Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Usalitiii......mpk kuzaaa,naumia but namuomba Mungu anope aman
 
Kwahiyo ndio umekuja kunisimanga huku?
 
Nashukuru mkuu nitamwonesha hii ujumbe
 
[emoji3][emoji3] huyu mapungufu yake mazuri hayaboi, hapo kwenye kutupa kikombe cha chai ili upokee simu yake mi hoi[emoji3][emoji3]

Yaan ukiona call yake ni kama mama Samia kakupigia no excuse na video call juu hili swala nishaliongea sana kuwa mtu asisipokea simu ni kawaida atakurudia bado sieleweki
Ushawah omba msamaha kuwa umepitiwa na usingizi,ananijua nikiegesha fuvu kitandani basi usingizi unanimeza lakin naambiwa kwanin sijapokea simu inabidi niombe Radhi ,wakati kupitiwa usingizi sio jambo la hiyari inatokea tu umepitiwa jamani
Wivuuuu miwivuuu
 
Hii sjaelewa,Kwan dawa za mswaki Zina sehemu ya kubinyia?
Ndio Mkuu, vile unaminya dawa ya meno kunaongea vile ulivyo. Kuna watu wanabinya kati kati, wengine juu, wengine mwisho na wengine mwisho alafu wanaikunja.

Nadhani mdau aliyelalamika ni hawa wakuminya mwisho ya tube, huwa ni watu wataratibu, makini na wenye utulivu kwenye mipango yao. No wonder analalamika.

Ukijichunguza utagundua huwa kuna mahali unabinya hiyo tube ya dawa kila siku.
 
Muhurumie jamani mtoto wa mwanamke mwenzio 😀😀
Acha aipate pate, anafurahisha sana namuhurumia asipate magonjwa tu, yani kila nifanyacho lazima atake kukijua simu isipopokelewa nijielezee kwa kina, kila siku nina kazi ya kusema ratiba yangu bila hivyo ni kesi tena kesi nzito sio masihara alishawahi nishtaki kwa mlezi wangu km mzazi tu kikesi cha kijinga hadi aibu,
 
Shoga wivu hauna umri
Nami huwa nacheka aisee ananiambia cheka tu unacheka nin sasa [emoji23][emoji23][emoji23]
Hakikisha wakati wa kucheka asikuone, wivu ndo mapenzi ila hawa wetu wamezidi japokuwa mi nimezoea akianza kutweta kama mjusi😂😂namsikiliza halafu nampa maelezo kesi ikiisha,,natafuta kanafasi kakucheka, k iheshimiwe na watu wote
 
Nakubaliana nawewe kuwa Kila mtu ana sehemu aliyozoea kubinyia lakini nakataa kuwa Kuna sehemu special ya kubinyia na kuwa Kuna uhusiano Kati ya sehemu ya kubinyia na tabia ya mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…