Ni lini Amiri Jeshi Mkuu atavaa sare za Askari Polisi au Magereza?

Umesema vyema. Lakini pia, wanapata wapi hii dhana ya uwakilishi kwenye combat dress?
Huwa kuna kikosi cha ujangiri kwenye mapori ya uhifadhi wanaitwa Game. Ni military forces wanakuwa trained mafunzo ya kijeshi kama nyongeza wanasoma zaidi ikolojia na uhifadhi.
 
Hata ningekuwa mimi ndiye Rais wa jamhuri nisingevaa sare zisizo na hadhi
 
Hebu leta hapa kama una nukuu au screen shot au short video...

Sidhani kama kuna uwezekano, tena wa Coloneal kusema vitu kama hivyo.. Sijawai kuona wala kusikia
 
Ni kweli maana gwanda hutisha wabadhirifu, wahalifu na mafisadi. Hao watanzania unaotaja ni kina nani? Maana unajumuisha wote kuwa wanatishika, kweli? Acheni uhuni jamaa kawakamata. Nyerere mwenyewe unayemnukuu kavaa magwanda sana.
Wabadhilifu gani mjomba?au hujasikia mabilioni yaliyopigwa kwenye korosho pamoja na kwamba jeshi lilisimamia zoezi?mafisadi unaowazungumzia ni hawa hawa wanaolipa vipande vya pesa na kuachiwa waendelee na maisha yao au kuna wengine?
 
Avae haya haya anayo yapenda lakini asiishie kuvaa tu afanye na kazi wafanyazo hao wanajeshi, sasa hivi kule Goma mauaji yamezidi ingependeza akaenda huko kujiunga na jeshi la umoja wa mataifa kutokomeza waasi wa ADF..
Kuna makamanda zaidi ya milioni rais akafanyeje?
Kama sisi tukileta umwambafy Congo,Rwanda,Burundi,Uganda na hata Kenya wanakaa chini.
Sema hatuko hivyo tunaogopa kugeuziwa kibao na wahisani
 
Kuna kitu naona watu wanaomkubali sana Rais hawaelewi,jamani hakuna kitu kisichokuwa na utaratibu hata kama wewe ni rais,hawa watu wanadhani ukiwa rais basi unaweza kujiamulia kufanya chochote unachojisikia/kitakachokujia akilini na kusiwe na shida kwakuwa wewe ni rais sidhani kama hii ni sawa,hao wanajeshi wenyewe wana utaratibu wa jinsi ya kuvaa hayo magwanda.kama uliwahi kumuona IGP Siro akikemea askari wake wanaovaa combat ndivyo sivyo au katika muktadha usiohusika.wanaoelewa utaratibu huwa wanavaa kutokana na mazingira au tukio linaloendana na uhusika lakini sio ukiamka tu ukijisikia kuvaa basi unavaa ingawa hauzuiwi na mtu kuvaa na ndio maana wanaojua utaratibu wanajizuia kuvaa tu bila sababu.
 
Umeandika wakati umezimia au?,kwahiyo hata inchi nyengine wakivaa hayo magwanda wanawakilsha,jkt,magereza na polisi?
 
Jeiwii linawakilisha majeshi yote na wewe...

Tanapa kijani
zimamoto nyekundu
magereza ugoro
polisi kaki
uhamiaji nyeusi

Kama unaziona hizo rangi kwenye gwanda ya JWTZ basi ujue ndio maana yake
umemaliza
 
kombati za jeshi linawakirisha majeshi yote kwenye kombati ile kuna blue ambayo ni uhamiaji kijani polisi nyekundu zimamoto ugoro magereza over
 
Producer aliyesababisha wimbo wa UNO wa Harmonize kufutwa YouTube, Atoa onyo kali kwa wasanii wanao-copy kazi zake
 
Jaman yy c ndo mtukufu sana wa majeshi yote au umeghafilika?
 
Magufuli kavunja katiba left, right and center.

Kavunja staha za urais left,right and center kwa maneno ma matendo.

Na bado wapiga zumari wake wanamtetea.

Walioamua kumtetea hata akifanya nini watatafuta sababu ya kumtetea.

Wanaopima mambo kwenye mizani washajua siku nyingi huyu hamnazo hafai kuwa rais.
 
Aiseee hebu punguza ukal kidogo kashasema yy hajaribiw
 
huyu ni mkuu wa Majeshi mwenye amri ya juu sio mkuu wa jeshi kama la polisi
 
Nimeona nitoe ushauri tu ili kuweka usawa kati ya majeshi.

Nashauri kwamba, Rais aweke zamu ya kuvaa nguo za majeshi yote, kama ni jeshi la polisi anaweza kuamua kuvaa zile za khaki, au za FFU au za trafiki.

Pia anaweza akapanga kuvaa nguo za askari magereza na safari nyingine akavaa za uhamiaji.

Hii itafanya majeshi yote yajisikie yako sawa
 
Akivaa zile za traffic mtasema Rais anadhalilisha hadhi yake

Watanzania hamna jema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…