Ni matumaini yangu wana CHADEMA wote si tu mmemsikia bali mmemuelewa vyema tu Kada wa CCM Pascal Mayalla

Hivi kwa mfano unawezaje kuhamasisha wananchi unao waongoza wawe na tabia njema wakati wewe mwenyewe dhahiri shahiri una tabia mbaya. Eti unajitetea kwamba kama una tabia mbaya mapolisi/mahakama itakufunga hivyo wasikuhoji hilo! Emu jaribu kufikiri kwa mapana na si kimbinyio ( narrow ).
 
Paskali hasomeki...utahusianisha vipi Katiba Ya Nchi na CHADEMA....Inakuwa ngumu kuaminika hata kwenye teuzi.....
 
Kuna kitu kwenye hitaji la Katiba mpya tunajidanganya na bahati mbaya bado hatujajua kuwa tunafanya utoto.
Hivi tumefanya utafiti Watanzania ambao watapigia kura katiba itakayopendekezwa wamefikia kiwango cha kujua umuhimu wa yale mambo ya msingi tunayolilia mfano Tume huru ya uchaguzi, mamlaka ya Rais, Serikali tatu?
Kwa jinsi Watanzania walivyo bila kutumia muda wa kuwaelimisha basi nakuambia hivyo vipengele CCM na vikundi vyake vya kihuni wanaenda kushinda mchana kweupe kuwarubuni Wananchi waikatae kweupe hapo mlichokitaka mtakuwa mmekipata.
Kazi ianze kuelimisha jamii kwa ukubwa wake, ila kutegemea sauti za wasomi pekee wanaojua maana ya katiba mpya hiyo kitu haipiti kwani haki ya kupiga kura haipo kwa wasomi tu.
Ili katiba mpya yenye manufaa ipatikane lazima hitaji hilo liwaguse CCM na si vinginevyo, yani kuwe na sauti moja kati ya wananchi na CCM(hawa sio wananchi bali kikundi cha mbwa mwitu).
Kinyume chake CCM wanaweza kuridhia mchakato halafu wakaja kushinda kwenye kura za ndio na hapana na hapo ndio tutakuwa tumepiga pasi ya mwisho kuwaruhusu CCM wakatawale tena.
 
Njaa itamuingiza Paschal kwenye uhalifu,namuomba mama ampe u DAS kabla hajaanza kazi yake ya awali
 
Ungefikiri wewe kwa mapana mana huo mfano wako haupo kwa uhalisia hapo tunazungumzia Katiba ambayo inaeleza kila kitu kifanyike.
Wewe umeleta mfano ambao haupo jibu hoja kwa hoja sio kwa mifano ya kuokota.
Jitaidi kufikiri nje box( shallow mind).
 
Mkuu unajichanganya, kwenye maandishi yako, unadhamiria kuonyesha umuhimu wa Katiba mpya ya wananchi

Au unataka kuwachamba chadema kupitia mgongo wa Katiba mpya

Tukiwa na katiba mpya na ikatokeaCcm au chadema vikafa vyote na kupotea the better, sisi hatujali
 
Jana nilikuona vizuri sana kwenye ule mjadala, ushauri wako haukuwa wa kiufundi bali wa kikada wa ccm. Kwa bahati mbaya hata hao cdm hawahitaji ushauri wako, japo una amini kuwa una mawazo mazuri ya kuwasaida cdm. Kama kweli ww ni mshauri mzuri, kuna vyama kama TLP, CUF, NCCR nk kawashauri. Ama kwakuwa pia ww ni mwanahabari, nenda kawasaidie vyombo vya habari viachwe kuminywa au nenda huko mahakamani unakowashauri cdm waende.

Uzuri ni kuwa mpaka sasa cdm wamefanikiwa mambo mengi bila ushauri wako , na hiyo katiba mpya wataidai kwa shinikizo, kwani bila hivyo hawatoipata. Ww nenda mahakamani kaidai katiba mpya maana hata ww unajua itapatikana.
 
Krav Maga CHADEMA huwa haijibishani na watu bali hujibu chochote kwa mikakati endelevu...Kumjibu yoyote kwenye chochote ni kujitoa kwenye reli
CDM haifanyi kazi mitazamo ya watu mitandaoni kama kuna lolote la muhimu kukihusu chama kuna utaratibu ndani ya chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…