Ni kweli Mungu hana Upendo? Au sisi tu ndio hatumuelewi!?

Ni kweli Mungu hana Upendo? Au sisi tu ndio hatumuelewi!?

Dreadnought

Eiyer ameshindwa kabisa kujibu hoja zako mkuu. Sina swali maana umeuliza kila swali nililotaka kuuliza na ameshindwa kabisa kujibu zaidi ya kukuona mkorofi huku akitafuta njia ya kukimbilia!!

Afadhali umeliona hilo, tena nimejaribu kuchambua mada yake ndefu na kuchukua sehemu chache ambazo zina utata, lakini naona ameamua kupuuzia na kusema mara namchosha n.k
 
Kabla ya kwenda huko unakokutaka ni kwamba hayo yote hapo yaliyokushangaza ni kwasababu Mungu wangu anaweza yote na mungu unaemjua wewe hawezi kuwa binadamu

Baada ya hayo nakuja kwenye swali lako;

Unataka nikupe jibu kwa kutumia ushahidi gani?
Je,huo ushahidi unauamini kwamba ni kweli?

Mbona mungu wako namba 2 alishindwa kujifufuwa? msome Paulo anasemaje hapa:

1 Wakorintho 15:14
Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

Paulo anasema kinaga ubaga kuwa "tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo", vipi Mungu wako uliyemweka namba 2 hapo juu kidogo unaedai kuwa "anaweza yote" mbona hakujifufua?
 
Mbona mungu wako namba alishindwa kujifufuwa? msome Paulo anasemaje hapa:

1 Wakorintho 15:14
Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

Paulo anasema kinaga ubaga kuwa "tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo", vipi Mungu wako uliyemweka namba 2 hapo juu kidogo unaedai kuwa "anaweza yote" mbona hakujifufua?

Haya maswli hapa hujayaona au unajidai huoni?
Unataka nikupe jibu kwa kutumia ushahidi gani?
Je,huo ushahidi unauamini kwamba ni kweli?

Nilikuuliza kwanza,kabla hatujafika huko nijibu hayo maswali kwanza kisha tutaendelea

Acha longo longo ...!!
 
Ishmael

Sawa ila kumbuka kuwa Adam ndiye aliyefanya hilo agano na Mungu hukufanya wewe au Mdogo wa au mwanao au Babu yako, Sasa suala la adhabu yao wewe linakuhusu nini? Ulikuwa na Adam siku ya hilo agano? Je huwa huwazi kama ingekuwaje kama wewe ungekuwa ndo adam na ungekataa kula tunda? Unahisi ni haki kwa Kosa alilofanya babu wa babu wa babu wa mababu lije likulize wewe na kukutoa machozi tena Msimamizi wa hiyo kesi Tukimuita ndiye mfalme wa Amani!!!! Amani iko wapi?

Je wewe ungekuwa ni baba mwenye busara ungeweza kumuachia Chizi amlee mwanao sababu jana mwanao alikukosea kwa kukuibia peni ndani ya nyumba? hivyo ndivyo Mungu alivyotuacha na Sisi na shetani....!!!! Upendo uko wapi hapa? Kwa dhiki, shida njaa na vifo.?



Mafundisho yanasema kwamba dhambi ya Adam imesababisha sio tu sisi kuwa na asili ya dhambi, lakini pia kuingia katika madeni ya hatia yetu mbele ya Mungu ambayo sisi tunastahili adhabu. Kuwa mimba na dhambi ya asili juu yetu (Zaburi 51:5) matokeo yake sisi tumerithi iliyo ovu sana, ambayo Yeremia 17:9 inaeleza moyo wa binadamu kuwa "ni mdanganyifu kuliko vitu vyote na zaidi ya tiba." Siyo eit Adam alipatikana na hatia tu pekee kwa sababu yeye alikua amefanya dhambi, bali hatia yake na adhabu yake ni (kifo) tunayostahili pia (Warumi 5:12, 19).

Kuna mitazamo miwili ni kwa nini hatia ya Adam inapaswa kuonekana na Mungu vile pia inafaa kwetu.

1. maoni ya kwanza yanasema kwamba binadamu alikuwa ndani ya Adamu katika hali ya mbegu; hivyo Adamu alipofanya dhambi, sisi tulifanya dhambi katika yeye. Hii ni sawa na mafundisho ya kibiblia kwamba Lawi (kizazi cha Ibrahimu) alitoa sehemu ya kumi Melkizedeki katika Ibrahimu (Mwanzo 14:20; Waebrania 7:4-9), ingawa Lawi hakuwa amezaliwa hadi baada ya mamia ya miaka.

