Kwa upande wangu sina mke kwa sasa, lakini nina mpenzi, nampenda sana, ila huwa ananichekeshaga sana.
1. Ana hasira za karibu(Plus ukorofi)
-kipindi ambacho anakujaga kuishi kwangu huwa anafanya vitu vinanikera sana hadi sometimes nachekaga tuu, ana sura ya kitoto, sauti ya kitoto, ni mfupi, yaan basically ni mtoto ndo maana hata akinikera nashindwa hata cha kumfanya mwishowe nacheka tuu.
-huwaga mara nyingi nachelewaga kurudi, sasa yeye hataki nichelewe kurudi, hataki kabisaaa, na ukimwambia nilikuwa sehemu flani hataki, yeye anachojua mm nilikuwa na wanawake wengine, hii inampelekea kufoka, kununa(sunajua zile morning drama, yaan asubuhi anawasha generator, halizimiki hata useme nn) pamoja na kushtaki kwa mama angu, sasa kuna siku hio sitoisahau, tulikuwa tunabishana akanimwagia maji usoni, aisee nilikasirika vibaya mno, aligundua nimekasirika akaanza kujiliiza, ugomvi wenyew ulikuwa ni wa kijinga sana, huwaga anafanya mambo kwa hasira alaf badae anaanza kujuta.
2. Anapenda kulia
-Baada ya kukukera, ukianza kuja juu analia, atalia hapo nusu saa nzima, Kitu kidogo tuu analia, na akianza kulia atakukumbushia mambo uliyomfanyia miezi sita iliyopita, na analia kokote hachagui sehemu ya kulia, barabarani, kweny mgahawa, kanisani etc
-Kuna siku tulikuwa kweny mkusanyiko wa watu akaanza kulia hadi watu wakawa wanatuangalia, na ukimbembelea ndo unachochea.
-Yaan ukimkosea analia na akikukosea wewe bado analia yeye, hadi leo bado sijaelewa hio kitu ikoje.
3. Anaongea sana
-Ila sikuiz nishamzoea, akianza kuongea naweka simu chini naanza kumsikiliza, anapenda sana kuniadisia mambo yake, na akianza kuadisia hamalizi, huwa sometimes hadi nasinzia, utakuta ananishtua anasema "mbona unalala au nakuboa?" sasa ole wako useme "Ndio", utazalisha kesi nyingine na mwisho wake ni vilio.
Mazuri yake;
-Anapatana sana na mama yangu.
-Ananipaga ushauri mzuri.
-Ni msafi.
-Pamoja na kuwa mkorofi anajua wapi amekosea na anaomba msamaha
-Ana maisha yake, hapendi kuiga watu.
-Anajiheshimu sana, havai nusu uchi.
-Hatumii pombe, sigara wala kilevi chochote, sio mtu wa kwenda bar/club.
-Ana hofu ya mungu.