anayolalamikia mleta mada kwamba Prof. Janabi hana.

Anadai kwamba kuna hatua ya MD, kisha hatua ya Mmed kisha ubingwa na ubobezi unafuatia. Je kuna njia ya kuruka Mmed ila ukawa cardiologist?
Kama inawezekana kule Marekani, Japan au hapa nchini mumsaidie mleta mada. Mmojawapo kagusia fellowship, je hii inaweza simama kama mbadala wa Mmed?

cc DR Mambo Jambo
Hapana Mkuu!
Janabi kafanya vyote..
Janabi kasoma MD, Mmed (Internal medicine Specified In tropical Medicine)

Kaja Akafanya Fellowship ya Cardiology Na akafanya reseaexh na study kibao mpaoa Kufikia Alipo We Jiulize Fellowship alifanya mwaka 2001 kama sijakosea sana Sasa Mpaka Leo study ngapi kafanya..

Mleta mada ana Chuki binafsi na Janabi nimewahi kueleza Humu kuhusu Janabi tangu mwaka jana
 
Mkuu, kwa kuwa unajitambulisha kwa Jina la Dr Mambo Jambo, naomba kuuliza swali kutokana na ulichoandika. Je, Fellowship ya Moyo peke yake, inatosha kumfanya Daktari yoyote kuwa DaktrBingwa wa Magonjwa ya Moyo?

Zaidi, unaweza kutueleza sifa za Kitaaluma za Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo?

Itapendeza kunipatia majibu ya maswali haya na kufanya huu mjadala kuwa na tija zaidi.
Fellowship Ya Moyo Ikiambatana na MMED ya Internal medicine..

Yes Inafaa Kumpa mtu Jina la Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Moyo..
 
Professor Janabi hana qualification yoyote ya kutibu moyo kibingwa, hana. Hakusomea popote na hakuwahi kutambuliwa na baraza la madaktari hapa Tanzania kama Daktari bingwa wa moyo. Na hata pale Muhimbili hajawahi kutibu moyo mtu kibingwa tangu awepo. Hana huo uwezo.
Mlikuwa wapi siku zote hizo anatibu watu mkijua kabisa siyo dkt wa moyo mbwa nyie?mkiambiwa hamna akili mnakataa!!
 
Hapana.
Kuna fellowship nyingi sana za miezi mpaka mwaka mmoja tu. Hutegemea professional, taasisi, na malengo. Hazina muda mahususi wa kufanana. Urefu wa muda wa mafunzo hauamui mafunzo kuitwa fellowship. Hakuna uhusiano wowote kati ya muda wa mafunzo na hayo mafunzo kuitwa fellowship.
Nitajie Fellowship Moja tu ambazo Inatolewa kwa Miezi au Mwaka mmoja..
Niko tayari Kujifunza..
Karibu
 
Ni ajabu sana anayehoji ubora wa elimu ya U.S ndio mtu ambayo nchi kuna kozi ilianzisha inaitwa ADDO kama sikosei nilishangaa eti mtu anasoma mwezi mmoja na anaruhusiwa kufanya dispensing ya dawa like serious??
Elimu Ya USA ni elimu Ambayo Iko Very practical Kuliko Yetu Nimekaa Kule..
Ukimaliza Zako MD haugusi Mgonjwa Bila Kufanya Residency angalau ya Miaka mitatu ambayo Huku Tunaita MMED..Au attending Dr.. yaani Ili upate Medical Licences lazima Ufanye Residency..

Elimu yao Ni Very practical Daktari aliyesomea USA yuko Vizuri Kuliko aliyesomea Tz
 
Mwisho kabisa, MCT wanatakiwa kutoa maelezo kwa umma, kwa hicho ulichowahi kusomea Professor Jababi (Masters of tropical health) ambacho hakina sifa yoyote ya udaktari bingwa wa moyo (maana mhitimu yoyote wa fani ya afya anaweza kusomea), kinampaje sifa mhusika kuwa daktari bingwa wa moyo?
Mimi siwezi kutetea upumbavu; lakini kwanza hebu twende taratibu?
1. Kwa nini umemhusisha na ubingwa wa magonjwa ya moyo? Kajitangaza hivyo yeye mwenyewe au vipi. Eleza hili kwanza limetoka wapi, halafu tutaendelea na mengine.
Katika nafasi hiyo ya WHO hawatafuti mtu mwenye sifa za ubingwa maalum wa matibabu.

2. Je, huyu ni daktari ( anayo shahada yoyote ya udactari); hata bila kuwa na huo "ubingwa wa moyo"?

3. Sita tetea chochote cha kuvunga vunga katika maswala ya elimu popote; kwa hiyo kama anadai kisicho kuwa halali, hiyo ni sababu ya moja kwa moja kumwondoa na kumdharau.

Hata hivyo, inaonyesha ujuha mkubwa sana kudhani kuwa Tanzania itakuwa na haki ya kupewa tena hiyo nafasi, kwa sababu ya yaliyo tokea. Huu ndio ujinga wenyewe. Tunapeleka uswahili wetu hadi kwenye maeneo yasiyo hitaji uswahili. Tunajiaibisha sana.

Lakini nilisikia akijisifu mwenyewe, kuwa alimfanyizia mtihani huyo marehemu aliye poteza uhai, na nadhani hata mke wake vile vile. Hilo pekee linaonyesha ulimbukeni.

hakuna anaye pinga mTanzania kujitosa tena kutafuta nafasi hiyo, lakini isitegemewe kuwa kutakuwepo na upendeleo maalum.
 
Back
Top Bottom