Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Ukumbini ndio mpango mzima, uwanjani hamna replay, kule labda uende kujaza uwanja
 
Nakuelewa kwanini umeamua kufanya uchaguzi huu. Mungu aturehemu sana. Watu hatujui kazi ya jumuiya kwa ujumla. Jumuiya ilianzia kwa mitume kwenye Matendo ya mitume 2:yote. Ukisoma mstari wa 46 utaelewa kazi ya jumuiya. Na kiukweli matendo yote ukiisoma utaelewa kazi ya jumuiya.

Sasa jumuiya saivi usipoenda huzikwi, hawakujali, hawana muda na wewe, haupati msaada. Kinachoniuma kuna bibi mmoja tuko nae huku. Anasali jumuiya ya kanisa fulani. Kuna muda anaweza kulala na njaa hana chochote. Hio ni story nilioikuta huku.

And too bad kazungukwa na wanajumuiya yake plus wakristo. Sasa ni Kristo yupi tunaemhubiri. Nilitegemea jumuiya tupeleke misaada mtaani kwa watu wenye hali ngumu, tuende kwenye mahospitali, vituo vya yatima, kwa wajane ili kuupeleka upendo wa Kristo kwa matendo.

Lakini cha kuumiza unaweza kuta katika jumuiya kuna mjane na hana maisha. Kuna yatima katika jumuiya kakosa hela ya kwendea shule na mlezi wake hali ngumu..shule anasitisha na bado yuko kwenye jumuiya ambayo ndani yake kuna mtu mwenye fedha. Show me Imani yako bila matendo, nikuoneshe Imani iliyo kwenye matendo.

If we are keen tutakosa mbingu wakristo almost wote. Hata Isaya nadhani aliandika dini ya kweli kabisa ni kwenda kutembelea yatima, wajane, kuwavisha maskini nguo, kuwapa chakula. Lakini nachoona saiv ni maigizo tu. Tujifikirie upys na kuchagua mambo sahihi ya kufanya.
 
Tall mnyama..
Kwani wafupi wamekukosea nini?🤣🤣🤣
 
Kwa hiyo tukusaidiaje?
 
Malengo ya jumuia ni mazuri kabisa ila viongozi wake ndo tatizo. Unakuta wengine ni walimu na wengine ni viongozi wa vyama vya siasa, kwa hiyo wanatoa amri kama kwa waumini kama wanafunzi au makada wa vyama.
GENTAMYCIME tafuta mwongozo wa jumuia utaona malengo Vs viongozi wa jumuia.
 

Kulea roho za watu bila kuwa na roho wa Mungu ni tatizo kubwa sana sio kwetu wakatoliki pekee bali hata kwa madhehebu na dini zingine. Lipo tatizo kubwa la kusimamia mambo ya kwa nguvu za mwilini huku rohoni hawana kitu

Ukikubali kuwa shekhe, padre, mchungaji unayeongoza kundi la waamini zitafute nguvu za rohoni, hekima na upendo viwe miongozo yako na umwombe Mungu ajalie wale unaowaweka kukusaidia kama makatibu, wenyeviti.... kuongoza kwa kufuata yale unayoamini. Vinginevyo badala ya kuwa tumaini lenye faraja kwa watu unaishia kuwa kikwazo na kuumiza watu
 
Nimecheka mno. Naona umeamua kunipiga Dongo Kiana. Haya bhana ila Jumuiya zenu sihudhurii ng'o na Mbinguni kwa Mungu Baba nitafika tu.
Asikutishe mtu! Hakuna mwenye mbingu wala jehanamu ya kukupeleeka!! Neno la Mungu likikuweka huru unakuwa huru kweli kweli!! Kwa sisi wahangaikaji jumamosi ni siku ya uzalishaji!! Fanya kazi zako, shiriki shughuli za kijamii, usimuumize mtu!! Achana na hizo mahakama watu walizoziunda ili kunyanyasa wenzao!!
 
Afu wanadai eti michango ni ya Mungu? Hawa ni wafanyabishara kama wengine tu! Afadhali Hela yangu ya sadaka nimpe yatima au mlemavu barabarani sio haya mambo ya kanisani....kanisani ilipaswa kusiwe na sadaka kabisa.
 
Mimi nasikia nadaiwa viwawa huko hata sielewi. Tena kibabe na kilazima. Katika suala la michango hapana aisee. Too much. Sihudguriagu hata ikiwa inasali kwetu. Wengi naonaga wanafiki tu. Kama mtu siongei nar naenda kusali Mungu si ataniadhibu kwa unafki?
 
Tatizo linakuja pale ambapo Mtu haendi Jumuiya, haendi Kanisani, hatoi michango yoyote ila akipatwa na shida anataka Kanisa limsaidie, nenda Jumuiya kwa ajili ya kusali kama kuna mambo mengine yanakukwaza achana nayo hayo ni mambo ya wanadamu na hakuna aliyemkamilifu.
 
Umetumia kigezo gani kuyaita mawazo yake Ujinga? Au ni hofu zako za kiimani na kidini?.... Amri za kanisa ziliwekwa na nani? Amri za kanisa zibaki kanisani... Uraiani kila mtu na sheria na amri zake wala si kupangiana amri na sheria..kila mtu na sheria zake na maamuzi yake..
 
Ila huladhimishwi kutoa yote japo kutoa hata kidogo kuliko kuacha kabisa na uwezo unao.
 
sawa,hiyo ni jumuiya yako mkuu. Umechukua hatua gani kusaidia hili ?Tatizo halikimbiwi na inawezekana wewe ndiye wa kusaidia kuirudisha jumuiya kwenye mstari wa unyoofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…