Ni mashine gani hapa mjini ukiwa nayo unaweza kujipatia 50000/-isiyo na presha kwa siku?

Ni mashine gani hapa mjini ukiwa nayo unaweza kujipatia 50000/-isiyo na presha kwa siku?

Nimeona fursa kwenye hii kwa mkoa ambao nipo na kijana wangu alikua akinielezea nikaona wazo lake sio mbaya, na inafaa sana kwenye kazi za metal fabrications, vupuri na mechanical modifications kwa ujumla.


DSC01073_1.jpg


Tukifika na huku tutakua tumepiga hatua japo kwa uchache.
CNC milling machines ni habari nyingine, ingawa zinahitaji mitaji mikubwa sana na highly skilled operators.

Pia nimegundua tuna changamoto ya kutopenda kujifunza kwa watanzania wengi, mfano kwenye metal fabrication asilimia kubwa ya vijana wanalipua kazi, ni watu wakuangalia sana pesa kuliko ubora wa kazi, mtu anatumia muda mwingi kulipua kazi kuliko kunoa ujuzi na ubobezi.
 
Kuna changamoto yeyote kuwa na ya solar?..naomba kujua Bei yake please. Hasa kwa mkoa wa Arusha
Iko hivi.
Mashine ya popcorn inatakiwa kuzalisha moto ili kutengeneza popcorns.

Katika nishati ya umeme, vifaa vinavyozalisha moto/joto huambatana na utumizi mkubwa nishati.

Hivyo basi ukinunua mashine ya solar inabidi ufanye ukokotozi wa kiasi cha nishati unachohitaji kufanya kazi zako kwa siku nzima bila kukwama.
Ninachohofia utajikuta unabeba mzigo mkubwa wa battery kwa ajili ya backup ya siku nzima.
 
Tafuta water pump au mashine ya kushindilia au pia compressor.

NB: Ukiwa nazo zote ni uhakika hukosi hata 500k per month katika nyakati mbaya. Kipindi kizuri unaeza kunja mpaka 2ml per month.
Hello. Mfano hizi machine unatakiwa kununua ukiwa karibu ya makazi gani? Au location itafaa Sana wapi?
 
Hello. Mfano hizi machine unatakiwa kununua ukiwa karibu ya makazi gani? Au location itafaa Sana wapi?
Kununua mashine yeyote kwa ajili ya biashara inategemea na upembuzi uliofanya kwa eneo ulipo.

Angalia mazingira uliyopo kuna changamoto zipi?

Changamoto zilizopo kwenye jamii yako ndio fursa yako ya kiuchumi, unazitatuaje aidha kwa kutoa huduma nzuri zaidi kuliko zilizopo tayari, au kwa gharama ya chini zaidi huku ukijiendesha kwa faida.
 
on progress, kwa sasa najifunza stencils yaani wall stencil,furniture stencil na craft stencil naona ina soko sana watu wanapenda urembo wa nyumba hawajengi kizamani
Miss Gf ufafanuzi tafadhali hapo unaposema "Watu wanapenda urembo wa nyumba hawajengi kizamani"
 
kupata elfu hamsini uwe na cpompressor kama tano maeneo tofautina makorokoro yote ya pancha kila kijana au kijiwe wakulipe elfu 10 kila siku.....
au ufungue tire service cente weka mashine za viraka vya moto,mashine za kuvua na kuvisha tire na spana ya upepo(auto) good location unaokota hio 50k per day...to my expirience...
 
Back
Top Bottom