2. Mtazamo mwingine mkuu ni kwamba Adam aliwahi kuwa mwakilishi wetu na hivyo, wakati alifanya dhambi, sisi tulipatikan na hatia pia.
 
Warumi1:
22 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. 23 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
24 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.

25 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
26 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.

27 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.

Soma vizuri kwa utuvu utajuwa yaliotajwa hapo yanapatikana wapi.
Anzia kusoma aya ya kwanza ndio utalewa nini kinasemwa hapo.
 
Kwa nini nisitumie immanent critique kama itanifikisha katika ukweli?

Hata katika kusolve mathematical equations kuna "Let a = b".

Nikianza uchunguzi wangu kuhusu kuwapo kwa mungu kwa kusema.

"Let "god exists" = true"
"Let "god is all powerful"= true"
"Let "god is all loving" = true"
"Let "god is all capable" = true
"Let "god created the universe" = true"


Then why this all loving, all powerful and all capable hodhead create a universe in which evil is possible while he could have created one in which evil is not possible?

Tunaanza na huyo mungu wa kwenye biblia (na quran na dini nyingine nyingi by the way) mwenye sifa hizo kwanza.

Unakubali kwamba huyu mungu ni wa maboksi?

Ukiahakubali hilo tutaenda huko kwingine, lakini kubali hili kwanza. Kwamba huyo mungu wa biblia uliyemtaja ni wa maboksi.

Halafu utasemaje immanent critique haikubaliani na dhana ya kutokuwepo kwa mungu bali kinyume chake wakati dhana yoyote, ikiwemo ya kuwepo kwa mungu yeyote, inaweza kupigwa immanent critique.

Wewe kweli unaelewa immanent critique ni nini au una parrot ninachoandika hapa tu?

LET is assumption.

Jaribu tena God Hater.
 
Yesu alifanya nini na siku ya tatu akafufuka kutoka kwa wafu waliokufa? soma Mhubiri 9:5,6,10 ujue mtu anapokufa huwa inakuwajee au Zaburi 146:4.. Mtu akifa amekufa yaani ni kama tv iliyozima haisikii wala kuhisi kitu roho za watu zingekuwa huwa zinaenda mahari basi tungeambiwa siku ya mwisho mungu ataenda mahari roho zilipo na kuzivisha miili tena ila unaambiwa siku ya mwisho makaburi yatafunguka na waliokuwa wafu watapata tena kuwa hai, Maana roho zilikuwa palepale Makaburini zimelala ila zitaamshwa.

Mtu akifa, mwili unazikwa makaburini(utaratibu mzuri wa kibinadamu kutunza mazingira, kwa kuwa uzipozikwa ukaoza utatoa harufu na nchi/mji/mtaa/kijiji pakakuwa hapakaliki, hivyo njia salama ya usafi ni kuufukia ardhini). Ndio maana Biblia katika kitabu cha Mwanzo inasema, "Uu mavumbi wewe na mavumbini utarudi", anayeambiwa hapo sio roho bali ni mwili. Mwili unatokana na udongo(kwa kiebrania na tafsiri ya kingereza wanasema, "humarusman" yaani "udongo" bali roho ikitoka ndani ya mwili ama inaenda Paradiso,(mahali katika ulimwengu wa roho ambapo watakatifu wanasubiria parapanda, hukumu ili wapelekwe mbinguni) au wanapelekwa kuzimu (sehemu katika ulimwengu wa roho ambayo wasiowatatifu/wadhambi hupelekwa kusubiria parapanda/hukumu ili watupwe(roho zao) katika ziwa liwakalo moto) Hapa ukumbuke pia kuwa kuzimu nayo itatupwa motoni. Pia mauti/kifo ambayo nayo ni roho kamili zitatupwa zote katika ziwa liwakalo moto kwa mujibu wa Biblia. Hili nalo ni somo la siku nyingine kuhusu kifo, kifo sio tukio kifo ni roho kamili/mauti ni roho kamili inayotenda kazi, inaweza kumwingia mtu na kuutoa uhai wake nje.

