Ni kweli Mungu hana Upendo? Au sisi tu ndio hatumuelewi!?


Wewe achana na utoto wangu, hiyo ni sifa kubwa sana unanipa.

Jibu hoja, kama hauna majibu kaa kimya. Wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Wapi Yesu anasema "Mimi Mungu"?
 
Eiyer we mungu wako alishindwa kuwasamehe madhambi mpaka akaamua kujitoa roho yake mwenyewe..
Hakushindwa bali kwasababu Mungu wangu hajipingi wala habadiliki badiliki kimaamuzi aliamua kuziheshimu sheria zake alizoziweka kwani alisema kwamba hakuna dhambi ambayo haitaadhibiwa kwasababu kuadhibu ni kutoa stahiki na kutoadhibu ni kuvunja sheria yake mwenyewe

Pamoja na hilo,Mungu wangu alisema yeye ni hakimu wa haki na ni Mungu mwenye huruma,isingewezekana kufanya kimojawapo bila kutumia njia aliyoitumia

Kwasababu Mungu ni wa huruma na ni hakimu wa haki lakini pia aliahidi kila dhambi ataiadhibu na kwasababu ni hakimu wa haki na kwasababu alitupenda zaidi wanadamu aliamua aadhibiwe yeye kwa makosa yetu ili tuwe huru

Kama unataka maelezo mazuri kuhusu hili soma mada ...

Mungu wako ni hakimu wa haki na ni mungu mwenye huruma?
 
Wewe achana na utoto wangu, hiyo ni sifa kubwa sana unanipa.

Jibu hoja, kama hauna majibu kaa kimya. Wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Wapi Yesu anasema "Mimi Mungu"?

Nataka sana kukujibu lakini siwezi kujibu swali kama mlevi ...

Niambie,unataka nikujibu kwa kutumia ushahidi gani?
Huo ushahidi ambao unataka nikujibu unauamini kwamba haudanganyi?
 

Hii nchi ina binadamu wa ajabu sana ....

Huyu anauliza kitu ambacho kimejibiwa kwenye mada,haya matatizo yakutokusoma sijui yatakwisha lini kwenye hii nchi ....!!
 

Wewe unamjuwa Mungu? wewe unalijuwa sanamu la mzungu lililovishwa nepi unaloliabudu.

Hapo sasa.
 

Unapomjadili Mungu wangu tafadhali usiniandikie jina lake ukaanza na "m".

Ndio Mungu wangu ni Hakimu wa Haki Na Ni mwenye Rehema Na Huruma. Na hapo hapo ni Mkali kwa wenye Viburi na wafanya HARAMU.

Sasa leta maswali yako ya mtego.
 
Wewe unamjuwa Mungu? wewe unalijuwa sanamu la mzungu lililovishwa nepi unaloliabudu.

Hapo sasa.

Hakuna kitu cha ajabu sana duniani kama mtu anapoamua kuwa mjinga kwa hiyari yake mwenyewe

Kwanini unaniwekea maneno mdomoni?
Niulize mimi namjua Mungu ama simjui na huyo Mungu ninaemjua ni yupi na sio kujilisha ujinga tu!
 
Unapomjadili Mungu wangu tafadhali usiniandikie jina lake ukaanza na "m".

Ndio Mungu wangu ni Hakimu wa Haki Na Ni mwenye Rehema Na Huruma.

Sasa leta maswali yako ya mtego.
Haki maana yake nini kwa mtazamo wako?
Huruma ni nini kwa mtazamo wako?

Nataka nikuulize swali kutokana na maoni yako wewe kuhusu yote hayo mawili ndio maana nimekuuliza hayo maswali,hivyo basi nijibu ili nikuulize swali!
 
Hakuna kitu cha ajabu sana duniani kama mtu anapoamua kuwa mjinga kwa hiyari yake mwenyewe

Kwanini unaniwekea maneno mdomoni?
Niulize mimi namjua Mungu ama simjui na huyo Mungu ninaemjua ni yupi na sio kujilisha ujinga tu!

Huyu mzungu mnaemuabudu mlio mvisha nepi vipi?

 
natamani nicomment hii mada ila mmh sijaisoma maana ni ndefu sana, atayeweza kufupisha anisaidie maana huu uwezo wa kusoma mada ndefu nahifadhi kwa kusoma bible tu
 
Wewe achana na utoto wangu, hiyo ni sifa kubwa sana unanipa.

Jibu hoja, kama hauna majibu kaa kimya. Wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Wapi Yesu anasema "Mimi Mungu"?

Revelation 21:7
 
Eiyer ubarikiwe sana mkuu,binafsi nimekusoma na kupata mambo mazuri mengi hapo,na hasa hapo mwisho jinsi Mungu alivyosolve equation ya kumuokoa binadamu bila kutangua adhabu bali kuitimiliza kwa kumtumia Yesu,na ndio maana siku ya kiama wale wasiokubali dhabihu ya mwana wa Adamu (kwa makusudi) wataibeba adhabu wenyewe.Nimekupata uzuri sana,pamenigusa hapo mno.Nina jambo moja la kuuliza humu wana jf tujadili.Hivi wana jf,tunaelewa nini tunaposikia maneno haya matatu:wema,uovu na haki?
 
