Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
MKUU
Historia inawahukumu Sana weupe dhidi ya weusi!!
Kabla ya kuniita mbaguzi ibadili historia ya Dunia kwanza!
Hata Sasa kinachoendelea kule ngoro ngoro na lolliondo ni historia kujirudia ile ya Mwanzo Kuwa weupe ni superior KWA weusi!!!
Unashangaa nini kama mweusi akikosa imani na weupe!!?
Kama vitabu vyenyewe vinafundisha chuki hiyo Hadi kwenye imani ZETU zenyewe ubaguzi upo wa wazi kabisa unafikiri wangapi watapona na hilo unaloliita chuki!!?
Ni kana kwamba waasisi wa imani ZETU WOTE Wana ueupe hakuna weusi lengo la kuandika hayo yote ni nini kama sio ubaguzi wa wazi!!?
Tangu mtu anazaliwa Hadi anazeeka anafundishwa ueupe ni maridadi kuliko weusi na matendo ya kidunia yanasadifu hivyo Sasa unataka huo upendo unaodhani wa weusi KWA weupe ushamiri kivipi LABDA!!?
Yaani tulazimishwe kupitia imani upendo KWA wanaotutesa sio!!?hivi ingekuwa vice versa ungehubiri HAYO!!?
Ngoja Tuone hatma!!
Nakubaliana na wewe yote uliyoyaandika sasa ingawa mwanzo uliamza na tuhuma kuwa mimi ni mwarabu HAPANA
Ubaguzi wanatufanyia sana ila mimi huwa siwezi kujiweka chini kwao na ninawaona wa kawaida tu kama Sisi
Najuana na wengi wenye pesa ndefu ila siwezi hata siku moja kuwanyenyekea wala kuwahitaji
Ukiwapa nafasi ya wao kujiona Superior hapo ndio tatizo linaanza
Akileta ubaguzi mpe za uso ila ukijishusha atakuona dhalili tu
Tusiwape nafasi hiyo ila na sisi tusiwe na chuki kisa walitutawala na kuuza babu zetu kama njugu
Hata Babu zetu wengine walihusika katika biashara hiyo
Niwie radhi sana kwa ukali wa maneno mwanzo
Ubaguzi umepungua sana miaka hii na duniani upo ila sio hivyo kama zamani
Watu wanabaguana kwa Koo na koo
Kabila kwa Kabila na Rangi pia
Ubaguzi hautaisha ila tuukemee kwa nguvu zote na tuwafundishe watoto wetu kwani Hakuna anaezaliwa na ubaguzi
Hao hao tulisoma nao na kucheza nao ila wanakuja kukatazwa baadae kuwa na sisi na wengine huvunja hiyo chain na kuamua kuoa kabisa
Usikasirike haya mambo yapo tupambane tu na hali yetu na kujielewa na kujitegemea