Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Umeandika kwa kutizama kwa jicho hasi ila umesahau kuwa jumuiya ni msingi wa imani kwani huwaleta wakristu pamoja kama kanisa moja.Hiyo ni moja ya faida pamoja na faida zingine nyingi ikiwemo kusali pamoja. Kama umeona mapungufu nilitegemea kama mkristu makini ungekuwa wa kwanza kurekebisha kasoro hizo ndogo ndogo na kusisitiza watu wahudhurie!
 
Kuna ULAZIMA gani na upi kuzikwa na ibada? Ina maana hiyo ibada itasaidia nini? Itafuta dhambi zako? Ibada ni Hofu za kidini na kiimani tu! Ukisha kufa umekufa hakuna anaye jua huko uliko nini kina endelea.
 
Kwangu mimi jumuiya ndo mpango mzima, never miss. Ukikua utajua.
 
Kitu pekee kinachofanya waumini washiriki shughuli za kanisa ni "Ukifa,hatukuziki".

Mpaka maparoko kwa sasa mkwara ni huohuo tu.

Mtu akija na huduma ya ibada za mazishi kwa waliosuswa na madhehebu yao,akawa na kwaya na waumini wake atapiga pesa!

BTW:Huku Jumuiya ni Jumatano.
 
Tafuta pesa acha kujilizaliza mambo madogo sana hayo.
Au unataka nani awe analipia zaidi yako wewe muumini.?
 
Tafuta hela ,ukiwa na hela hukosi wa kukuzika watajaa hata wasiokujua ,wapenda kula mtaani watajaa kwenye mahema.Huo ni utaratibu was duniani Mungu hausiki nao
Si kweli.Kumbuka yule bilionea wa Impala Arusha alikataliwa kuzikwa pamoja na utajiri wake
 
Wee toaa tu mkuu usiofu Wala nn to sadaka mengine yatajulikana tu
 
Zaburi 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
² Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
 
Hawa watu bn Padri aligoma kuja kusali kweny mazishi ya baba angu kisa ety alikua ahudhulii hivo vikao vyao vya asubui ety hadi tutoe faini me nkamwambia tu bi mkubwa mine natafuta wasabato waje wamzike mshua angu eeeeh nkatoa taarifa hapo S.D.A haraka haraka wakaja kutuongezea ibada hadi siku ya mazishi
 
Uongo mtupu.Hakunaga hicho kitu RC
 
Aisee wewe ni kichwa. Mimi ni Mlutheri nimetoka kumwambia mke wangu sitaki jumuiya kuanzia leo asubuhi. Shenzi type!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…