Last edited by a moderator:

Ngoja nikupe somo la bure hapa

Umedai kwamba hayo maneno uliyowekewa na mtumishi ISHAMel sio maneno ya Yesu au kwa lugha nyingine hapo hakuzungumzwa Yesu,ngoja tuone maandiko yanasema nini kuhusu Yesu na kuhusu kuwa Alfa na Omega

Ufunuo 1:7
7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.


Kwenye huo mstari tunaona Yohana anasema kwamba kuna atakaekuja na kila jicho litamuona na wote waliomchoma na kabila zote za dunia zitaomboleza kwaajili yake

Kwa lugha rahisi kabisa inaeleweka ni nani atakaekuja kwenye mawingi na inaeleweka ni nani aliechomwa,huyu sio mwingine bali ni Yesu Kristo [Danieli 9:26 kwa ushahidi na hii hapa chini kwa uthibitisho zaidi

Mathayo 24:30
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.


Huo ushahidi unaonesha kabisa huyo anaesemwa kwenye Ufunuo hapo juu ni Yesu Kristo,sasa fungua moyo wako kupata ushahidi utakaoitikisa ngome ya imani yako na kuisambaratisha kwa kishindo cha ukuu wa Mungu mkuu

Ufunuo 1:8
8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.


Maneno hayo yanaonesha huyo anaezungumza anasema kuna wakati atakuja,sote tunajua kabisa kwamba atakaekuja sio Miwingine ila ni Yesu Kristo,hili ni wazi kwasababu maandoko yameyuthibitishia kwamba Yesu ndie atakaekuja kama hayo maandiko hapo juu yanavyotuonesha,kwa mujibu wa maandiko ni kwamba atakaekuja ni Yesu Kristo siku hiyo ya mwisho pamoja na Jeshi kuu la mbinguni na sio Mungu baba

Ufunuo 19:11-13
11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.


Maandiko hayo hapo juu yanatuyonesha kwamba huyo ambae atakuja ni neno la Mungu,ngoja tuitazame Biblia inasema neno la Mungu ni nani

Yohana 1:8
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.


Sote tunajua kwamba aliefanyika mwili ambae ni neno ni Yesu Kristo hivyo hili linaendelea kuthibitisha kwamba ni yule ambae alisemwa kwenye Ufunuo 1 kwamba ni Alfa na Omega

Ufunuo 1:17-18
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Sasa hapo tunaona maneno kutoka kwenye kinywa cha mhusika mwenyewe ambae anasema ni wa kwanza na wa mwisho sawasawa na Alfa na Omega,lakini anaendelea kusema kwamba alikuwa amekufa na sasa yu hai,hakuna yoyote ambae alikuwa amekufa na akawa hai tofauti na Yesu Kristo

Dada yangu Faiza,huna namna ya kukataa haya na yapo wazi kabisa kwa mba Yesu ni Alfa na Omega na ni Mungu mwenyewe [Ufunuo 1:7]

Glory to God Faiza ......

Karibu kwenye furaha ya kweli kwa Yesu Kristo Mungu mkuu aliekuumba wewe,Kahtaan na mimi na wote pia!
 
Last edited by a moderator:
Haki maana yake nini kwa mtazamo wako?
Huruma ni nini kwa mtazamo wako?

Nataka nikuulize swali kutokana na maoni yako wewe kuhusu yote hayo mawili ndio maana nimekuuliza hayo maswali,hivyo basi nijibu ili nikuulize swali!

Sasa we unauliza vitu ambavyo hata maana yake Hujui?
Au unataka kurefusha uzi kwa maswali ya kitoto?
We mtu mzima unauliza nini maana ya haki?
 
Sasa we unauliza vitu ambavyo hata maana yake Hujui?
Au unataka kurefusha uzi kwa maswali ya kitoto?
We mtu mzima unauliza nini maana ya haki?

Mkuu maneno mengi ya nini?

Nimekuambia kwamba nataka nikuulize maswali kutoka kwenye maoni au mtazamo wako kuhusu maana ya hayo maneno,sasa kipi huelewi hapo?

Mbona kama una hofu na jibu lako mkuu?
 

Mkuu roho mtakatifu ni mkuu sana anapotufungulia vifungo ambavyo vimetesa wengi sana miaka na miaka ...

Hili ni jambo ambalo limewasumbua wengi na wengi hawalielewi vizuri na ndio maana kuna mikanganyiko sana

Tumpe sifa Yesu Kristo alietupa roho wake kuja kutufumbulia maneno makuu ya Mungu

Kuhusu hayo maneno matatu mkuu yanahitaji tafakuri ndefu ili kuweza kuyaelewa vizuri na sio kukurupuka tu,tunahitaji tutafakari na kumshirikisha Roho Mtakatifu ili tuweze kuyaelewa vyema zaidi ya sasa mkuu

Mkuu nakuomba umwage elimu yako hapa kuhusu hayo namna unavyoyaelewa ili tujifunze pamoja

Tubarikiwe sote kiongozi!
 
Dini ya kweli ni Islamic tu nyingine ni biashara.

Umeingia choo cha kike kijana ....

Hapa hatuhubiri kuhusu dini tunajadili mambo makubwa ya Mungu mkuu aliyoyafanya kwa wanadamu pamoja na kujibu madai ya watu ambao wanadai Mungu anajikinza ....

Kama una cha kuongeza au kuuliza unaweza kuuliza,lakini zingatia kiwe ndani ya mada tafadhali ....

Karibu ....!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…