Mbowe asitoke pale, manaccm yanataka kuvuruga chama. Angalia wanaopiga kelele wote ni CCM
Kwa sasa Chadema ni Chama kikubwa na kina watu makini sana hata Mbowe akistaafu na kuwa miaongoni ya Wajumbe wenye nafasi maalumu katika maamuzi ya kichama chama kina watu waliomwaga damu zao.
Wapo akina Heche , Lisu, Lema , ambao kwa hakika wanakijua Chama .
Mbowe anaweza akabaki kama mjumbe na mwanachama lakini asibaki kwenye uenyekiti.
Ni rahisi kuangalia chama kwa jicho la juu juu na kuona kuwa Mbowe anafaa mpaka Chama kiingie madarakani lakini Kuna hatari kubwa sana kwani chama kinaanza kuonekana kama mali ya mtu badala ya taasisi.
Hakuna Mweyekiti anayeweza kupata nafasi kwenye chama kikubwa kama Chadema halafu akiuze. Mrema alisalitiwa na wenzake ambao walijiona ni wasomi hawawezi kuongozwa na Mrema. Ilikua ni vita ya madaraka ndani ya Chama CCM hua wanakoleza tu vurugu lakini vurugu zinaanzia ndani ya Chama.
Wanasiasa wote wanafanana.
Kuna wanasiasa wanaharakati kama Lisu ,Mwabukusi ,Dr. Slaa n.k. Na kuna wanasiasa wanaopenda madaraka na kuwa na heshima popote wanapokuwa . Kuna wanasiasa wanawaza maslahi binafsi . Haya makundi yapo kwenye vyama vyote . Ukichunguza sana utaweza kunaini alipo Mbowe. Chama kinahitaji siasa tofauti na wakati wowote uliopita kutokana na makosa waliyoyafanya ya kupoteza uelekeo uliokuwa umekijengea heshima kubwa ya kupambana na Mafisadi . Wakati wa JPM chama kikaingilia vita vya mafisadi na magufuli ndani ya CCM na kujikuta wanawapa CCM nafasi ya kuitangaza Chadema kama Chama cha kupingapinga.
Awamu hii ndiyo awamu sahihi kabisa iliyoletwa na Mungu ili Chadema kiingie madarakani kuteleleza sera ya kupambana na mafisadi kwa sababu CCM ilipoteza nafasi ya kupambana na Mafisadi ikabaki kupambana na Demokrasia na vyama vya upinzani pamoja na mazuri aliyofanya Magufuli akajikuta anawapa mafisadi nafasi ya kupumua na kutengeneza njama zao dhidi ya watu waadilifu .
Mbowe anachotakiwa ni kuacha Demokrasia ifanye kazi kwa uwazi. Chadema ikiendelea kuingilia michakato ya kidemokrasia ndani ya chama kwa kisingizio cha kuwaita watu fulani kuwa ni wasaliti tutakuja kuzalisha taifa la ajabu sana.
Kauli ya Usaliti kwa wale wanaotofautiana kisiasa ni kauli mbaya na ya hatari sana. Chadema wanapaswa kuiacha haraka sana .
Kauli hiyo ilitolewa na JPM kama Kauli ya kusimamia misimamo yake dhidi ya mafisadi na wezi lakini ikapokekewa tofauti na watu ndani ya mifumo fulani na kujikuta inagharimu usalama wa Baadhi ya wanasiasa akiwemo Lisu.
Kauli ya usaliti imekua ikiwaumiza sana baadhi ya wanasiasa ndani ya Chadema na wengine kujikuta wanakosa hata marafiki kwa hofu ya kuitwa wasaliti . Sio kauli nzuri. Hata kusema kuwa kuwa hakuna mtu anayeweza kukiongoza kwa sasa chama Chenye wanachama zaidi ya milioni Nane wengi wakiwa vijana sio kauli ya kujenga. Ni kauli za watu wasio na dira. Haina tofauti na kauli ya CCM kuwa kwa sasa hakuna kama mama .
Chadema kinapaswa kuwaaminisha wananchi kuwa kwa sasa Chadema kuna watu wengi wenye uwezo wa kuongoza chama kwenda mbele zaidi na wajitokekeze kugombea nafasi mbali mbali ikiwemo uenyekiti. Hapo ndipo tunapoweza kuwaona wenye uchu wa madaraka na wenye kutumwa na CCM na mawakala wengine kwa sababu wataanza kukosa adabu na wengine kujionyesha wazi tabia zao na hapo wanachama wenyewe watawaaibisha kwa kuwanyima kura.
Demokrasia ya kweli kamwe haiwezi kuangusha Taasisi. Vyama hata CCM vinakwepa demokrasia kwa sababu ya kuweka mbele maslahi binafsi ya kakundi kadogo.
Hata Mbowe akigombea mara mia moja ni sawa mana suala la ukomo halimaanishi ndiyo demokrasia . La hasha . Demokrasia ni Uongozi unaotokana na watu kwa haki na uwazi . Pawe na demokrasia ya kweli na uchaguzi wa wazi na wa haki na kampeni ziwe wazi na midahalo ya wazi bila kuwatusha wengine au kuwapa majina mabaya ya usaliti ndani ya Chadema .
Neno usaliti linaweza likasababisha mtu akapigwa mawe na wananchi jambo ambalo ni hatari sana .