Ni kweli kwamba watumishi wasiopitishia mishahara yao benki ya CRDB hawana nafasi ya mikopo katika benki hiyo?

Ni kweli kwamba watumishi wasiopitishia mishahara yao benki ya CRDB hawana nafasi ya mikopo katika benki hiyo?

Ni wajibu wa CRDB Kuhakikisha hili suala kama lipo basi wachukue hatua za haraka na kulisitisha mapema iwezekanavyo ili kutokupoteza wateja,ulimwengu wa sasa sio wa kujibana ktk mazingira hayo utakosa wateja wengi sana kwa Tanzania ya sasa
 
Inasemekana wameishiwa na hela. Ndio maana leo wameanzisha promosheni watu wawekeze hela kwenye benki yao ili wapewe riba ya 9% kwa mwaka mpaka miaka 3. Ili ile hela ambayo watu watawekeza watu wakakopeshwe kwa riba ya juu zaidi (16%-13%).
 
Si kweli. Kachukue tu rafiki mpunga.
Siyo lazima mshahara upitie kwao.
Sijawahi ona benki ambayo chanzo kikuu cha marejesho ya mkopo ni mshahara alafu wakakubali kutoa mkopo ili hali mshahara wako uko benki A, alafu watarajie wewe ukichukiwa mshahara ndo upeleke marejesho kwao, kwa hela ipi? hii mishahara ya wafanyakazi wa TZ ambao kabla ya kupokea mshahara ulishatumika akilini na kukopa tena. Ni lazima mshahara upitie kwao wachukuwe cha kwao kwanza alafu kinachobaki ndo ukapambane na hali yako
 
Hio ni kwa ajili ya security issues,,, Huruma na Pesa ni vitu havijawai kwenda sambamba
 
CRDB wajinga sana kwanza mkopo wako unachukua muda mrefu sana utapitia hadi kwa mwanasheria...
CRDB ktk mkopo watakao kupa wanakata Processing Fee kubwa sana...
Mfano NMB wakikupa mkopo wa 1m basi watakata laki 1 wakat CRDB watakukata laki 2. Pia kama NMB watakupa laki9 basi CRDB watakupa laki7.8 japo makato ya kila mwezi yatafanana kwa wote ktk kipindi chote cha mkopo...
 
Hakuna bank itakupa mkopo kama mshahara haupiti kwao
Huelewi kitu,sijui kwa sekta binafsi ils kwa serikalini tunakopa tu,mm nilikopa CRDB na mshahra unapitia NMB,mwajiri wangu anawajibika kupeleka makato tu
 
CRDB wajinga sana kwanza mkopo wako unachukua muda mrefu sana utapitia hadi kwa mwanasheria...
CRDB ktk mkopo watakao kupa wanakata Processing Fee kubwa sana...
Mfano NMB wakikupa mkopo wa 1m basi watakata laki 1 wakat CRDB watakukata laki 2. Pia kama NMB watakupa laki9 basi CRDB watakupa laki7.8 japo makato ya kila mwezi yatafanana kwa wote ktk kipindi chote cha mkopo...
crdb insurance na processing fee wanakata hela nyingi sana aisee
 
Sio kweli nini sasa?!Benki gani hiyo ambayo inafanya hivyo? Kama unakopa kupitia mshahara lazima mshahara upitie benki husika.
mkuu CRDB wanafanya hivyo kwa sasa ni lazima mshahara wako upitie kwao. Nimeshuhudia watumishi wamejaza fomu na kusainisha Halmashauri na mwisho wa yote kipengele cha kuhamisha mshahara kinatibua mipango yote
 
Ndio ipo ivo nenda kwenye bank yako ya mshahara kama unataka Nbc unahisha mshahara wako...
 
Back
Top Bottom