Utajuaje kuwa mtu ni roho? Soma Luka 16:19 ambapo YESU anaelezea, kumbuka hapo hakuwa anasema mfano la hasha alikuwa akizungumzia habari ya jambo lililotokea, akaanza kwa kusema " Palikuwa na mtu mmoja tajiri, aliyevaa nguo za zambarau na kitani safi, na masikini mmoja jina lake Lazaro ambaye alikuwa akisubiri kujishibisha kwa makombo kutoka katika meza ya jule tajiri" Biblia inaendelea kwa kusema, "Ikawa yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani mwa Ibrahimu, yule tajiri naye akafa, akazikwa, kule kuzimu akayainua macho yake.........." inaendelea hapo. Sasa swali la kujiuliza ni kuwa kama tajiri alikufa, akazikwa, na alionekana kuzimu akiyainua macho yake sasa aliyekufa ni nani na aliyekuzimu ni nani? Jibu ni rahisi kuwa aliyekufa sio tajiri aliyekufa ni mwili wa Tajiri na tajiri mwenyewe ambaye ni roho amekwenda kuzimu, na upande mwingine ni kuwa yule masikini Lazaro yeye mwili wake ulizikwa ndio, ila roho yake ipo Paradiso kule alikopelekwa na malaika mpaka kifuani mwa baba Ibrahimu.(Kumbuka huyu Ibrahimu ndio baba wa imani, ibrahimu baba wa wayahudi wote (christians) na baba wa waarabu wote (Muslims). Ambaye kimsingi naye yupo paradiso, akisubiria kuingia katika mji mpya wa Jerusalemu, mji utakaoshuka toka mbinguni.

Nimalizie kwa kusema hivi, mbingu ipo, roho ikitoka mwilini ndio tunasema umekufa.Na roho yako inautambuzi inaweza kutambua kila kitu kwa kuwa imeambatana na nafsi (mind) ama wengine hupenda kuiita soul. Soul na spirit ni vitu viwili tofauti. Soul(nafsi), Spirit(roho) flesh (mwili). Kikubwa zaidi ni kuhakikisha kuwa unaacha dhambi,unampokea YESU kuwa Bwana na Mokozi wa maisha yako(roho) ili roho yako ambayo ndio wewe ikitoka katika mwili iende paradiso mahali salama na sio kuzima, kwa shetani na malaika zake. Kumpa Yesu maisha ni rahisi, ukiamini kwa moyo na ukakiri kwa kinywa kuwa Yesu alikufa,na siku ya tatu akafufuka, ukatubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, utakuwa umeokoka. Tafuta kanisa linalohubiri habari njema za wokovu, sikiliza neno la Mungu, lielewe, amini ndani ya moyo wako na ukiri kwa kinywa.
 
Duh! umenchanganya hapo na hapo ndiyo kuzingumkuti kinapoanzia. Yaani huyo wa juu ni Mungu namba moja kama ulivyoweka na huyo wa chini ni Mungu namba mbili kama ulivyoweka?

Wapi Yesu anasema "Mimi Mungu" niabuduni?
Yesu anakujibu hapa:

Revelation 21: 6-7.

SASA NA WEWE NIONYESHE WAPI ALLAH KASEMA MIMI ALLAH NI MUNGU NA WAPI MUHAMMAD KASEMA MIMI MUHAMMAD NI MTUME WA MUNGU.

NOTE: Sitaki aya ambayo mtu anamsemea Allah kuwa yeye ni Mungu, nataka Allah mwenye aseme kuwa MIMI ALLAH NI MUNGU

Hivyohivyo, NATAKA Muhammad aseme kwa Mdomo wake mwenyewe kuwa MIMI MUHAMMAD NI MTUME WA MUNGU.

Upo kwenye Msiba dada.

USIKIMBIE WEYE
 
Yesu anakujibu hapa:

Revelation 21: 6-7.

SASA NA WEWE NIONYESHE WAPI ALLAH KASEMA MIMI ALLAH NI MUNGU NA WAPI MUHAMMAD KASEMA MIMI MUHAMMAD NI MTUME WA MUNGU.

NOTE: Sitaki aya ambayo mtu anamsemea Allah kuwa yeye ni Mungu, nataka Allah mwenye aseme kuwa MIMI ALLAH NI MUNGU

Hivyohivyo, NATAKA Muhammad aseme kwa Mdomo wake mwenyewe kuwa MIMI MUHAMMAD NI MTUME WA MUNGU.

Upo kwenye Msiba dada.

USIKIMBIE WEYE

Mbona umeweka namba tu hukuweka hiyo aya? unacheza na namba? Unanshangaza, weka aya tukupe darsa. Hatutaki manamba yako. Weka aya Yesu anasema "Mimi Mungu" niabuduni, wacha porojo.
 
Anzia kusoma aya ya kwanza ndio utalewa nini kinasemwa hapo.

