Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Wakuuu habari za usiku.

Moja kwa Moja twende kwenye maada. Mimi kwa upande wangu mapungu yafuatayo kitoka kwa mama watoto wangu nimekubali KUISHI NAYO.

1. Kuto pokea simu.
Mke wa Mimi hapokei simu hata aione inaita hataahughulika NAYO Hadi amalize shughuli zake. Ukimpigia simu asipo pokea usijisumbue kutuma sms,ukituma Kuna siku utaisoma mwenyewe.

2. Dawa ya mswaki.
Kwenye matumizi ya hii KITU yeye huminya popote pale.

3. Kijichanganya na WATU.

4. Ukimkosea hakiulizi na haoneshi kama amechukia ila utaulizwa siku nyingine na atawasilisha kwa njia ya utani.

5. Akikukosea ukiuliza atakuambia nisamehe baba......... hapo hata uongee vipi hatakujibu.
Hapendi kabisaa kijichanganya na WATU hasa ukitaka umuudhi fika nyumbani Anza kumwongelea mtu hapendi kabisaa na anachukia kwa dhati.

Haya ndo baadhi ya mambo ambayo nimeamua KUISHI NAYO na nimefamikiwa KUISHI NAYO kwa muda wa miaka 19 ya ndoa yetu.
Usalitiii......mpk kuzaaa,naumia but namuomba Mungu anope aman
 
Bora wewe unajibiwa asante baba, wengine ni wanabisha hawajakosea na wako sahihi.. 🤣😂
Ukishinda hoja utaambiwa basi yaishe.
Nina mwanangu ana majanga, wakati mwingine unaona hata aibu kumtembelea nyumbani kwake.
Mkewe ana kaujeri kakimya kimya, ukimuona ni mpole lakini ni mjeuri kinoooma, mwanangu anapata tabu saana, kuna muda anafikiria kumuacha.

Mie wangu ni kutaka kujua kila kitu in details, ananiboa saana, chochote kile atataka in details, hata apige simu mtu akuongeleshe atakuuliza nani huyo, ndio yupi. 😂🤣 Unamuliza utamjuaje sasa, hata nikikutajia fulani huwezi kumjua 😂, sijui ni kupenda kuongea na simu au vipi
Hata umpelekee zawadi atataka kujua yoote, kama umekopa, umemnunulia na sh ngapi, unajiuliza we unataka kujua nini, yaani ni shughuli pevu 😂
Kingine anapenda mnoo kuongea na simu, bora muwe karibu hii inasaidia, akiwa mbali anapiga simu ataongea mpaka stori zaitaisha, mie mvivu kubonga na FONI naishia kuweka loudspeaker tu.
Sometimes hana stori, anakupihia anakwambia mwanao anakuita, sasa mtoto Mwenyewe ndio bado hajatimiza mwaka vizuri, kuongea haongei, unajua tu hapa nimemisiwa.

Mengine madogo madogo, yanachangiwa na maisha yangu ya awali.
Elewa neno AWALI. lizingatie vema.
Kwahiyo ndio umekuja kunisimanga huku?
 
Ni mbaya sana, nilikuwa hivyo kutokusoma sms na kupokea simu yaani naweza masaa nisiguse simu,


Sasa kuna siku dogo alikuwa anaumwa na homa imemuanzia shule,mama yupo mbali kapewa taarifa ananipigia sipokei na dogo hali si shwari kapelekwa hospital,

Mama alimpigia mtu wa mbali na nyumbani na kumuambia aje aniambie nipokee simu[emoji23], kutizama simu imepigwa hatari


,kumtafuta akaniambia ipo siku utafuatwa na kuulizwa marehemu mama yako utazika hapahapa au utasafirisha[emoji15], aisee toka siku hiyo nipo makini,

na bora anipigie sipatikani lkn sio kutokupokelewa anakerwa.
Nashukuru mkuu nitamwonesha hii ujumbe
 
[emoji3][emoji3] huyu mapungufu yake mazuri hayaboi, hapo kwenye kutupa kikombe cha chai ili upokee simu yake mi hoi[emoji3][emoji3]

Yaan ukiona call yake ni kama mama Samia kakupigia no excuse na video call juu hili swala nishaliongea sana kuwa mtu asisipokea simu ni kawaida atakurudia bado sieleweki
Ushawah omba msamaha kuwa umepitiwa na usingizi,ananijua nikiegesha fuvu kitandani basi usingizi unanimeza lakin naambiwa kwanin sijapokea simu inabidi niombe Radhi ,wakati kupitiwa usingizi sio jambo la hiyari inatokea tu umepitiwa jamani
Wivuuuu miwivuuu
 
Hii sjaelewa,Kwan dawa za mswaki Zina sehemu ya kubinyia?
Ndio Mkuu, vile unaminya dawa ya meno kunaongea vile ulivyo. Kuna watu wanabinya kati kati, wengine juu, wengine mwisho na wengine mwisho alafu wanaikunja.

Nadhani mdau aliyelalamika ni hawa wakuminya mwisho ya tube, huwa ni watu wataratibu, makini na wenye utulivu kwenye mipango yao. No wonder analalamika.

Ukijichunguza utagundua huwa kuna mahali unabinya hiyo tube ya dawa kila siku.
 
Muhurumie jamani mtoto wa mwanamke mwenzio 😀😀
Acha aipate pate, anafurahisha sana namuhurumia asipate magonjwa tu, yani kila nifanyacho lazima atake kukijua simu isipopokelewa nijielezee kwa kina, kila siku nina kazi ya kusema ratiba yangu bila hivyo ni kesi tena kesi nzito sio masihara alishawahi nishtaki kwa mlezi wangu km mzazi tu kikesi cha kijinga hadi aibu,
 
Shoga wivu hauna umri
Nami huwa nacheka aisee ananiambia cheka tu unacheka nin sasa [emoji23][emoji23][emoji23]
Hakikisha wakati wa kucheka asikuone, wivu ndo mapenzi ila hawa wetu wamezidi japokuwa mi nimezoea akianza kutweta kama mjusi😂😂namsikiliza halafu nampa maelezo kesi ikiisha,,natafuta kanafasi kakucheka, k iheshimiwe na watu wote
 
Ndio Mkuu, vile unaminya dawa ya meno kunaongea vile ulivyo. Kuna watu wanabinya kati kati, wengine juu, wengine mwisho na wengine mwisho alafu wanaikunja.

Nadhani mdau aliyelalamika ni hawa wakuminya mwisho ya tube, huwa ni watu wataratibu, makini na wenye utulivu kwenye mipango yao. No wonder analalamika.

Ukijichunguza utagundua huwa kuna mahali unabinya hiyo tube ya dawa kila siku.
Nakubaliana nawewe kuwa Kila mtu ana sehemu aliyozoea kubinyia lakini nakataa kuwa Kuna sehemu special ya kubinyia na kuwa Kuna uhusiano Kati ya sehemu ya kubinyia na tabia ya mtu
 
Back
Top Bottom