Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kweli ujinga ni kipaji.The Magufuli Legacy
Hakuna shaka wala ubishi kuwa miradi ya kufua umeme Bwawa la Mwl Nyerere na SGR ikianza kazi ni uamuzi wa Magufuli ambao utabaki katika historia ya WaTz ikiwa ni pamoja na kuhamishia Makao Makuu ya nchi Dodoma. Magufuli Legacy
Hivi hapo cha ajabu ni nini alichokifanya ambacho kilikuwa hakijawahi kufanyika?
1) Hivi TAZARA na reli ya kati siyo reli?
2) Hivi, Mtera, Kidatu, Kihansi, siyo mabwawa?
Jambo pekee alilolifanya ni kuhamishia makao makuu Dodoma, ambalo kwa teknolojia ya Ulimwengu wa sasa, hakuna chochote tutakachoongeza.
Hivyo vingine vyote vilifanyika wakati wa watangulizi wake. Tena walivianzisha na vikakamilika.
Mahaba yakizidi, hufifisha akili. Ukianza kuorodhesha yaliyofanyika wakati wa JPM, kiuhalisia ni machache na madogo kuliko yaliyofanyika wakati wa baadhi ya watangulizi wake.
Kikubwa alichofanikiwa marehemu kuliko mtangulizi wake yeyote, ni kutengeneza kundi kubwa la wajinga wa kumwabudu na kumsifia kwa kila alilolifanya hata likiwa dogo kiasi gani na kulifanya lionekane ni kubwa la ajabu.