Ni mashine gani ambayo ukiipata itafungua njia zako za kibiashara?

Ni mashine gani ambayo ukiipata itafungua njia zako za kibiashara?

Me nikipata frige na brenda ya kutengenezea juice nahisi maisha yangu yatanyooka faster kuna sehemu nimeichungulia furusa buwa na wahitaji ni wengi, hata nikipata used kwa bei powa nitafurahi naamini baada ya mda mfupi hera yangu itarudi na faida juu
Upo mkoa gani?
 
Napitia nyuzi sioni wadau wanataja zile mashine za kujaza hewa matairi ya pikipiki, guta, bajaji,
Zinauzwa Bei gani zile!
Nahisi Kama nazo Ni mchongo bomba wa kijasiriamali
Aina hii
download.jpg
 
Kila mtu ana ndoto ya kuwa na mradi mkubwa wa biashara.

Lakini lazima tukubali ili ufike sehemu lazima uanzie somewhere.

Kwa wajasiriamali wengi huwa tunatamani ukipata mashine au kifaa fulani basi itakufungulia milango na kukusogeza sehemu kuzifikia ndogo zako.

Mimi moja ya mashine nayotamani kuimiliki ni ya kutengeneza bahasha au vifungashio vya karatasi.

Naamini soko lake sio la kutafuta na ukishaipata mashine production yake haiitaji nguvu kazi kubwa.

Mimi nikiipata hii mashine wateja wangu watakuwa corporate nitakuwa natengeneza bahasha za barua size kubwa mpaka ndogo kabisa na nikipata tenda nitakuwa naweka na logo ya kampuni husika.

Wateja wengine ni wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya vifungashio.

Sijajua bongo kama zinatengenezwa ila nimeshahangaika sijazipata ila ukiangiza China zinaanzia bei mil 1.5 kwa ambazo sio express wala auto.

Tutajie mashine yako unayoitamani...

View attachment 2237802
Mashine ya kusindika bangi.
 
Hivi wakuu kuna machine ya kuvuna or kupiga piga mpunga baada ya kukatwa/kuvunwa? Inaweza kuwa sh ngapi? Natamani niipeleke kijijini kwetu, iwarahisishie kazi wakati pia nikipiga pesa
 
Back
Top Bottom