Wacha porojo, wewe weka kuanzia huo mwanzo, hapo umeelewa na nimekuuliza swali hujalijibu, rudia kusoma ujibu swali.
 
Mbona umeweka namba tu hukuweka hiyo aya? unacheza na namba? Unanshangaza, weka aya tukupe darsa. Hatutaki manamba yako. Weka aya Yesu anasema "Mimi Mungu" niabuduni, wacha porojo.
Teyari umesha pata ile juisi ya pilipili. Si nilikwambia kuwa "USIKIMBIE WEYE" Unaona jinsi nilivyo tabiri zaidi ya Marehemu Shehe Yahaya

SASA NA WEWE NIONYESHE WAPI ALLAH KASEMA MIMI ALLAH NI MUNGU NA WAPI MUHAMMAD KASEMA MIMI MUHAMMAD NI MTUME WA MUNGU.

NOTE: Sitaki aya ambayo mtu anamsemea Allah kuwa yeye ni Mungu, nataka Allah mwenye aseme kuwa MIMI ALLAH NI MUNGU

Hivyohivyo, NATAKA Muhammad aseme kwa Mdomo wake mwenyewe kuwa MIMI MUHAMMAD NI MTUME WA MUNGU.

Upo kwenye Msiba dada.

USIKIMBIE WEYE
 
kahtaan

Kama unamaanisha Yesu, basi Yesu alikuwa asilimia 100 binadamu, asilimia 100 Mungu...

Sasa huyo ndiye Yesu sasa, hata kwenye hesabu zako amekataa...

1; Mungu ninaemzungumzia hapa ni Ehyeh Asher Ehyeh
2; Yesu ni Mungu!

Summun bukmun mwenyewe...

Unaona jinsi ilivyo rahisi kummaliza Allah na watoto wake.

Usiogope kusoma, wewe anzia aya ya 1 na tuambie nini hasa kinasemwa hapo?

MwenyeziMungu ameshasema Ktk
Quraan Al anaam 6:111

وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ

NA LAU kuwa tungeli wateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeli amini, ila Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wamo ujingani.

Nyie subiri Moto Wa Jahannamu tu.

Manake nyie Quraan imeshawaita.

صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ

Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.

Albaqara 2:18.

Swadakallahu laadhim
 
Last edited by a moderator:
Exhibit:

YESU KRISTO MUNGU MKUU, ( 1TITO 2:13 )

Mgalatia Ishmael tazama sifa za Mungu na Sifa Za yesu uone tofauti.
Na sisi tutatumia andiko lenu hilo hilo mpaka muache Ukafiri.

Yakobo 1:13). Mungu hajaribiwi na Shetani.

-(Mat 4:1). Lakini Yesu alijaribiwa na Iblisi.

(Isaya 40:28).Mungu hachoki.

(Yoh. 4:6)Lakini Yesu-alichoka


(Ezekiel 28:8-9).Mungu hauwawi


(Matendo 5:30)Lakini Yesu aliuwawa

Mungu hafi (Daniel 6:26).

Lakini Yesu alikufa (Mat. 27:50)



(1Wafalme 8:39)Mungu anajua kila kitu.

Lakini Yesu hakujua kila kitu (mti wa mtini).(Mat. 21:18-19)-

Ilhali haukuwa msimu wa matunda-(Marko 11:13)

Mungu hali, lakini Yesu aliona njaa na akala.(Marko 11:12; Luka 11:37-38, 24:42-43)

(Zaburi 121:3-4).Mungu hasinzii.-
Lakini Yesu alilala fofofo.(Marko 4:37-38; Mat. 8:23-25)

Na Mungu Hatairiwi lkn Yesu alitahiriwa.

Yaani msipotuelewa Sisi nyie jiandaeni na Moto wa jahannamu tu.
 
Last edited by a moderator:
MwenyeziMungu ameshasema Ktk
Quraan Al anaam 6:111

وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ

NA LAU kuwa tungeli wateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeli amini, ila Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wamo ujingani.

Nyie subiri Moto Wa Jahannamu tu.

Manake nyie Quraan imeshawaita.

صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ

Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.

Albaqara 2:18.

Swadakallahu laadhim

Hapa tunamzungumzia Mungu wa kwenye Biblia na sio huyo wa kwenye Quran,Mungu wa kwenye biblia ni tofauti na wa kwenye Quran,tafadhali fuata masharti ya mjadala .....

Huyo mungu wa kwenye Quran mnamjua nyie tu na mnaweza kuanzisha mjadala unaomhusu!
 
Back
Top Bottom