Ni matumaini yangu wana CHADEMA wote si tu mmemsikia bali mmemuelewa vyema tu Kada wa CCM Pascal Mayalla

Ni matumaini yangu wana CHADEMA wote si tu mmemsikia bali mmemuelewa vyema tu Kada wa CCM Pascal Mayalla

Sorry nachoelewa ni kwamba CHADEMA,,,CCM,,,ACT au vyama vyote vya siasa vitapita lakini TANZANIA itabaki milele. Ivyo au ni kwamba Katiba mpya ni kwa manufaa ya chadema au nchi nzima.
Ni kama nchi nzima basi hayo madhaifu ya chadema hayana mantiki Katika Katiba mpya.
Chadema kuvunja Katiba yao tumuachie msajili wa vyama,,yeye ndio anapaswa achukue hatua.
Hivi kwa mfano unawezaje kuhamasisha wananchi unao waongoza wawe na tabia njema wakati wewe mwenyewe dhahiri shahiri una tabia mbaya. Eti unajitetea kwamba kama una tabia mbaya mapolisi/mahakama itakufunga hivyo wasikuhoji hilo! Emu jaribu kufikiri kwa mapana na si kimbinyio ( narrow ).
 
Paskali hasomeki...utahusianisha vipi Katiba Ya Nchi na CHADEMA....Inakuwa ngumu kuaminika hata kwenye teuzi.....
 
Kuna kitu kwenye hitaji la Katiba mpya tunajidanganya na bahati mbaya bado hatujajua kuwa tunafanya utoto.
Hivi tumefanya utafiti Watanzania ambao watapigia kura katiba itakayopendekezwa wamefikia kiwango cha kujua umuhimu wa yale mambo ya msingi tunayolilia mfano Tume huru ya uchaguzi, mamlaka ya Rais, Serikali tatu?
Kwa jinsi Watanzania walivyo bila kutumia muda wa kuwaelimisha basi nakuambia hivyo vipengele CCM na vikundi vyake vya kihuni wanaenda kushinda mchana kweupe kuwarubuni Wananchi waikatae kweupe hapo mlichokitaka mtakuwa mmekipata.
Kazi ianze kuelimisha jamii kwa ukubwa wake, ila kutegemea sauti za wasomi pekee wanaojua maana ya katiba mpya hiyo kitu haipiti kwani haki ya kupiga kura haipo kwa wasomi tu.
Ili katiba mpya yenye manufaa ipatikane lazima hitaji hilo liwaguse CCM na si vinginevyo, yani kuwe na sauti moja kati ya wananchi na CCM(hawa sio wananchi bali kikundi cha mbwa mwitu).
Kinyume chake CCM wanaweza kuridhia mchakato halafu wakaja kushinda kwenye kura za ndio na hapana na hapo ndio tutakuwa tumepiga pasi ya mwisho kuwaruhusu CCM wakatawale tena.
 
Njaa itamuingiza Paschal kwenye uhalifu,namuomba mama ampe u DAS kabla hajaanza kazi yake ya awali
 
Hivi kwa mfano unawezaje kuhamasisha wananchi unao waongoza wawe na tabia njema wakati wewe mwenyewe dhahiri shahiri una tabia mbaya. Eti unajitetea kwamba kama una tabia mbaya mapolisi/mahakama itakufunga hivyo wasikuhoji hilo! Emu jaribu kufikiri kwa mapana na si kimbinyio ( narrow ).
Ungefikiri wewe kwa mapana mana huo mfano wako haupo kwa uhalisia hapo tunazungumzia Katiba ambayo inaeleza kila kitu kifanyike.
Wewe umeleta mfano ambao haupo jibu hoja kwa hoja sio kwa mifano ya kuokota.
Jitaidi kufikiri nje box( shallow mind).
 
Katiba ni ya wananchi na hitaji la katiba mpya ni hitaji la wananchi, ila ili kuipata hiyo katiba mpya ni mchakato wa kujenga hoja zenye nguvu ya hoja na sio hoja za nguvu.

Chadema wameamua kutumia hoja za nguvu, kupiga kelele na kususa ili kushinikiza, down the drain, they will go...6ft under!.
P
Mkuu unajichanganya, kwenye maandishi yako, unadhamiria kuonyesha umuhimu wa Katiba mpya ya wananchi

Au unataka kuwachamba chadema kupitia mgongo wa Katiba mpya

Tukiwa na katiba mpya na ikatokeaCcm au chadema vikafa vyote na kupotea the better, sisi hatujali
 
Jana nilikuona vizuri sana kwenye ule mjadala, ushauri wako haukuwa wa kiufundi bali wa kikada wa ccm. Kwa bahati mbaya hata hao cdm hawahitaji ushauri wako, japo una amini kuwa una mawazo mazuri ya kuwasaida cdm. Kama kweli ww ni mshauri mzuri, kuna vyama kama TLP, CUF, NCCR nk kawashauri. Ama kwakuwa pia ww ni mwanahabari, nenda kawasaidie vyombo vya habari viachwe kuminywa au nenda huko mahakamani unakowashauri cdm waende.

Uzuri ni kuwa mpaka sasa cdm wamefanikiwa mambo mengi bila ushauri wako , na hiyo katiba mpya wataidai kwa shinikizo, kwani bila hivyo hawatoipata. Ww nenda mahakamani kaidai katiba mpya maana hata ww unajua itapatikana.
 
" Ili CHADEMA tuwaamini kuwa AGENDA yao ya Kudai Katiba Mpya ina Mashiko na wana Hoja ya Msingi hebu wao kama Chama waanze Kwanza kuonyesha kuwa wanaheshimu Katiba ndani ya Chama chao ambapo kuna uvunjifu mkubwa tu wa Katiba " Pascal Mayalla

Nukuu hii nimeitoa baada ya Kumsikia na Kumtizama jana Usiku Star Tv akiwa Mgeni rasmi kwa Dar es Salaam katika Kipindi kilichokuwa Kinasimamiwa na Mtozi Aloyce Nyanda.

Najua hapa JamiiForums kuna wana CHADEMA wengi tu na wale walio Neutral kama Mimi Krav Maga hivyo kwa pamoja ama tutaweza Kukubaliana nae au Kumpinga kwa Hoja.

Na wakati mnamjibu mwana CCM Pascal Mayalla kumbukeni kuwa huyu ni Msomi wa Fani nyingi nchini Tanzania za Habari na Sheria, Mjasiriamali mkubwa, Mjuaji wa Mambo mengi nchini Tanzania, Member Mkongwe JamiiForums, Mwanasiasa mwenye Mafanikio na Mtu mwenye Network kubwa sana ya Viongozi ( Watawala ) wa Tanzania hii na huenda hata katika Teuzi zijazo za DC au DED safari hii akawemo.
Krav Maga CHADEMA huwa haijibishani na watu bali hujibu chochote kwa mikakati endelevu...Kumjibu yoyote kwenye chochote ni kujitoa kwenye reli
CDM haifanyi kazi mitazamo ya watu mitandaoni kama kuna lolote la muhimu kukihusu chama kuna utaratibu ndani ya chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom