Tunazungumzia bongo ambapo Dar muuguzi alirekodiwa akiosha vifaatiba kwa majichumvi ya bombani, kisha vingetumika kwa mgonjwa mwingine baada ya yule wa mwanzo.
Tunaisema bongo ambapo vituo kadhaa vya afya mwaka huu vimegundulika kutumia friji za kutunzia nyanya kuhifadhia damu. Wakati kwingine damu inatengwa components zake na inahifadhiwa kwenye friji maalum za damu, sisi kuna watumishi damu wananunua friji la Mr. UK au Boss pale Kariakoo wanatia damu humo.
Na uko unakosoma mtandaoni wagonjwa wanatumia gharama kubwa kujikinga na madhara, ndio maana mtu akitoa figo hupewa kitita cha fedha ya kujikimu.
Lifestyle pale itabadilika, sasa wewe unatoa figo alafu siku ukiumwa kichwa unaenda kununua Panadol za 200 duka la mangi. Panadol zimetengenezwa Vingunguti ambapo ukizipeleka Uingereza au Ujerumani wakizipima unaweza fungwa jela.
Unakunywa dawa ukikojoa unasikia harufu yake, wakati una figo moja we unadhani kuna maisha hapo. Wakati wenye hela wanatumia painkillers za Pfizer au Moderna vidonge vitano laki. Ukitoka hapo unagoogle kuona utaishi miaka mingapi, aaah bongo unahisi kwanini tuna life expectancy ya miaka 66 na Japan wana 85?