Ni mfu, ajabu nderemo zake zina ujazo kuzidi walio hai. Kwanini?

Ni mfu, ajabu nderemo zake zina ujazo kuzidi walio hai. Kwanini?

View attachment 2454555

Leo tena mfu hapo juu amepokea nderemo za kutosha na zisizo elezeka kutoka kwenye hadhira fulani kila lilipotajwa jina lake. Ajabu!

Ni wazi ipo haja kwa tusiompenda huyo jamaa tujiulize ni wapi anapo tuzidi kete ilihali hayupo nasi ajabu bado nderemo kwake zinazidia zetu tulio hai tena mbele ya walio hai wenzetu.

R.I.P JPM.
Wekeni na clip tuone.
 
Shangwe za marehemu tu hizo.

Kwa miila za kiafrika marehemu husifiwa hata kama alikuwa muovu.

Sasa huyu jamaa alikuwa muovu kweli kweli. Ndiyo maana hajaishi (Y. Makamba).
Ujumbe mmeupata.
 
Lilikuwa shamba Sana hili jamaa. Lilipenda sifa za kitoto mnoooo!

Sasa kupigwa picha na.mafaili yoye haya ndiyo nini?
Ukijifungua hilo gubu dhidi ya JPM litakwisha na utakuwa busy kulea kichanga chako
 
Lakini si unafahamu jinsi alivyominya haki ya kupata habari? Hao wote ni watumwa wa ujinga uliotokana na kunyimwa haki yao ya kujua ukweli juu ya uovu aliokuwa akiutendeka.
Kwani wengine habari walizipata wapi kwamba Magufuli ndio muuwaji anauwa hovyo raia?
 
Alishangiliwa na watu wa namna gani? Maana Afrika wajinga na wasio na akili ni wengi kuliko wenye akili.

Fikiria huko Uganda, hakuna Rais aliyewahi kubebwa na kushangiliwa kama Idd Amin Dada. Wewe unafikiri Afrika limekuwa bara la giza kwa bahati mbaya? Giza linaanzia vichwani mwa walio wengi.

Si ulishuhudia hapa kwetu kuna wakati shetani alitoa amri Lisu auawe kwa risasi, na kweli alitandikwa risasi. Kila mwenye akili Duniani alisikitika, lakini kuna Watanzania walishangilia na kumsifu muuaji eti ni kiongozi jasiri.

Shangilio la mwenye akili huashiria ubora lakini shangilio la mwendawazimu huashiria aibu.
Labda kwa kuwasaidia hao watanzania wenzako katika kuwatoa ujinga ungewawekea ushahidi kabisa usio na shaka kuthibitisha Magufuli alitoa hilo agizo, pengine hapo ndio wataelewa maana pengine nao wana mtazamo tofauti kuhusu kushambuliwa kwa Lissu.
 
Matendo mema hayamfanyi mtu kuwa Mungu ilo ndio kosa lake
Mungu ni mwenye wivu
 
Ukijifungua hilo gubu dhidi ya JPM litakwisha na utakuwa busy kulea kichanga chako
[emoji23][emoji23][emoji23]Sexless hata mumewe akishindwa kusimamisha ili ampande anamsingizia marehemu Magufuli
 
Hao watu wanampendaje si tunaambiwa alikuwa anauwa na kuwateka? Unataka kuniambia hao watu hawajui kwamba maelfu ya ndugu na jamaa zao waliyotekwa na kuuliwa kwamba aliyefanya hivyo ni Magufuli au wanajua ila wamempenda hivyo hivyo?
Watu wanakupenda ukifa hii ndio Tanzania
Enzi za Magu walisema Bora JK
Enzi za Mama wanasema Bora JPM
Sasa Subir enzi za Mama ziishe ahahah
 
Mwamba from chato mda huu angekuea chato na watumishi mngekuwa mshakura mishahara yenu mpo kujiandaa kwa X Mass,.ila hawa warabu wa zanzibar hawajui x Mass nini mpaka mda huu watumishi mnapiga mihayo tu wameondoa mazoea mliyozoeweshwa 😂😂😂
Tetesi Zina sema pesa hamna hazina huko; tusubiri hii 1.8 trilioni iingie watalipwa tu
 
Magufuli anachukiwa saaaana JF kuliko huko mitaani na mitandao mingine kama twitter, instagram, facebook na platforms nyingine.

Naanza kuhisi kuna IDs zimetengenezwa humu nyingi na mabwanyenye za kumchafua. Cha ajabu huko mtaani hali ni tofauti. Ukitaka uonekane mbaya muongelee vibaya huyu marehem mtaani uone kitakachokukuta.
Ndo unashtuka leo?? Kuna account nyingi sana za serikali humu JF..

Yaani propaganda zao hawana pa kuzipeleka tofauti na JF
 
Hao watu wanampendaje si tunaambiwa alikuwa anauwa na kuwateka? Unataka kuniambia hao watu hawajui kwamba maelfu ya ndugu na jamaa zao waliyotekwa na kuuliwa kwamba aliyefanya hivyo ni Magufuli au wanajua ila wamempenda hivyo hivyo?
Hizo zilikuwa propaganda
 
Lilikuwa shamba Sana hili jamaa. Lilipenda sifa za kitoto mnoooo!

Sasa kupigwa picha na.mafaili yoye haya ndiyo nini?
Duh kwahyo hii nayo ni sababu ambayo mmekaa ofisini pale Lumumba mkaona mkitype hivi mtatushawishi kabisa watanzaAnia Tumchukie??
Mbona mmeishiwa mbinu kabisa
 
Alishangiliwa na watu wa namna gani? Maana Afrika wajinga na wasio na akili ni wengi kuliko wenye akili.

Fikiria huko Uganda, hakuna Rais aliyewahi kubebwa na kushangiliwa kama Idd Amin Dada. Wewe unafikiri Afrika limekuwa bara la giza kwa bahati mbaya? Giza linaanzia vichwani mwa walio wengi.

Si ulishuhudia hapa kwetu kuna wakati shetani alitoa amri Lisu auawe kwa risasi, na kweli alitandikwa risasi. Kila mwenye akili Duniani alisikitika, lakini kuna Watanzania walishangilia na kumsifu muuaji eti ni kiongozi jasiri.

Shangilio la mwenye akili huashiria ubora lakini shangilio la mwendawazimu huashiria aibu.
Ukifuatilia hotuba za IDD utagundua alikuwa raisi bora kabisa. Achana na ile muvi tafuta stori halisi
 
Back
Top Bottom