Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Pole huyo mkeo hayupo makini. Vitu kama socks ukishaanua zinaunganishwa pamoja ili zisipotee. Na ni vyema ukawa na sehemu maalumu ya kuzihifadhi.
 
Pole huyo mkeo hayupo makini. Vitu kama socks ukishaanua zinaunganishwa pamoja ili zisipotee. Na ni vyema ukawa na sehemu maalumu ya kuzihifadhi.
Mbona hata mimi naweza nikaweka kitu mahali na baada ya muda nikasahau?siwezi kusema hayupo makini kwa sababu ukiondoa hizi changamoto chache vingine vyote anavifanya kwa usahihi,anajitambua kama mke na mama ndani ya nyumba.

Ni kusema hizi kwa kiasi kidogo sana huwa ni kero lakini huwezi kuziita ni kero wakati yale ya msingi anayafanya correctly,zamani nilikuwa naongea sana kuhusu vitu kama hivi lakini nilipoona havibadiliki nikaachana navyo maisha yanaenda.
 
Kwa upande wangu sina mke kwa sasa, lakini nina mpenzi, nampenda sana, ila huwa ananichekeshaga sana.

1. Ana hasira za karibu(Plus ukorofi)
-kipindi ambacho anakujaga kuishi kwangu huwa anafanya vitu vinanikera sana hadi sometimes nachekaga tuu, ana sura ya kitoto, sauti ya kitoto, ni mfupi, yaan basically ni mtoto ndo maana hata akinikera nashindwa hata cha kumfanya mwishowe nacheka tuu.
-huwaga mara nyingi nachelewaga kurudi, sasa yeye hataki nichelewe kurudi, hataki kabisaaa, na ukimwambia nilikuwa sehemu flani hataki, yeye anachojua mm nilikuwa na wanawake wengine, hii inampelekea kufoka, kununa(sunajua zile morning drama, yaan asubuhi anawasha generator, halizimiki hata useme nn) pamoja na kushtaki kwa mama angu, sasa kuna siku hio sitoisahau, tulikuwa tunabishana akanimwagia maji usoni, aisee nilikasirika vibaya mno, aligundua nimekasirika akaanza kujiliiza, ugomvi wenyew ulikuwa ni wa kijinga sana, huwaga anafanya mambo kwa hasira alaf badae anaanza kujuta.

2. Anapenda kulia
-Baada ya kukukera, ukianza kuja juu analia, atalia hapo nusu saa nzima, Kitu kidogo tuu analia, na akianza kulia atakukumbushia mambo uliyomfanyia miezi sita iliyopita, na analia kokote hachagui sehemu ya kulia, barabarani, kweny mgahawa, kanisani etc
-Kuna siku tulikuwa kweny mkusanyiko wa watu akaanza kulia hadi watu wakawa wanatuangalia, na ukimbembelea ndo unachochea.
-Yaan ukimkosea analia na akikukosea wewe bado analia yeye, hadi leo bado sijaelewa hio kitu ikoje.

3. Anaongea sana
-Ila sikuiz nishamzoea, akianza kuongea naweka simu chini naanza kumsikiliza, anapenda sana kuniadisia mambo yake, na akianza kuadisia hamalizi, huwa sometimes hadi nasinzia, utakuta ananishtua anasema "mbona unalala au nakuboa?" sasa ole wako useme "Ndio", utazalisha kesi nyingine na mwisho wake ni vilio.

Mazuri yake;
-Anapatana sana na mama yangu.
-Ananipaga ushauri mzuri.
-Ni msafi.
-Pamoja na kuwa mkorofi anajua wapi amekosea na anaomba msamaha
-Ana maisha yake, hapendi kuiga watu.
-Anajiheshimu sana, havai nusu uchi.
-Hatumii pombe, sigara wala kilevi chochote, sio mtu wa kwenda bar/club.
-Ana hofu ya mungu.
 
Huyu ana vumilika unless kama ana chepuka ni tatizo..
 


You have the best wife brother, Mshukuru Mungu sana na mthamni.
 
Mie nikijua nimeyabananga, naomba tu msamaha, kwani neno lenyewe halinikati hata pumzi.

We kama ni muomba msamaha mzuri, uje nikuoe rafiki yangu, mkewe kiswaswadu, hajui kukosea, hajui kuomba msamaha. 😂🤣
mi kwenye mahusiano nakuwaga mdogo sana ila sio kwenye maisha mengine hapo kuuomba msamaha sio rahisi kabisa,

kuna neno asante, pole na samahani haya matatu husaidia kudumisha mahusiano au kubomoa
 
Safi sana hakika mko vizuri

katabia kakununa tunako wengi hata mie ninako tena sana 😂kananikera kila mara najisemea sitanuna tena lakinj ndo yesheyesheyeshe, narudi kule kule na naona kabisa inavyomnyima raha ila ndo mambo ya drama tena, itabidi nikaombewe aisee
 
Mungu akupe nini tena ndg gunia la chawa? Hizo drama tunazo wanawake wengi na huwa tunazifanya tukiwa na mwanaume huyo 1, ukiona ke alikuwa hivyo then akaacha ujue mko zaidi ya mmoja hivyo mnamuweka bize kiasi hana muda wa drama, hii ni siri nawaibia chunguzeni ex wenu mliowafumania mtagundua hilo hawakuwa na hizo drama, sie wanawake drama na mapenzi ya kweli hutembea pamoja
 
Hii ni Chai tena baridiiiiiiiiiiiiiiii. Hizi ni ndoto zako unazoota unatupiga sound hakuna mwanaume wa namna hii tena wa kiafrika na kama yupo basi atakuwa na shida ya akili au lah, jamaa wanamtindua. Kwa umri wangu wa miaka 40's ndio nimesoma na kujua kuw kuna mwanaume tena mme wa mtu ana hizi tabia. Pole hapo ke wawili wanaishi pamoja.
 
Maisha ya tamthilia za kifilipino hayo. Mbona sisi huku kwetu Mbeya hakuna wanawke wenye hizo mambo. Maandishi yanaelezea umri na tabia ya mtu.
 
Umebahatika kuwa na mke mzuri! Hizi ni tabia nzuri kwa mke material hasahasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…